Tiba ya tumbo kuuma--weak enzymes

HAZOLE

JF-Expert Member
Feb 25, 2011
1,551
708
Hi jf members,
naombeni msaada wa dawa itakayonisaidia kutibu tumbo linalouma. Nimeenda kupima kwa daktari nikaambiwa enzymes zangu ni weak/dhaifu kwahiyo tumbo linakuwa na wakati mgumu sana kusaga chakula.
Pia daktari akashauri nisiwe nakula vyakula kama mayai na samaki na soda zenye gesi nyingi kama pepsi na kokakola.
Najua wataalamu mpo hapa jf, naombeni mnisaidie ktk hili na kwa wale wote waliokutana na hii case, i would appreciate their
moral and professional advise.
Nawatakieni j2 njema.
 
tumia sana juice ya parachichi iliyochanganywa na maziwa na asali.
 
Mfumo wa usagaji chakula (digestive system)

Wakati tunapomeza chakula husukumwa hadi tumboni kupitia kwenye koo (gullet). Tumbo ni kama mfuko wa misuli na hukaa na chakula kabla ya kukisukuma kupitia kwenye deodeni (duodenum) ambao ndio mwanzo wa utumbo. Chakula kinapowasili kunyazi cha tumbo huanza kuzalisha asidi ili kuvunja vunja chakula na kukifanya kiwe rahisi kusagika. Asidi ina nguvu sana na kama ingekuwa peke yake bila kuwepo tabaka la mnyunyizo uliogandana unaoitwa utelezi (mucus) ambao huzifunika kunyazi ili kuilinda, asidi basi ingeweza kulimong'onyoa tumbo lote.

Hakika shukurani zote anastahili Allah S.W kwa mpango wa uumbaji wake wenye hikma kubwa mno.
" YEYE (MWENYEZI MUNGU) NDIE ANAEWATENGENEZENI SURA MATUMBONI JINSI APENDAVYO HAKUNA WA KUABUDIWA ILA YEYE, MWENYE NGUVU MWENYE HIKIMA" (3:6)


Uislam umekataza kula kwa kupindukia kiasi. Madhara yake ni mengi mno, lakini mojawapo katika hayo ni kuharibu ustawi wa afya. Mwenyezi Mungu ametuonya juu ya jambo hili kwa kusema:
" ....... NA KULENI (VIZURI) NA KUNYWENI (VIZURI), LAKINI MSIPITIE KIASI TU. HAKIKA YEYE (MWENYEZI MUNGU) HAWAPENDI WAPITAO KIASI." (7:31)


Sababu hasa ya kutosagika chakula tumboni ni kula sana au kunywa kupita kiasi au kula mlo usio sawa pombe vyakula vya mafuta mengi kama chipsi vyakula vyenye asidi nyingi kama vile machungwa lakini kwa bahati mbaya au nzuri hakuna seti moja ya kanuni juu ya ule nini au usile nini. Watu hutofautiana katika kudhurika na vyakula, hivyo ni suala tu la kuainisha mwenyewe ni chakula gani ambacho kinakudhuru na halafu akakiacha.

Baadhi ya watu, hukutana na matatizo ya kutosagika chakula chochote kile watakachokila. Hawa wanaweza kuwa wanasumbuliwa na mojawapo ya matatizo kadhaa kwa mfumo wa usagaji chakula.

UVIMBE (GASTRITIS)
Kama kuna asidi nyingi sana na utetelezi (mucus) unaofanya kazi ya kuizua asidi ni ndogo tumboni, hapo asidi huanza kudhuru kunyazi za tumbo (stomach lining). Kwa hali hiyo utakabiliwa na tatizo la kutosagika chakula kwahio huo unakuwa ni uvimbe-tumbo (uvimbe mwasho wa kunyanzi za tumbo)

Namna mbalimbali za vyakula vinaweza kuuvuruga ulingano wa asidi na utetlezi. Vile vile uvutaji sigara madawa (kama vile aspirini) au matatizo ya mhemko (emetional problems) huwa ndio sababu kuu, na mara nyengine hakuna sababu ya wazi zaidi. Mara kwa mara tatizo la aina hii la kutosagika chakula hujimaliza wenyewe hatimaye. Utakapoacha kutumiwa dawa au kubadilisha dawa na kutumia aina nyengine za dawa za matatizo ya mihemeko yataondoka kunyanzi za tumbo nazo zitajikarabati wenyewe na tatizo la kutosagika chakula litakwisha Inshallah.

Mara nyingi zaidi unaweza kujitibu mwenyewe matatizo ya kutosagika chakula lakini kama utakumbana na mojawapo wa dalili hizi zinazofuatia utatakiwa umuone doktari.:

1. Maumivu makali ambayo huzui shughuli zako kila siku.
2. Maumivu ya kila siku zaidi ya siku 3
3. Maumivu ya mara kwa mara ambayo huendelea kurudi kwa baada ya wiki 2
4. Maumivu ya mgongo baada ya kula.
5. Kupoteza uzito bila sababu.
6. Kupoteza hamu ya kula.
7 Maumivu nyuma ya mfupa wa kidari wakati wa mazoezi au baada ya mazoezi


KUJITIBU MWENYEWE
I.Kula kwa makini
Epuka vyakula na vinywaji vinavyokudhuru.
Usile mara kwa mara
Usile muda mfupi tu kabla ya kulala
Epuka vinywaji vyenye asili ya maziwa.


