Daniel Mbega
JF-Expert Member
- Mar 20, 2013
- 338
- 180
MSOMAJI wetu ameuliza kama kuna vipimo vikubwa zaidi na dawa za kutibu tatizo la moyo kupanuka. Anadai mwanzo alikuwa anapumua kwa shida akaenda hospitali, wakampiga picha ya X-Ray na kumwambia moyo wake umepanuka na mapigo ya moyo wake hayaendi vizuri. Alipewa dawa za mwezi mzima, katumia ila bado anapumua kwa shida.
Moyo Kupanuka ni Nini?
Moyo ni ogani ya misuli iliyopo kwa mwanadamu na wanyama, kazi yake kubwa ni kusambaza damu sehemu mbalimbali za mwili. Damu inayosambazwa huupa mwili oksijeni, virutubisho na kuondoa takamwili.
Moyo hupanuka ili kukabiliana na tatizo la misuli ya moyo kuharibika. Moyo kupanuka kunaweza kusababishwa na vitu vingi sana, ila sababu kuu zinazopelekea moyo kupanuka ni kupanda kwa shinikizo la damu (hypertension) na ugonjwa wa mishipa ya moyo kuziba (coronary artery disease).
Soma zaidi hapa => Tiba na Jinsi ya Kuishi na Moyo Mkubwa! | Fikra Pevu