kbm
JF-Expert Member
- Oct 5, 2012
- 5,224
- 1,676
KAMPUNI ya simu za mkononi Tigo, imeboresha ofa yake ya WhatsApp ya bure kwa kutangaza kuwanufaisha zaidi wateja wake pindi wanaponunua kifurushi cha kila siku cha Extreme kwa Sh. 1,000.
Faida ya nyongeza inajumuisha muda wa maongezi wa dakika 50, sms bila kikomo, MB 8 zitakazotumika ndani ya saa 24 pamoja na kutumia WhatsApp bure.
Tigo ilianza kuwapa wateja huduma ya WhatsApp bila malipo kuanzia mwanzoni mwa mwaka huu kila wanaponunua vifurushi vya wiki au mwezi.
Mkuu wa Kitengo cha Vifaa vya Intaneti wa Tigo, David Zacharia, katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, alieleza kuwa Tigo itaanza kutoa faida za ziada pamoja na WhatsApp kwa wateja wote pindi wanaponunua kifurushi cha extreme cha Sh. 1,000.
“Ofa hii mpya ni kwa wateja walio na simu zenye uwezo wa kutumia huduma ya Intaneti. Hili linaonesha ni jinsi gani tulivyodhamiria kuleta mabadiliko ya kidijitali katika masisha ya wateja wetu na pia tunavyoongoza kwa ubunifu,” alisema Zacharia.
Kwa mujibu wa Zacharia, Tigo ina wateja zaidi ya milioni 10 na Januari, mwaka huu ilikuwa ni kampuni ya kwanza nchini kutangaza upatikanaji wa huduma ya WhatsApp bure kwa wateja wake pindi wanaponunua vifurushi vya wiki au mwezi au kwa kununua kadi mpya ya simu.
Mtandao huo wa kijamii unaopatikana kwa watumiaji wa simu za kisasa za smartphone.
WhatsApp ni mtandao dada wa kijamii kwa Facebook ambao Tigo ilianza kushirikiana nao tangu mwaka 2014 na mwaka 2015 ilizindua Facebook ya kwanza ya kisasa ikiwa na menyu ya Kiswahili.
WhatsApp ni huduma maarufu ya simu ya kutuma ujumbe ambayo ina watumiaji zaidi ya milioni nane nchini Tanzania na watumiaji zaidi ya bilioni moja duniani.
Chanzo: NIPASHE