Tinubu aagiza polisi wote warudi kulinda raia na si viongozi, Itasaidia kuongeza hali ya usalama nchi humo?

Fascinating

Member
Joined
May 14, 2025
Posts
93
Reaction score
224
Juzi Jumapili, Ikulu ya Abuja ilikuwa kimya lakini ndani kulikuwa kwa moto sana. Rais Tinubu alikuwa amewaita wakuu wote wa vyombo usalama: IG Kayode Egbetokun, DG DSS Tosin Ajayi, Chief of Army Staff Lt-Gen Waidi Shaibu, Chief of Air Staff Air Marshal Sunday Kelvin Aneke. Mkutano haukuchukua muda mrefu. Walipotoka, Agizo lilikuwa tayari ni;
Polisi wote waliokuwa wameambatishwa kama walinzi wa binafsi kwa VIP – wanasiasa, wafanyabiashara, magovernor, maseneta na watu mashughuri. Wameondolewa mara moja.
IMG_2857.webp

Polisi hao wanaondoka kwenye mageti ya vigogo, kwenye kulinda nyumba za kifahari, wanaondoka na kwenye misafara ya viongozi. Na wmeagizwa wanarudi mitaani, vijijini, barabarani, pale wananchi wa kawaida wanapohitaji ulinzi zaidi.
Tinubu aliweka wazi kuwa
Maafisa wengi wa polisi wamekuwa wakilinda watu wachache wenye madaraka na pesa, wakati maeneo mengi ya nchi hayana hata askari mmoja.

Hali ya kiusalama nchini Nigeria imezidi kuwa si shwari kabisa, Hii ni kutokana kuongezeka kwa matukio ya kuhatarisha usalama wa raia kaskazini-mashariki mwa nchi hiyo maeneo ya Borno, Adamawa na Yobe ambapo makundi ya Boko Haram na ISWAP bado yanaendelea kusumbua. Pia kaskazini-magharibi mwa nchi hiyo maeneo ya Zamfara, Katsina, Kaduna, Sokoto na Niger kuna magenge ya waporaji yanayoendelea kuua na kuteeka nyara watu. Hata Katikati na Kusini mwa nchi hiyo katika maeneo kama Rivers, Delta, Bayelsa, hata Lagos na Ogun, wahalifu wa kutumia silaha wamezidi kuwa na matukio ya mala kwa mala ambayo hugharimu maisha ya raia wengi. Wananchi wengi wanaishi kwa hofu, wakulima hawaendi shambani, watoto wengi hawaendi shuleni. Hali ya usalama nchini Nigeria imesababisha vifo zaidi ya 10,000 tangu Rais Tinubu aingie madarakani Mei 2023, lakini 2025 pekee imekuwa mbaya zaidi.
  • Katika nusu ya kwanza ya 2025 (Januari-Juni), watu 2,266 waliuawa na magenge yenye silaha au insurgents (kama Boko Haram na ISWAP), na hii imevuka idadi ya vifo vya 2024 yote. Hii inajumuisha matukio makubwa ya mashambulio dhidi ya raia lile la Septemba 2025 katika kijiji cha Mafa, Yobe, ambapo 170 waliuawa na ISWAP.
  • Kuanzia Mei 2023 hadi Mei 2025, takliban watu 10,217 waliuawa katika majimbo ya Benue, Edo, Katsina, Kebbi, Plateau, Sokoto, na Zamfara kutokana na mashambulizi ya gunmen na magenge. Katika Zamfara pekee, 1,088 waliuawa katika nusu ya kwanza ya 2025. Katsina, zaidi ya 294 waliuawa na 306 walitekwa nyara (wengi wanawake na wasichana) kutoka Mei 2023 hadi Mei 2025. Hii inajumuisha mashambulizi ya kila siku na magenge ya bandits.
  • Borno na Yobe (kaskazini-mashariki), makundi ya Boko Haram na ISWAP wameua mamia, watu 63 waliouawa Septemba 2025, Darul Jamal, Borno, na 170 waliuawa Yobe. Jumla ya vifo vya Boko Haram tangu 2009 ni zaidi ya 350,000, na 2025 inaendelea kuongeza.
Majimbo mengine: Katika Plateau, zaidi ya 100 waliuawa Aprili 2025 katika mashambulizi mawili makubwa; Kaduna na Benue vifo zaidi ya 200 katika mashambulizi moja la Juni 2025.
Kwa jumla, ripoti za Mei 2025 zinaonyesha takliban vifo 6,800 vinavyohusiana na vurugu katika nusu ya kwanza ya mwaka, na idadi inaongezeka kwa kila mwezi.

