TIC yaagiza uhakiki maeneo ya uwekezaji

diana chumbikino

JF-Expert Member
May 29, 2018
428
368
1552197313336.png

MKURUGENZI wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Geofrey Mwambe, ameagiza serikali za Wilaya za Siha, Hai na Moshi kuhakiki upya maeneo yote yaliyotengwa kwa ajili ya uwekezaji na kupeleka taarifa zake katika kituo hicho ili kuepusha migogoro

Mwambe alitoa agizo hilo jana alipotembelea maeneo ya uwekezaji katika wilaya hizo, kuangalia changamoto na hatua ambazo zinaweza kuchukuliwa kuweka mazingira rafiki zaidi ya uwekezaji. Alisema kituo hicho kipo tayari kuwasaidia wawekezaji wa aina zote pamoja na kuweka miundombinu rafiki, lakini ikisisitiza wawekezaji waliokuja nchini kuzingatia sheria na taratibu za nchi.

Alisema serikali imejipanga kuhakikisha wawekezaji wote wanapewa stahiki zao na kuandaliwa mazingira rafiki ya uwekezaji kimkataba, miundombinu na kupata ushauri kulingana na mpango kazi wao.

“Kwa maeneo mliyoyatenga ya kwa ajili ya uwekezaji, yahakikini katika wilaya zetu, leteni taarifa kituo cha uwekezaji kwa idadi, ukubwa na fursa zilizopo ili tuweze kutafuta wawekezaji.

mtusaisidie kuwa mabalozi wazuri kwa yeyote anayetaka kuja kuwekeza hapa nchini." Akiwa katika Wilaya ya Siha, Mkurugenzi huyo wa TIC alitembelea mashamba ya uzalishaji wa kuku ya Kampuni Irvines Tanzania Ltd na uwekezaji wa Pararachichi katika Kampuni Africado inayouza bidhaa zao nje ya nchi.

Mkuu wa Wilaya ya Siha, Onesmo Buswelu, alisema wao kama serikali watahakikisha kuna patikana umeme wa kutosha na kuwapa ushirikiano wa hali na mali ili waweze kuwekeza bila usumbufu wa aina yoyote. “Tupo tayari kutoa ushirikiano kwa wawekezaji wageni na waliopo ikiwa watafika na kuzingatia sheria na taratibu za uwekezaji hapa nchini.

”alisema Awali, Mkurugenzi wa Shamba la Kuku la Irvines Tanzania Ltd, Dk. Pietro Stella alimuomba Mkurugenzi huyo wa TIC kuangalia changamoto mbali mbali zinazowakabili baadhi ya wawekezaji kama vile changamoto ya miundombinu.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom