Timu yangu imeniangusha!

Mphamvu

JF-Expert Member
Jan 28, 2011
10,702
3,288
Hii ni timu ambayo nimekuwa nikiipenda tangu udogo, bila kushurutishwa na yeyote na bila shinikizo lolote. Inaitwa Texas Dume, inapatika Mikocheni 'A' kuanzia mtaa wa Masjid Nawal mpaka Kidosho. Tangu zamani, vurugu zimekuwa ni utamaduni wa timu yangu hii, hasa pale inapofungwa kwenye uwanja wake wa nyumbani pale Shule ya Msingi Mikocheni, zamani timu yangu ilikuwa ikicheza mechi zake kwenye Viwanja vya kulimia chumvi, au Chumvini, pale Old Bagamoyo Road kutazamana na kota za maafisa wa polisi za Mikocheni. Juzi, Jumapili, timu yangu hii ilikuwa na mechi na Nondo F.C. ya Mwenge pale Mikocheni S.M. Asubuhi na mchana wote, kundi la ushangiliaji na harambee la timu maarufu kama Kigoma Nyoko (wao hutembea na ngoma ndogo hivi) walipita kuchangisha fedha na kuhamasisha watu kuja kwa wingi kuishangilia timu yao. Mimi kwa moyo wa dhati kabisa, nikajitolea mchango wangu wa fedha ili kuisaidia timu yangu kipenzi iweze kushinda mechi hiyo ya kombe la jezi.
Kilichotokea uwanjani jioni ile ni vurugu kubwa zilizozuka baada ya Texas Dume kufungwa goli la dakika za mwisho. Vurugu hizo zilipelekea mechi kuvunjika, watu kuumia hovyo na zaidi mtoto mmoja kupigwa na chupa ya kichwa iliyomfanya azirai na kukimbizwa hospitali ya Mwananyamala, kwa bahati mbaya mtoto yule alikuwa mkazi wa Msasani Kisiwani, hakuwa shabiki wa Texas wala Nondo F.C. Madhara ya kuumizwa kwa mtoto yule yamefika pahala, sisi wakazi wa Mikocheni tumekuwa 'wanted' kule Kisiwani, yaani ukionekana tu, ama zako ama zao!
Sasa jamani timu yangu kipenzi, vurugu hizi mpaka lini? Naomba wanaJF mlio wakazi wa eneo tajwa na washabiki wa Texas DUME, mumwambie Kimwanya, kiongozi wa Kigoma Nyoko, atumie ushawishi alio nao kujaribu kuwatuliza wanaTexas pale ambako kunakuwa na mwelekeo wa vurugu kwenye mechi zetu za nyumbani.
Naomba kuwasilisha...
 
Ina maana hakuna wadau wa soka la mchangani?
Hata huku pia kuna mpira jamani...
 
Ina maana hakuna wadau wa soka la mchangani?
Hata huku pia kuna mpira jamani...

Tehtehteh Hii Ndio kwanza nimeiona Mkuu kwahiyo Vijana wa Maandazi Road kule Magunia Msasani wanakupiga biti sio? huwa wanakutowa mbio na mawe au Upupu? Pale kwenye chumvi serikali wamepaharibu Kujengwa nyumba bila kufikiria sasa mazara yake Maji ikinyesha mvua hayajui wapi yaende. Kuongeza Marazi tu.
 
Tehtehteh Hii Ndio kwanza nimeiona Mkuu kwahiyo Vijana wa Maandazi Road kule Magunia Msasani wanakupiga biti sio? huwa wanakutowa mbio na mawe au Upupu? Pale kwenye chumvi serikali wamepaharibu Kujengwa nyumba bila kufikiria sasa mazara yake Maji ikinyesha mvua hayajui wapi yaende. Kuongeza Marazi tu.

mkuu kule ni noma.
Vijana wa kule wamepinda zaidi ya dawa ya mbu, kama ulishawahi kuwasikia Mbwa Mwitu, wakija maungoni lazma wakulaze hoi siku kadhaa.
Chumvini was awesome those days, game ilikuwa hainipiti pale. Serikali famba, ilitaifisha yale mabwawa, halafu ikayakalia kitambo bila matumizi. Sasa hivi washajichukulia wajanja.
Aaagh!
 
Back
Top Bottom