Tigo: Kwa wizi huu mmezidi, acheni ujanja ujanja

Jurrasic Park

JF-Expert Member
Sep 13, 2013
3,797
6,795
Habari

Mimi ni muumini wa mtandao wa Tigo tangu kipindi kile cha xtreme kama mwaka 2011. Tigo naipenda kwa sababu ya internet yake ya 4G ina nguvu kuliko mitandao mingine na hivi karibuni nilipokea 2000 ya Tigo faida. naipenda sana TIGO.

Sasa kuna mtindo wa kupigiwa namba hii 0901 65 65 64 kisha wanaanza na Tigo hadithi. Ukiwasikiliza wanadai ujiunge. Sasa usipojiunga huwa wanapiga tena na tena. Baadaye unaanza kuona 150 zinapungua kila siku na ukipiga 100 wanakuambia umejiunga Tigo hadithi.

Ukitaka kujitoa unaandika ONDOA kisha unatuma 15668. Ukijitoa wanabadilisha namba. Wanakupigia tena kwa 0713 800 800 mambo ni yale yale.

Ndugu zetu wa TIGO tunaombeni mtuonee huruma maana haiwezekani nijiunge kwenye hadithi za 'kishenzi' maana siyo mtoto nisikilize hadithi za Abunuasi sihitaji.

Asante
 
Kweli ni wezi, kuna utaratibu wa kukopesha sh 900 hata bila kuomba, imenitokea mara mbili napokea msg kwamba "umepokea mkopo wa sh 900 na utarejesha sh 990", wakati huo nakuwa na bando la wiki tayari, ikijitokeza tena ntavunja hiyo laini, ukizingatia uwa siitumii kwa internet
 
Back
Top Bottom