Tiba Ya Kutopenda!

bi dada, siku hizi kuna wa kijijini?
nenda kule kijijini siku hizi, wewe uliyetoka mjini ndo utajiona si mali kitu............... chezea utandawazi
 

Mapenzi Ni Maelewano, Kama Kuna Kikwazo Kinachofanya Mwenzio Aone Hujafata Alichoomba Toka Kwako,Yafaa Kumtaarifu Na Mkafikia Muafaka...Yeye Hakuniambia Kama Kuna Suala Litakalomzuia Kufata Maombi Yangu Kwake!

Mkuu Nazani Unajua Suruali Hasa Za Kubana Zinavyochoresha Maungo Ya Hawa Viumbe,Mi Sikupenda Mpenzi Wangu Avae Suruali Wakti Yuko Mbali Nami!
Nilishamtaarifu Kuwa Sitaki!
 

Asante Ila Mimi Sio 'Dictator'
Nilimkuta Kavaa Sketi Na Nikamtaarifu kutopendezwa Na Suruali!
Siku Imekuwa Ndefu Kwangu,,,Nitajitahd Kufata Ushauri Wako!
 
Ni kweli mapenzi ni maelewano. Kama hupendi avae suruali za kubana basi mfahamishe hivyo badala ya kumpiga marufuku kuvaa suruali kabisa, na kama ni kicheche hata akivaa gauni la kwendea msikitini la kuziba hadi nyayo bado anaweza kuufanya ukicheche wake bila tatizo lolote.

 

Sasa Nimejifunza Jambo,Kina Kirefu,Utapata Maji Yalotulia!
Ngwe Ijayo Lazima Niwe Makini Na Mikazo Tata!
 
kwani umemuoa
kama hujamuoa kwanini unampangia masharti
kumzuia kuvaa suruali inahusu!!!!
hata angevaa gunia kama hajatulia hajatulia tu
inavyoonyesha huna msimamo na mahusiano yako.
 


The End of the world as we know it.
Aisee.
jana nimeona matangazo kibao yanayo wafaa watu kama wewe.

Wanavuta wapenzi,wanatoa pesa za majini,
wanakuunganisha na freemason,hata ahera ukitaka wana kupeleka.

Dunia ni yako,chagua lolote mkuu.
 
Ni Kweli Na Hasa Mkisikilizana Na Kushrikishana
kwa Mfano Kuna Siku Yeye Alinipangia Kuvaa Kaptura,Nikamtaarifu Kutokuwa Nayo Na Kumuomba Uchaguzi Mwingne Na Mambo Yakawa Sawa!

sio Dhambi Ila Kutonishirikisha Kama Atabadiri Nilichomuambia, Kulinikasirisha!


Ha ha,hili swali hua silipendi ila naomba nilitumie leo.
Wewe ni kabila gani eti?
 
kila Mtu Anakila Hasichopenda Mpenzi Wake Afanye...Kuna Wengne Hawapendi Wapenzi Wao Wavae Hereni N.k
Mimi Sipendi Mpenzi Wangu Avae Suruali Kwani Ilizidisha Chachu Ktk Muonekano Wa Maungo Yake!

He he he,aaaah.
Kweli dunia nzuri sana,asante kwa kuniongezea siku.
 
we Acha Tu "FP"..Kambi Inafuka Moshi,Najuta!

Mkubwa kama vipi mrudie mapemaa mzee, maana ukichelewa tu wale waliokuwa wanajiuliza nitampata lini watakuwa wameshaona kivuno.......utateseka mzee na kama unavyojua kipendacho roho tena:frusty:
 

kama nataka kukuonea huruma hivi.
Kua mwanaume bana,mwanaume hapendagi hivo.
Labda yeye kesha kuwahi kwa waganga,ukienda huko una haribu zaidi.

Nenda kwa YESU,yeye ana funika yote na hakuna wa kumzidi.
 
Uamuzi kweli ni wako, lakini kuna mamboya msingi ya kufikia uamuzi. Mapenzi ni kukubali kumfurahisha umpendaye na siyo kujifurahisha wewe binafsi. Kama mpenzi wako hajali kama utachukia au la kuna walakini. Kwa mawazo yangu ni kuwa kwake suruali ni ya thamani sana kwake kiasi kuwa yuko tayari kukukosa wewe abaki na suruali, lakini kwa upande mwingine na wewe uko tayari umkose yeye kuliko avae suruali. Kwa ufupi hakuna kati yenu aliyetari kukubali wazo la mwenzake wala hamko tayari kufurahishana, kila mmoja anataka kujifurahisha yeye binafsi. Suruali hapa ni symbol tu yakuonyesha jinsi mnavyopishana. Maisha ni kusikilizana si kusikilizwa wewe peke yako. Hebu tujiulize maswali rahisi tukitegemea kupata majibu magumu. Mpenzi wako akiacha kuvaa suruali atapata madhara gani? Na je; mpenzi wako akivaa suruali wewe binafsi utapoteza nini? Tukijibu maswali haya kwa ufasaha, tutakuta mahusiano yetu pengine ni bora zaidi kuliko mavazi kwa sababu tunaweza kuhusiana vizuri zaidi hata bila ya mavazi na kwa kweli wakati wa mahusiano ya asili kati mume na mke mavazi hayana nafasi.
 
kwani umemuoa
kama hujamuoa kwanini unampangia masharti
kumzuia kuvaa suruali inahusu!!!!
hata angevaa gunia kama hajatulia hajatulia tu
inavyoonyesha huna msimamo na mahusiano yako.

JICHO Msimamo Nnao Sana,si Ndo Maana Nahtaji Changu..Mwanzo Zilikuwa Hasira Nikasusa!
 
The End of the world as we know it.
Aisee.
jana nimeona matangazo kibao yanayo wafaa watu kama wewe.

Wanavuta wapenzi,wanatoa pesa za majini,
wanakuunganisha na freemason,hata ahera ukitaka wana kupeleka.

Dunia ni yako,chagua lolote mkuu.

Uhakika? nahtaji Muhanga Mwenye Ushuhuda Sababu Sihitaji Kuingia Kwa Matapeli!
Poa Lakin Nitakupm Rafiki!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…