Machafuko yanachochewa na itakadi za kidini pamoja na nia za kufanya uharifu yamesababisha mamilioni ya watu kuyahama makazi yao kutokana na vurugu na matishio ya kiusalama.
  • Takriban milioni 3 wamehamishwa na vurugu tangu 2023, wengi katika kaskazini-mashariki na magharibi. Borno pekee ina waliohama milioni 1.7 (IDPs) na waliorudi nyumbani 886,000 (returnees) hata hivyo wengi bado wanaishi katika kambi za wakimbizi.
  • Zamfara, 450,000 wamehamishwa na mashambulizi ya bandits, na 638 vijiji vimesakwa, 725 viko chini ya udhibiti wa magenge.
  • Plateau na Katsina, maelfu wamehamishwa mara kadhaa, na wengi wamelazimika kuombaomba ili kuishi. Hali iliyopelekea kukosa uhakika wa kupata chakula na huduma za kiafya, hasa baada ya kufungwa kwa kambi kama Muna IDP camp iliyopo Borno, jambo lililosababisha maelfu waathirike zaidi.
Hali ya maisha ya binadamu katika maeneo haya yamezidi kuwa magumu kutikana uwepo wa majanga ya asili ambapo Mafuriko ya 2025 yameongeza shida zaidi kwa kuua karibu watu 700 na kusababisha zaidi ya watu 896,000 kuhama makazi yao, hasa katika majimbo 18 kama Borno na Yobe.

Mkutano wa rais Tinubu wakuu wa vyombo vya usalama ni wazi ulikuwa umejikita kwenye hali inayozidi kuwa tete nchini humo hususani baada ya matukio ya hivi karibuni likiwemo lile la kushambuliwa kwa masafra wa Brigedi ya Task Force 25.

Katika tamko hilo rais Tinubu aliongezea kuwa ” Kuanzia sasa, yeyote anayehitaji walinzi wenye silaha atawaomba kutoka Civil Defence (NSCDC). Polisi sasa ni wa raia wa kawaida.
Pia ameidhinisha kuajiri polisi wapya 30,000 na kushirikiana na majimbo kuboresha vituo vya mafunzo.
Hii si ahadi tu. Ni hatua inayoanza kutekelezwa mara moja. Polisi wengi tayari wameanza kuondoka kwenye nyumba za VIP na kurejea kwenye kituo vya karibu nawe.”

Suala uwajibikaji ni tatizo kubwa sana nchini Nigeria ambalo linagharimu maisha ya raia wengi wanakumbana kadhia ya matukio ya kiharifu na hata kukatishwa uhai wao, huku watu wanaopaswa kuwalinda wakionekana wanalinda wachache wenye uwezo wa kiuchumu na madaraka linaweza kufanya iwe kwa mara ya kwanza kwa muda mrefu, ambapo mwananchi wa kawaida anaweza kuhisi yupo usalama wake umepewa kipaumbele.
Tusubiri tuone kama mabadiliko haya yatadumu na kuwa muarobaini wa hali ya usalama katika nchi hiyo.

