Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 53,337
- 120,836
Wanabodi,
Mimi ni miongoni mwa watu ninaotatizwa sana na ukiukwaji wa haki unaofanyika popote ndani ya JMT na ni miongoni mwa watu wa mwanzo mwanzo kabisa kumuita rais wetu Dr.John Pombe Magufuli kuwa ni dikiteta.Magufuli ni Dikiteta!, Tanzania Ilihitaji Dikiteta, Tumempata!. Atakayeleta Fyoko, Ataisoma Namba!
Udikiteta ni Dhana Tuu or ni Real?. "Lets Call A Spade A Spade!"Dikiteta ni Mtu Mwenye Tabia Hizi!".
Character Assassination ni Modus Oparandi ya Madikiteta Katili Wote Duniani!
Katika tumbua tumbua majipu ya rais Magufuli niliunga mkono dhana nzima ya utumbuaji na dhima ya utumbuaji ila sikuunga mkono utekelezaji wa utumbuaji huo kutokana na baadhi ya utumbuaji kufanywa kidikiteta kwa chuki, papara na double standards za hali ya juu kwa kukiuka sheria, taratibu na kanuni.
Utumbuaji Majipu wa Rais Magufuli: Is It A Right Thing, At The Right Time, And Doing It Right, Or ?!
Je, Kila utumbuaji ni wa haki, au kuna kumkomoa Kikwete?!
Je inawezekana huu ndio mwisho wa utumbuaji wa papara na kukurupuka?! Mkuu kutumbuliwa soon!
Lakini kwa hii timua timua ya kuwatimua vigogo wa CCM, nimefarijika sana kwa sababu kumbe huu utumbuaji wa kidikiteta sio kwa serikali tuu bali hata kwa CCM. Hii ni plus kwa Magufuli kuwa katika tumbua tumbua, anatumbua tuu bila kumuangalia mtu usoni kuwa nani ni nani, kama mtu kama Sofia Simba ameweza kutumbuliwa, then kiukweli Magufuli sio mchezo! .
Rais Magufuli, Waliomchagua Wanajuta!, Wasiomchagua Wanamshangilia!. Akishika Chama, Watakoma
Rais Magufuli: Utumbuaji majipu usitafsiriwe kama ukatili
Hakuna ubishi kuwa CCM ni chama kikongwe kinafanya mambo yake kiutu uzima. Kwenye katiba yake kinazo taratibu za nidhamu zilizofuatwa ndani kwa ndani, kimya kimya hadi kufikia hatua ya mwisho ya watu kupigwa chini ndipo umma unaambiwa na kupigwa na surprise. Huu ni ukomavu na ndiko kufanya maamuzi makubwa kiutu uzima. Pongezi ziende kwa Mwenyekiti Magufuli. Wapinzani mjifunze kutoka CCM.
Ugomvi wa Baba na Mama.
Mara nyingi watoto huwa hawawezi kufahamua kuwa kumbe kuna siku baba na mama huwa wanagombana ugomvi wa kimya kimya chumbani. Mara kwa mara wanawake wakiudhika huwa wanachukia na kuwanyima 'chakula' waume zao, hivyo kuna wanaume kibao hulala njaa na hawasemi. Kuna wanawake kibao hubakwa na waume zao na wengine hupokea hadi vipigo lakini hawasemi. Kuna mara kibao baba na mama wanakuwa wamenuniana ila akija mgeni warajikausha na kuzuga, akiondoka, ugomvi unakuwa umekwisha, hivyo ile mgeni njoo mwenyeji apone sometimes ni kweli.
Ugomvi ukiwa mkubwa hadi mama kufungasha ndipo hakuna namna lazima watoto watajua tena hawatajua sababu ya ugomvi ni nini au nani ni mkosaji na amekosa nini. Hiki ndicho kilichofanyika CCM, watu wametimuliwa bila wanachama kuelezwa wamefanya makosa gani zaidi zaidi ya neno usaliti lakini hakuna taarifa yoyote huku nje nani amefanya nini, hali iliyopelekea watu kuhisi sababu ni huu wimbo wa "Tunaimani na Lowassa...
