Toosweet
JF-Expert Member
- May 27, 2012
- 2,141
- 1,982
Heshima kwenu Wanabodi,
Mpaka sasa ni takriban miezi 19 toka Mh. Rais aanze kusimamisha na kufukuza viongozi waandamizi wa serikali na wanasiasa. Makada wa CCM wamekuwa wakidai kuwa Mh. Rais anasafisha nchi kwa kuwa ni mzalendo.
Hawa ni baadhi ya waliofutwa;
Machi 6,2016 Katibu Mkuu Kiongozi balozi Segue aliyimbuliwa.
Machi 13,2016 aliteuwa wakuu wa mikoa 26 na kutimua 13
Aprili 26,2016 alisimamisha Mkurugenzi Mkuu wa TCRA Dr. Ali Simba kwa kudaiwa kutosimamia vema utekelezaji wa mkataba wa mawasiliano na kusababisha nchi kupoteza Tsh 400 bilioni kwa mwaka.
Aprili 26,2016 Rais alitimua makatibu tawala wa mikoa 10 na kuingiza wapya wawili, kwa jumla aliteua 26.
Julai 7,2016 Rais aliweka pembeni wakurugenzi 120.Aliteua wakurugenzi wa halmashauri za majiji watano(5),manispaa 21,majiji 22,na wilaya 137.
Desemba 30,2016 alitema makatibu wakuu watano na kuingiza wapya.
Wengine waliosombwa na panga la Rais Magufuli ni aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani Charles Kitwanga, Edward Hosea aliyekuwa Mkurugenzi TAKUKURU, Anne Kilango, Mkurugenzi wa TANESCO Felchesmi Mramba. Wengine ni aliyekuwa Mkurugenzi wa NIMRI Dr. Mwele Malecela, aliyekuwa Waziri wa Habari na mbunge wa Mtama Nape Nnauye, Diwani Athumani aliyekuwa Mkurugenzi wa Upelelezi Makosa ya Jinai, aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini Sospeter Muhongo na hivi karibuni aliyekuwa IGP,Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini kamanda Ernest Mangu.
Hawa ni sehemu tu ya waliosimishwa, teuzi zao kubatilishwa au kuambiwa watapangiwa kazi nyingine. Kusimamisha au kubadili viongozi Mara kwa Mara kunaondoa ufanisi. Watendaji huingia hofu ya kuondolewa kwenye nafasi, huchelea kuanzisha mipango au miradi mipya. Kuleta kiongozi mpya kabla ya yule wa awali kuzoea mazingira na kufahamu wafanyakazi watakaomsaidia kazi, hifanya ofisi, taasisi, wizara kushindwa kufikia malengo.
Nawasilisha.