Amnesty International: “Mounting Death Toll and Looming Humanitarian Crisis” (Mei 2025)

Global Centre for the Responsibility to Protect: Nigeria Update (Novemba 2025)

Human Rights Watch: World Report 2025 - Nigeria Chapter (Januari 2025)

UN OCHA: Nigeria 2025 Humanitarian Needs and Response Plan (Januari 2025)

Reuters: “Nigeria Insurgents, Bandits Kill More in First Half of 2025” (Julai 2025)

The New Humanitarian: “Boko Haram is Back” (Novemba 2025)

US Department of State: 2024 Country Reports on Human Rights Practices - Nigeria (Agosti 2025)

Soufan Center: “From Criminality to Insurgency” (Agosti 2025)

Nannew.ng
 
Tuendelee kuwaangalia wenzetu, ila hata hapa tanzania tukiendelea na huu uhuni unafanyika na serikali ya sasa ndio tunapoelekea,
Population itakavozidi kua kubwa ndivyo hatari inazidi na si miaka mingi, less than 30yrs,
Serikali inaona kuteka watu ni kawaida ila ni uasisi wa jamii ya kizazi kijacho, na hatari ikianza itamkuta kila mmoja haitachagua chama, dini wala kabila
 
Juzi Jumapili, Ikulu ya Abuja ilikuwa kimya lakini ndani kulikuwa kwa moto sana. Rais Tinubu alikuwa amewaita wakuu wote wa vyombo usalama: IG Kayode Egbetokun, DG DSS Tosin Ajayi, Chief of Army Staff Lt-Gen Waidi Shaibu, Chief of Air Staff Air Marshal Sunday Kelvin Aneke. Mkutano haukuchukua muda mrefu. Walipotoka, Agizo lilikuwa tayari ni;
Polisi wote waliokuwa wameambatishwa kama walinzi wa binafsi kwa VIP – wanasiasa, wafanyabiashara, magovernor, maseneta na watu mashughuri. Wameondolewa mara moja.
View attachment 3507286

Polisi hao wanaondoka kwenye mageti ya vigogo, kwenye kulinda nyumba za kifahari, wanaondoka na kwenye misafara ya viongozi. Na wmeagizwa wanarudi mitaani, vijijini, barabarani, pale wananchi wa kawaida wanapohitaji ulinzi zaidi.
Tinubu aliweka wazi kuwa
Maafisa wengi wa polisi wamekuwa wakilinda watu wachache wenye madaraka na pesa, wakati maeneo mengi ya nchi hayana hata askari mmoja.

Hali ya kiusalama nchini Nigeria imezidi kuwa si shwari kabisa, Hii ni kutokana kuongezeka kwa matukio ya kuhatarisha usalama wa raia kaskazini-mashariki mwa nchi hiyo maeneo ya Borno, Adamawa na Yobe ambapo makundi ya Boko Haram na ISWAP bado yanaendelea kusumbua. Pia kaskazini-magharibi mwa nchi hiyo maeneo ya Zamfara, Katsina, Kaduna, Sokoto na Niger kuna magenge ya waporaji yanayoendelea kuua na kuteeka nyara watu. Hata Katikati na Kusini mwa nchi hiyo katika maeneo kama Rivers, Delta, Bayelsa, hata Lagos na Ogun, wahalifu wa kutumia silaha wamezidi kuwa na matukio ya mala kwa mala ambayo hugharimu maisha ya raia wengi. Wananchi wengi wanaishi kwa hofu, wakulima hawaendi shambani, watoto wengi hawaendi shuleni. Hali ya usalama nchini Nigeria imesababisha vifo zaidi ya 10,000 tangu Rais Tinubu aingie madarakani Mei 2023, lakini 2025 pekee imekuwa mbaya zaidi.
  • Katika nusu ya kwanza ya 2025 (Januari-Juni), watu 2,266 waliuawa na magenge yenye silaha au insurgents (kama Boko Haram na ISWAP), na hii imevuka idadi ya vifo vya 2024 yote. Hii inajumuisha matukio makubwa ya mashambulio dhidi ya raia lile la Septemba 2025 katika kijiji cha Mafa, Yobe, ambapo 170 waliuawa na ISWAP.
  • Kuanzia Mei 2023 hadi Mei 2025, takliban watu 10,217 waliuawa katika majimbo ya Benue, Edo, Katsina, Kebbi, Plateau, Sokoto, na Zamfara kutokana na mashambulizi ya gunmen na magenge. Katika Zamfara pekee, 1,088 waliuawa katika nusu ya kwanza ya 2025. Katsina, zaidi ya 294 waliuawa na 306 walitekwa nyara (wengi wanawake na wasichana) kutoka Mei 2023 hadi Mei 2025. Hii inajumuisha mashambulizi ya kila siku na magenge ya bandits.
  • Borno na Yobe (kaskazini-mashariki), makundi ya Boko Haram na ISWAP wameua mamia, watu 63 waliouawa Septemba 2025, Darul Jamal, Borno, na 170 waliuawa Yobe. Jumla ya vifo vya Boko Haram tangu 2009 ni zaidi ya 350,000, na 2025 inaendelea kuongeza.
Majimbo mengine: Katika Plateau, zaidi ya 100 waliuawa Aprili 2025 katika mashambulizi mawili makubwa; Kaduna na Benue vifo zaidi ya 200 katika mashambulizi moja la Juni 2025.
Kwa jumla, ripoti za Mei 2025 zinaonyesha takliban vifo 6,800 vinavyohusiana na vurugu katika nusu ya kwanza ya mwaka, na idadi inaongezeka kwa kila mwezi.