Ukisikiliza wengi waliimba karibu wote hata hao mnaowaona hata kama hawaimbi kwa sauti, wala kupiga makofi, lakini wanaimba kimoyo moyo!.
Kuhusu Lowassa nilisema hivihttps://www.jamiiforums.com/threads/kuelekea-2015-kama-ccm-itamsimamisha-edward-lowassa.314614/page-26
Licha ya kukubalika, Jina la Lowassa halitafika hata CC!
Kama kweli hili kosa lao ni kumshangilia Lowassa kuonyesha kumsupport Lowassa, then kiukweli kabisa CCM watakuwa ni wamewaonea fulani kwa sababu kwa mujibu wa katiba ya CCM, kumsupport mgombea yoyote wakati wa uchaguzi sio kosa, hivyo hilo sio kosa lao, after all uteuzi ulifanywa kimizengwe. Waliotimuliwa wanamakosa yao ambayo ni mambo yao ya ndani kama ugomvi wa baba na mama chumbani, tumeonyeshwa tuu wakitupiwa virago vyao nje.
Kuhusu mmoja wa watuhumiwa Mama Sofia Simba, mimi niliwahi kumzungumza hapa na kumuita ni ubatili!, Uenyekiti wa UWT: Ni Vita Kati ya Ukweli na Ubatili!
Ni imani yangu kuwa watuhumiwa wote walijadiliwa toka vikao vya chini kimya kimya. Wakapewa barua za mashitaka yao, wakapewa muda wa kujibu tuhuma, wakaitwa kujieleza, wakahojiwa na kupewa muda wa haki ya kusikilizwa na kujitetea, kisha vikao vikafikia maamuzi kimya kimya na hatimaye ndipo vikao vya maamuzi vikatangaza maamuzi yale. Huu ni ukomavu wa hali ya juu na CCM kinastahili pongezi za dhati kwa hili.
Chedema utumieni uzoefu na ukongwe wa CCM katika kufanya maamuzi yake kwa kuzingatia katiba zenu, niliwahi kuwashauri hivi kuhusu udikiteta katika kuendesha mambo yenu ya ndani.Uamuzi wa CHADEMA dhidi ya madiwani: "A Big Mistake!"
Wito: CHADEMA Watendeeni Haki Wanachama Wenu Ili Kuwatendea Haki Watanzania 2015!
Wafuasi wa Zitto na Manazi wa CHADEMA: Tunajenga Nyumba Moja, Tunagombea Fito za Nini?
CHADEMA Ikipewa Nchi, October 2015, Hakuna Hatari Kugeuka Utawala wa Kidikteta? Nauliza Tuu!
Chadema, CUF na NCCR Mageuzi, kukitokea tena utovu wa nidhamu, fanyeni mambo yenu kimya kimya, tumieni kanuni zenu na mamlaka halali za nidhamu, mfano Zitto alipotimuliwa, kikao kilichomtimua ni Kamati Kuu wakati mamlaka yake ya nidhamu ni Baraza Kuu. Msione ugumu kujifunzeni kwa wakongwe kama CCM ili angalau 2020 Watanzania tuweze kuwafikiria tuwajaribishe vinginevyo tutaendelea kiongozwa na chama kikongwe kilichozeeka mpaka basi lakini kila kinapofanya face lift kama hii, kinarudia ujana hivyo hata hapo mlipo kama mnajidhania mmesimama, angalieni 2020 msianguke jumla kwa sababu by that time CCM itakuwa kama kigoli mweupe kwenye Chagulaga, ikimeremeta, kufuatia kazi nzuri ya Magufuli ndio maana tumeshauri Kwa Kasi hii ya Magufuli, kuna haja Kufanya Uchaguzi wa Rais 2020?
Mabadiliko yoyote yanayoanzia juu kwenda chini bila kujadiliwa na watu wa chini katika ushirikishaji, no matter ni mazuri kiasi gani, pia ni udikiteta, ila kitendo cha CCM kuitisha Mkutano Mkuu kuya ruber stamp ni kufuata katiba yake, hivyo hongera sana CCM kwa mabadiliko, na Hongera kwa ukomavu, vyama vingine igeni mfano.
Jumatatu njema
Paskali.