Kwa kufanya hivo utazuia tumbo lako kuzalisha asidi nyingi.

II.Acha kuvuta sigara
Uvutaji sigara unaweza kusababisha chakula kisisagike.
Wavutaji hupata vidonda vya tumbo kwa urahisi.


III.Badilisha mtindo wa maisha yako
Kutosagika chakula kunaweza kusababishwa na mfadhaiko unaotokana na shida za kimaisha, tabu dhiki, matatizo na mambo kama hayo.​
 
Mfumo wa usagaji chakula (digestive system)

Sala ambayo husaliwa mara tano kwa kila siku ni ibada yenye kuleta utulivu mkubwa wa kiroho. Sala humuondolea mja khofu, huzuni, wasiwasi kwa jambo ambalo linamtatiza au liko nje ya uwezo wake. Mtu baada ya kufanya juhudi zake zote za kimaisha, baadae humelekea Allah S.W na kumuomba uongozi na msaada. Kwahio ibada ya salaa inatosha kuwa kinga ya maradhi pamoja na balaa ya kila aina.

Dhibiti uzito wako.
Watu wenye uzuto mkubwa sana wanafursa zaidi ya kukubwa na tatizo la kutosagika kwa chakula, punguza uzito. Uislam umezungumzia juu ya habari hii ya kudhibiti uzito kwa ajili ya afya yako. Mtume S.A.W anasema: "Yatosha kwa mtu kuondosha njaa kwa matonge machache ili kuimarisha uti wake wa mgongo''. Kama unataka kula hadi kushiba, basi uache theluthi moja ya chakula theluji moja ya maji na theluthi moja ya hewa" (Tirmidh)

Jaribu dawa.
Kama kutosagika kwako chakula hakujakuletea tatizo kubwa sana, basi jaribu dawa za kuzima asidi (anti-acid) ambazo hufanya kazi ya kubatilisha asidi ya tumbo na kuifanya isiwe na madhara.


MATIBABU MAALUM

Inawezekana kwamba dalili zako (za kutosagika kwa chakula) zinamaanisha kuwa na hali ambayo inahitaji matibabu zaidi.

Kupwa kwa asidi (Acid reflux)
Asidi ndani ya tumbo zinaweza kuchoma chini ya koo na kusababisha kiungulia, maradhi yatokanayo na kupwa yanaweza kuwa na sababu tofauti tofauti.

Ngiri (Hiatus hernia)
Kiasi cha mpasuko wa sehemu ya juu ya tumbo kupitia kiwambo (diaphgram) husababisha ngiri, ni kawaida sana hasa kwa watu wenye uzito mkubwa wanawake na wagonjwa wanasikia kuingulia pindi wanapolala kwa kunyooka au kujikunja.

Ugumu unaoota kwenye nyongo (gallstone)
Nyongo ni maji maji yenye mchanganyiko wa rangi ya njano na kijani (yellowish-green) yanayotengenezwa kaika ini, kisha yakahifadhiwa katika kibofu nyongo (gall bladder) na kupelekwa katika mahala ambapo husaidia kuyeyusha mafuta. Wakati mwengine kutosagika kwa chakula kunaweza kusababishwa na ugumu unaoota kwenye nyongo.

Vidonda vya tumbo (ulcer)
Kidonda chenye pepsini ni baka bichi ambalo hutokea katika kunyazi za tumbo au duodeni aisha kwa sababu kuna asidi nyingi sana ama utetelezi wenye kuzui asidi ni mdogo.

Kwahio ni muhimu kujitizama afya zetu ile tuepukane na matatizo madogo madogo kama hayo ambayo baadae huweza yakawa ni maradhi makubwa.​
 
Mkuu tumia dawa hii Tangawizi mara nyingi hutumika katika tiba ya indigestion, tumbo la hedhi na kuhara na kuiondoa dhiki tumbo. Ni bora kwa sababu ni baadhi ya nakala Enzymes digestive kutumika katika mchakato protini mwilini. Chemsha Tangawizi kwa maji ya moto uwe unakunywa kila siku kutwa mara 3 asubuhi mchana na jioni itakusaidia matatizo yako.

Pia waweza kutumia chai ya mdalasini uutwange upate unga wake changanya na maji uchemshe kisha unywe kama unavyokunywa chai itakusaidia hayo matatizo yako.
 
Hi jf members,
naombeni msaada wa dawa itakayonisaidia kutibu tumbo linalouma. Nimeenda kupima kwa daktari nikaambiwa enzymes zangu ni weak/dhaifu kwahiyo tumbo linakuwa na wakati mgumu sana kusaga chakula.
Pia daktari akashauri nisiwe nakula vyakula kama mayai na samaki na soda zenye gesi nyingi kama pepsi na kokakola.
Najua wataalamu mpo hapa jf, naombeni mnisaidie ktk hili na kwa wale wote waliokutana na hii case, i would appreciate their
moral and professional advise.
Nawatakieni j2 njema.
Thanks Allah bado uko hai.
Sijui ulitumia dawa gan.
 
Back
Top Bottom