Machafuko yanachochewa na itakadi za kidini pamoja na nia za kufanya uharifu yamesababisha mamilioni ya watu kuyahama makazi yao kutokana na vurugu na matishio ya kiusalama.
  • Takriban milioni 3 wamehamishwa na vurugu tangu 2023, wengi katika kaskazini-mashariki na magharibi. Borno pekee ina waliohama milioni 1.7 (IDPs) na waliorudi nyumbani 886,000 (returnees) hata hivyo wengi bado wanaishi katika kambi za wakimbizi.
  • Zamfara, 450,000 wamehamishwa na mashambulizi ya bandits, na 638 vijiji vimesakwa, 725 viko chini ya udhibiti wa magenge.
  • Plateau na Katsina, maelfu wamehamishwa mara kadhaa, na wengi wamelazimika kuombaomba ili kuishi. Hali iliyopelekea kukosa uhakika wa kupata chakula na huduma za kiafya, hasa baada ya kufungwa kwa kambi kama Muna IDP camp iliyopo Borno, jambo lililosababisha maelfu waathirike zaidi.
Hali ya maisha ya binadamu katika maeneo haya yamezidi kuwa magumu kutikana uwepo wa majanga ya asili ambapo Mafuriko ya 2025 yameongeza shida zaidi kwa kuua karibu watu 700 na kusababisha zaidi ya watu 896,000 kuhama makazi yao, hasa katika majimbo 18 kama Borno na Yobe.

Mkutano wa rais Tinubu wakuu wa vyombo vya usalama ni wazi ulikuwa umejikita kwenye hali inayozidi kuwa tete nchini humo hususani baada ya matukio ya hivi karibuni likiwemo lile la kushambuliwa kwa masafra wa Brigedi ya Task Force 25.

Katika tamko hilo rais Tinubu aliongezea kuwa ” Kuanzia sasa, yeyote anayehitaji walinzi wenye silaha atawaomba kutoka Civil Defence (NSCDC). Polisi sasa ni wa raia wa kawaida.
Pia ameidhinisha kuajiri polisi wapya 30,000 na kushirikiana na majimbo kuboresha vituo vya mafunzo.
Hii si ahadi tu. Ni hatua inayoanza kutekelezwa mara moja. Polisi wengi tayari wameanza kuondoka kwenye nyumba za VIP na kurejea kwenye kituo vya karibu nawe.”

