Tigo imetengeneza fursa kwa Makampuni mengine ya simu

Tigo imetengeneza fursa kwa Makampuni mengine ya simu

SUTAGI-

JF-Expert Member
Joined
Nov 9, 2018
Posts
278
Reaction score
517
Airtel, Vodacom, Halotel, Zantel na TTCL hamjaona fursa ya kunadi biashara zenu ktk msimu huo ambao Tigo wameutangazia umma wa Watanzania kuwa kwao usiri wa taarifa za wateja wao siyo kipaumbele?

Muda huu mnatakiwa kuanzisha bundle zenye majina kama.

Siri bundle (Dakika 10 mitandao yote + Ujumbe mfupi 100 + Data 100MB) kwa shilingi 500 tu.

Freeman bundle (Dakika 100 mitandao yote + MB 50) kwa shilingi 1000

Kwa kipindi hiki mkiweka vifurushi vyenye majina kama hayo mkayatangaza nina uhakika kabisa mtapata wateja wengi ambao watahama kutoka upande wa pili.

Ninamshukuru Mungu tangu nianze matumizi ya simu sijawahi kumiliki line ya Tigo.
 
Wasiojali wateja tuwatie kapuni, Hadi pale watakapo wathamini wateja/waajiri wao🗑️.
 
Tigo majinga kweli, ndiyo maana wana vifurushi vyenye majina ya kihuni. Mfano: Cha asuhuhi!
 
Hayo majina ya vifurushi mleta uzi ni Freeman brain
 
Shida sio tigo wala mtandao mwingine bali ni sheria ya mawasiliano ndizo zinzwabana wamiliki wote mitandao, hata voda wakitakiwa kutoa taarifa kwa mamlaka wanapaswa kufanya hivyo. sheria iko wazi inalazimisha wamiliki kutoa taarifa kwa serikali ili kufanikisha uchunguzi.

Hakuna taasisi inayomlinda mteja wake dhidi ya serikali..... serikali inayo msamlaka ya kuomba taarifa yeyote ya mteja kutoka kwa mtoa huduma yeyote yule, hakuna cha voda, halotel, airtel n.k

Serikali ikihitaji taarifa inapewa
 
Back
Top Bottom