Tigo kuweni makini na Tigopesa yenu

Tigo kuweni makini na Tigopesa yenu

MNAFU

Member
Joined
Jan 16, 2014
Posts
99
Reaction score
24
Ninaandika kwa masikitiko kwani naona kama Kampuni hii ya Tigo haitajirekebisha katika kutatua Matatizo ya kimitandao yanapojitokeza basi Sisi wateja tunaweza kuiogopa Kampuni hii kutumia Huduma zake.

Tarehe 09/06/2015 majira ya saa 4 asubuhi nilihamisha kiasi cha shs. 2,500,000/= toka akaunti yangu ya Tigopesa kwenda benki ya NMB. Fedha ilitoka katika akaunti yangu ya tigopesa na nikapata message. Kwa Bahati mbaya haikwenda ktk akaunti ya NMB na haijaingia hadi Leo, siku ya 3.

Lengo ilikuwa kuweka fedha hiyo benki kuniwezesha kufanya biashara fulani muhimu. Niliisubiria hiyo fedha siku hiyo lakini wapi hadi biashara niliyotaka kufanya ikafa. Kiukweli Tigo wamenipa hasara kubwa!

Hiyo ni tisa, kumi umekuwa ni fedha hiyo kurudishwa Kwenye akaunti yangu ya tigopesa au basi iwekwe Kwenye akaunti! Pesa imepotea! Na haijulikani imepotea wapi??? AIBU SANA.

Siku Ile ya tukio niliwapigia customer care Mara kadhaa ambapo kwanza walisema ni kweli wameona tatizo na litafanyiwa kazi ndani ya saa 24. Nikasubiri muda huo ukaisha, Jana nikapiga Simu tena nikapewa Ahadi nyingi, siku ukaisha. Leo tena Nimepiga Simu nikapewa stori hiyo hiyo. Leo ni siku ya 3.



Najua Watu wa tigo mpo humu. Na kwa nini Hata hamna special thread humu? Wenzenu Vodacom wanayo. Na Pia wana special group email ambayo ukiandika wanafanyia kazi. Mbona nyinyi hamna?

Wakuu naomba ushauri Wenu nifanyeje kuipata Pesa yangu?

Wapi napoweza peleka lalamiko langu likashughulikiwa haraka?
 
Mkuu pole sana. 2.5mil nyingi Hizo. Ikibidi nenda TCRA! Angalia hiyo 24hrs yaweza kwenda Hata mwezi!
 
Matatizo haya hutokea mitandao yote ila hujabainisha aina ya tatizo, pili inapotokea matatizo haya ni lazima ujue tatizo liko wapi zaidi kwani kuna washirika watatu wanaohusika na kufanyika muamala. Ukijua tatizo liko wapi ndio njia ya kutatua tatizo kwa haraka,kuna mtu alipata tatizo kama hilo ila si kwa kampuni ya tigo akapata usumbufu ila baada ya kujua kiini cha tatizo pesa yake alirudishiwa ndani ya muda mfupi. Nenda ofisi ya tigo wakuhakikishie kama muamala umetoka kwao, kama umetoka wakupe vielelezo (printout) inayothibitisha muamala huo ndipo uende bank. Na hakika hii ndio njia stahili, hata ukienda tcra wataomba muhtasari ya ufuatiliaji. Kama hujafuata utaratibu unaotakiwa watakuelewesha utaratibu unaotakiwa kufuatwa.
 
Matatizo haya hutokea mitandao yote ila hujabainisha aina ya tatizo, pili inapotokea matatizo haya ni lazima ujue tatizo liko wapi zaidi kwani kuna washirika watatu wanaohusika na kufanyika muamala. Ukijua tatizo liko wapi ndio njia ya kutatua tatizo kwa haraka,kuna mtu alipata tatizo kama hilo ila si kwa kampuni ya tigo akapata usumbufu ila baada ya kujua kiini cha tatizo pesa yake alirudishiwa ndani ya muda mfupi. Nenda ofisi ya tigo wakuhakikishie kama muamala umetoka kwao, kama umetoka wakupe vielelezo (printout) inayothibitisha muamala huo ndipo uende bank. Na hakika hii ndio njia stahili, hata ukienda tcra wataomba muhtasari ya ufuatiliaji. Kama hujafuata utaratibu unaotakiwa watakuelewesha utaratibu unaotakiwa kufuatwa.

Ahsante Tindi.

Ukweli ni kuwa tigo tatizo wanalijua vizuri. Nimekwishaongea na customer care zaidi ya Mara 6 (na kupewa tracking Id) ambapo wakicheki wanasema ni kweli nilituma Ila haikwenda na wamepeleka kitengo kinachoshughulikia Mambo ya benki. Tatizo hapa ni how long?

Binafsi Nina ufahamu wa kutosha kuhusu Haya Mambo ya mitandao, na Najua itarudishwa kwangu au itawekwa ktk Ile account ya benki. Tatizo ni lini itafanyika!!!

Lakini Pia mtandao tunatumia nchi nzima na Wakati mwingine tuko ndani hasa ya Tanganyika, kilomita nyingi toka ofisi ya mtandao husika (wilayani au mkoani) na Hata benki Pia. Tunafanyaje hapo? Kama ni mtandao tunatakiwa kuwa na utaratibu rafiki wa kutatua Matatizo. Sio Kila Kwenye tatizo mteja afike ofisini, n.k.

Kwani kwa mfano Mimi Nikifika ofisi ya tigo Nakwenda kufanya nini hasa? Wanione wathibitishe ni Mimi au nini hasa? Fedha inatakiwa iingie ktk account au irudishwe ilikotoka, full stop.

Otherwise nakushukuru.
 
Last edited by a moderator:
Ahsanteni wakuu naona wamerudisha Kwenye akaunti yangu ya tigopesa.

Lakini ni usumbufu usio na lazima. Fedha imetumwa Source A kwenda Destination B. Kama Kwenye A imetoka na Kwenye B haikufika basi kuna sehemu imekwenda. Yaani kuna akaunti imekwenda (call it anything account). Kinachotakiwa ni kufanya verification if it was a regitimate transanction. Baada ya hapo unaamua kuitoa huko na kuirudisha Kwenye Source A au Kwenye destination B. Tatizo hapo ni uzembe wa Kitanzania. Inachukua masaa mangapi? 3 days?

Watanzania tubadilike. Transaction hiyo walinikata 7,000. LAKINI WAMERUDISHA 2,500,000 TU.

Je hiyo 7,000 si wameniibia?
 
tigo huwa hawako makini kwenye ela bora ukatumia m pesa
 
duuuuh nami kuna mtandao fulani nilinunua umeme tangu mwanzoni mwa mwezi wa tano mpaka leo kimyaaa hakuna cha umeme wala nin. kila nikipiga custumer care naambiwa nisubiri saa 24 lkn hakuna utatuzi. watakuwa wamenidhulumu
 
Tigo ni hovyo kabisa, mimi muamala wangu umekwama kwao tangu tar 2/06/2015 mpaka leo.

Pole sana ndugu yangu. Yaani tatizo kubwa la tigo ni kuwa kila ukipiga customer care anayepokea anakupa 24hrs kusubiria tatizo lako kutatuliwa na unatumiwa id. Kwa hiyo unakuta 24hrs haiishi! Ukipiga tena unapewa 24hrs na kutumiwa tracking Id nyingine. Mimi nilipiga Mara 6 hivyo nilikuwa na tracking Ids 6 tofauti!

Mshindani Wao Vodacom katoa email address (group address) ambayo ukiandika inawafikia wengi na hivyo kushughulikiwa haraka. Tigo naona hawana hiyo kitu kwa hiyo unajikuta lazima uongee na customer care Yao na unapata majibu Yale Yale!!!

Angalia hawana hata special thread humu jf Wakati wenzao wanayo! Wenzao wanaitumia hiyo angalau kupata mawazo au malalamiko ya wateja! So lazima wakopi lakini what is the alternative?

Kwa kweli wanahitaji kubadilika na kuboresha Huduma zao?

By the way nilisikia Kampuni ya tigo ilikuwa Kwenye mchakato wa kuuzwa na Sijui kama ilishauzwa au vipi?
 

  • naomba kujuzwa ni kias gani maximum amount naweza kuwa nayo kwenye tgo pesa​



 
aisee, nami yamenikuta leo. nimetuma hela 1M kwenda CRDB tangu tarehe 8-Dec-2015 mpaka leo chalii.
nimeongea na huduma kwa wateja naambiwa hela imekwama haikwenda. sasa imekwama wapi nami haijarudi katika salio langu?? imeambiwa nisubiri masaa 24, lkn hayo masaa 24 nadhani itakuwa siku 3 au 4 zaidi.

nina urgent payment ya kufanya, now am stack. so disappointed!!
 
Tigo bado ni tatzo kwenye sim banking...! Pamoja na makato makubwa lakini huduma bado za kiwango cha chini..
 
Tahadhari, usije ukatuma hela kutokea tigopesa kwenda benki, UTAJUTAAA! USIJARIBU KAMWEEEEEEEE!!!!!!
 
kwa expirience customer care wa kwenye simu wa tigo waharudishi hela utapigwa kalenda ya masaa 24 had unyooke

nenda kwa branch na hela itarudishwa instantly yaliwah nikuta kma yako

nilikosea namba ya wakala
 
Hawa tigo nawadai laki moja ya tigo pesa, na elfu ishirini ya overscratched vocher tangu tarehe 7/9/2015 nawalia timing tuu yule muhuni pale atanitambua(office makumbusho), offer yangu ya 30GB 4G every month for 3months baada ya kununua modem ya 4G, (mlimani city) watumishi wao si waaminifu kama siyo hao wazungu na wahindi wao wanataka kutuibia
 
Onyo: Usijaribu kutuma fedha kwenda benki (akaunti) kwa kutumia tigopesa! Utajutaa!!!!
 
Tigo ni wezi....... Mi nilituma laki 7 kutoka Tigo kwenda airtel....... Nilipambana mwezi na nusu ndo ikarudi...... Sitaki hata kuwasikia
 
Yaani tigo wana wafanya kazi wezi hatari mimi wameha nitpeli mtu katoa pesa kwenye namba yangu ya biashara kwamba kuna mtu alita ela akiwa mbali lakini mimi sms sikuina na maesabu yangu hayakuongezeka siku ya tatu ndio wananitumia sms
 
Back
Top Bottom