Suala uwajibikaji ni tatizo kubwa sana nchini Nigeria ambalo linagharimu maisha ya raia wengi wanakumbana kadhia ya matukio ya kiharifu na hata kukatishwa uhai wao, huku watu wanaopaswa kuwalinda wakionekana wanalinda wachache wenye uwezo wa kiuchumu na madaraka linaweza kufanya iwe kwa mara ya kwanza kwa muda mrefu, ambapo mwananchi wa kawaida anaweza kuhisi yupo usalama wake umepewa kipaumbele.
Tusubiri tuone kama mabadiliko haya yatadumu na kuwa muarobaini wa hali ya usalama katika nchi hiyo.

Amnesty International: “Mounting Death Toll and Looming Humanitarian Crisis” (Mei 2025)

Global Centre for the Responsibility to Protect: Nigeria Update (Novemba 2025)

Human Rights Watch: World Report 2025 - Nigeria Chapter (Januari 2025)

UN OCHA: Nigeria 2025 Humanitarian Needs and Response Plan (Januari 2025)

Reuters: “Nigeria Insurgents, Bandits Kill More in First Half of 2025” (Julai 2025)

The New Humanitarian: “Boko Haram is Back” (Novemba 2025)

US Department of State: 2024 Country Reports on Human Rights Practices - Nigeria (Agosti 2025)

Soufan Center: “From Criminality to Insurgency” (Agosti 2025)

Nannew.ng
Hii nchi inasikitisha na kufurahisha.

Kuna msemo niliwahi kukutana nao unasema 'Nigeria ni nchi ila sio Taifa'..

zitto junior T14 Armata JokaKuu
 
Ni kweli kabisa, aliyesema hivyo hakukosea. Nigeria ina kila viashiria vya kuwa failed state. Takwimu za 2024 za Fragile States Index zinaonyesha Nigeria inashika namba 15 kwa nchi dhaifu na zilizo katika hatari zaidi ya kuanguka kama Taifa. Kwa nafasi kama hiyo ni sawa kabisa na kusema Nigeria ni “Kuti kavu, kuanguka si suala la ajabu”
IMG_2858.jpeg
 
Hii nchi inasikitisha na kufurahisha.

Kuna msemo niliwahi kukutana nao unasema 'Nigeria ni nchi ila sio Taifa'..

zitto junior T14 Armata JokaKuu
Tinubu hayupo serious bado, hivi majuzi kachagua mwalimu wa zamani wa shule ya msingi kuwa Waziri wa Ulinzi kwenye nchi yenye usalama mdogo sana.

Brigadier General aliyeuwawa na magaidi alikuwa anawasiliana na staff kwa WhatsApp na walitumia masaa kadhaa kumtafuta msituni baada ya kutoroka magaidi waliomshambulia. Cha ajabu alipotoa location yake kwenda kwa jeshi, magaidi wakajua yuko wapi na wakamuwahi.

Makosa mengine ni ya Muhammad Buhari huyo ndio alikuwa Rais wa hovyo sana na ajabu katoka jeshini. Yeye alikuwa terrorists anawaita bandits alafu anawaunga jeshini kama njia ya kuwashawishi waachane na uvunjifu wa amani. Matokeo yake ni kama ya DRC ya Laurent Kabila, jeshi lina mamluki.

Nimeona viongozi wa Nigeria wamecha kutumia bulletproof vehicles sasa hivi wanatumia armoured vehicles kabisa. Kama wako frontline.
 
Hatari sana...

Nigeria na utajiri wake wote inaelekea kuwa 'Drc' ya Africa Magharibi.
 
Hii nchi inasikitisha na kufurahisha.

Kuna msemo niliwahi kukutana nao unasema 'Nigeria ni nchi ila sio Taifa'..

zitto junior T14 Armata JokaKuu
Udini na ukabila umeimaliza Nigeria. Ukiwakuta huko diaspora au mitandaoni wanapenda kujiona wao ndio top kwenye kila kitu ila uhalisia nyumbani ni tofauti kabisa. Its a failed state in many ways
 
huyo Tinubu amepigwa mkwara na D.Trump kwamba ana wajibu na jukumu la kulinda Christians wanaouliwa kila siku nigeria na muslims jihadist boko haram ...
 
Back
Top Bottom