Tibaijuka Katolewa Kafara Kwa Sababu ya Uzembe Wake Mwenyewe

Captain-Chui

Member
Dec 11, 2014
80
49
Tanzania ni nchi ya kula. Ukipewa nafasi unakula. Watazania wengi ni mafisadi kila mmoja kwa nafasi yake. Cha msingi wewe hakikisha tu kwamba hukamatwi. Ukikamatwa utaathibiwa, sio kwa sababu umeiba bali ni kwa sababu umefanya uzembe ukakamatwa. Professor Tibaijuka amefanya uzembe akakamatika. Kwa hiyo inabidi aadhibiwe atolewe kafara kuwafumba macho wananchi. Wenzake wajanja wlichukua pesa cash kwenye mifuko ya rambo na magunia na kufuta ushahidi. Yeye Prof Tibaijuka anajianika anafungua account kuweka ushahidi wazi. Inaonekana huyu prof ana akili tu za darasani, lakini akili za kifisadi ni sifuri.
 
Kweli hata mi nimefikiri hivyo hivyo Kuwa kwake na domo wazi ndiko kuliko mkost maana kakiri kabisa kuwa kweli kapewa hela. Je Presee angeweza kuendelea kumlinda haikuwa raisi ilibidi tu atolewe kafara ya Krismas pole kwake na familia nzima huo ni msiba.
 
ni bora hata yeye kasema ukweli na kaonyesha pesa zilipokwenda.
 
Watu huwa hawajifunzi jinsi ya kufuya nyayo zao pale wapitapo. Wengine huwa waonesha kama wanaenda kumbe wanarudi
 
Mdomo ulimponza kwa mara ya kwanza alipokiri kupewa mgao(wake?) Na ukamponza tena kwa kuropoka mbele ya waandishi wa habari kuwa han'goki!! Huku akijua wazi kuwa kuna mwenye mamlaka juu yake,hivyo kitendo cha kutomwajibisha kingechukuliwa kama ni rais kuburuzwa na watumishi walio chini yake,angejinyamazia haya huu upepo ungepita tu.
 
Ulimi uliponza kichwa
Hakuna sababu nyengine yeyote ya kutolewa kafara zaidi ya kuonekana soft target na ilikuwa lazima ionekane hatua imechukuliwa na Raisi, kama ni kupokea pesa hana tofauti na wengine waliotajwa kupokea pesa na kama ni ulimi kuna wengi waliosema zaidi ya alivyosema yeye. Anajua Mama alichukua lakini hakuwa kwenye mtandao ambao unafahamu mchezo mzima wa escrow ulivochezwa.Huyu mjinga alikubali kupewa pesa ili alipe kwa kutoa upendeleo akiwa Waziri wa Ardhi kama wanavyotoa viongozi wengi wa serikali pale wafanyabiashara wanapowapa zawadi au pesa ili wawaweke kama kinga pale wanapokuwa na shida.
 
Kikwete jana alisema AG amejiuzuru na kusema kuwa kama kuwapotosha wengine ni yeye kwa hiyo akaamua kustaafu! Lakini pia amesema pesa sio ya umma!! sasa kama pesa siyo ya umma huyu mama anakosa gani kupokea pesa ambayo ni ya rafiki yake? kama yeye alipopewa suti ya nguo??
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom