Tishio la uhai wetu

Tishio la uhai wetu

Joined
Mar 22, 2018
Posts
12
Reaction score
26
Tishio la uhai wetu na sheria yetu ya mazingira.

Ally buyuknohutcu pamoja na mkewe aysin ni miongoni mwa wanaharakati 207 waliouwawa kikatili kama nguruwe mwaka 2017.Kosa lao kubwa lililopelekea kufanyiwa unyama huo ni Harakati zao za kutetea uhifadhi wa mazingira na kuhakikisha dunia inakuwa sehemu salama ya kuishi.

Kwa mujibu wa shirika la kimataifa la global witness,mwaka 2017 ni mwaka ambao wanaharakati wengi zaidi wa mazingira waliuwawa kikatili.Katika ripoti hiyo nchi ya Brazil imetajwa kama sehemu hatari zaidi Kwa wanaharakati wa mazingira ,ikifuatiwa na ufilipino.

Kwa upande wa nchi yetu Tanzania mauaji haya ya kikatili Kwa wanaharakati wa mazingira sio maarufu sana,japo mwaka 2017 dalili mbaya zilianza kujitokeza hasa baada ya mauaji ya mwanaharakati wa kupinga ujangiri na Biashara haramu ya meno ya tembo comrade Wayne litter.

Tafiti zinaonyesha sababu kubwa inayopelekea vifo Kwa wanaharakati wa mazingira ni maendeleo ya viwanda.Hivyo basi,wakati huu ambao nchi yetu imejikita zaidi kwenye Harakati za kuhakikisha inakuwa nchi ya viwanda,nazani ni muda sahihi wa kuboresha sheria za mazingira,hili kuhakikisha maendeleo haya ya viwanda hayana madhara Kwa mazingira na wananchi Kwa ujumla.

Ni kitu kizuri sana nchi yetu kuwa ya viwanda,ila ni hatari sana nchi yetu kuwa na viwanda bila kuwa na sheria imara za uhifadhi wa mazingira.Mapungufu yote yaliyopo kwenye sheria yetu ya mazingira ya mwaka 2004 ni wakati wake sasa kuyaondoa.

Mjamaa Samwely Kisinga
Msendembali-songea
 
Mbona sijafahamu mahusiano ya hivo vifo vya wanaharakati na maendeleo ya viwanda? Au una ushahidi juu ya sababu zilizopelekea vifo hivo?
 
Back
Top Bottom