Tigo washitakiwe kwa false advertisement

Lycaon pictus

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2021
Posts
10,904
Reaction score
18,866
Tigo wanatangazo jipya, 'Mzigo umeongezwa' wanasema wameongeza vifurushi. Kwa bei zao hizi mpya. 500 inanunua MB 150. Tsh 3000 inanunua mb 1500. Mimi sioni kilichoongezeka zaidi ya kupotosha watu. Juzi tu nilikuwa nanunua mb 1000 kwa Tsh 1000. Haijalishi wanaviita vipi vifurushi vyao.

Ukitangaza sana unaweza kupotosha watu kuwa vifurushi vimeongezeka kumbe vimepungua.

Washitakiwe kwa false advertisement.
 
Hakuna kilichopotoshwa, hawajasema wamepunguza bei wamesema "mzigo umeongozwa" wakimaanisha gharama ya kununua vifurushi ndio iliyoongezwa

Mzigo = pesa
 
Mitandao ipo kibao jidai tigo ndio kabila lako huwezi badili ufe nao
 
Nakuunga mkono. Kwa ujinga wao huo nimeamua kuwahama mazima. Line yao napokelea simu tu. Siweki vocha tena. Pumbaff zao.......
 
Unaishitaki serikali
 
Hivi yule wakili msomi aliyeshtaki kampuni moja ya sim yupo wapi 😂😂

Ova
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…