Tiba Kwa kutumia Mshubiri ALOE VERA TONIC

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,331
33,146
MSHUBIRI.jpg



ALOE VERA

ama Mshubiri ni mmea ambao una sifa ya kipekee ya nguvu ya matibabu kuliko mmea mwengine wowote duniani.


Katika historia ya dunia, Aloe vera imetumika kwa manufaa mbali mbali ya kiafya, imetumika kama dawa asilia kwa vizazi mbali mbali.

Mmoja kati ya watu mashuhuri ambao wameshawahi kutumia Aloe vera maishani ni pamoja na M. Ghandi.

Mike Adams katika kitabu chake cha THE ALOE VERA MIRACLE imeonesha uwezo wa Aloe vera kwa:

1) Kupunguza kasi ya ukuwaji wa vimbe za kansa.
2) Kushusha cholesterol mwilini.
3) Kuongeza kinga ya mwili.
4) Kukinga mwili dhidi ya mawe kwenye figo.
5) Kuleta uwiano sahihi wa asidi ndani ya mwili.
6) Kutibu vidonda vya tumbo.
7) Kupunguza shinikizo la damu.
8) Huongeza kasi ya kuponya vidonda mwilini.
9) Huongeza ufanisi wa mfumo wa mmeng'enyo wa chakula.
10) Husaidia kuleta uwiano sahihi wa mmeng'enyo wa sukari na wanga mwilini.
11) Kupunguza uwezo wa kupata kansa ya utumbo mpana.
12) Kuboresha afya ya ngozi n.k.

ALOE VERA TONIC:
Hii ni juisi halisi ya Aloe vera iliyochanganywa kidogo na kitunguu saumu na ndimu ili kuipa nguvu zaidi na kuiboresha.

Asilimia 96% ya Aloe vera mna maji ambayo ndani yake mnapatikana:
i) Essential oil.
ii) Amino acid.
iii) Minerals.
iv) Vitamins
v) Enzymes.
vi) Glycoproteins na
vii) Acemannan.

Acemannan huupa mwili nguvu na kinga dhidi ya maradhi kwa sababu huipa nguvu T-lymphocyte cells ambayo huipa mwili kinga (immune booster).

Juisi ya Aloe vera kwa kunywa hunawirisha ngozi na kutibu maradhi mengi ya ngozi kama acne eczema.
Huondoa muwasho washo wa ngozi na vichomi kwa ndani ya mwili na huzuia kujikuna kuna. Pia huondoa alegi (Allergy).
Aloe vera hutibu maradhi mengi sana kwa sababu ukinywa huua virusi, bacteria na fangasi ndani ya damu na tumbo. Pia husafisha na kuondoa ndani ya damu na tumbo sumu na kemikali itokanayo na vyakula vya viwandani na madawa ya hospitali.

Aloe vera pia hutibu vidonda vya tumbo (ulcers), husaidia tumbo kusaga chakula vizuri, huboresha mzunguko mzuri wa damu, huwapa nafuu kubwa sana wale walioathirika kwa maradhi ya kisasa (HIV) kwa sababu huipa nguvu na kuiboresha chembechembe nyeupe hai ya damu (white blood cells). Kazi ya chembechembe nyeupe hai ya damu ni kuukinga mwili dhidi ya maradhi (immune system).

Huongeza kinga mwilini (CD4).

Pia hutibu kisukari, ngiri, malaria, chango la akina mama, pumu na matatizo ya mkojo.
Dozi: Kunywa kikombe kimoja cha kahawa kutwa mara mbili (1x2) asubuhi kabla ya chakula na usiku kabla ya kulala. Kikombe cha kahawa ni sawa na vijiko vitano vikubwa vya chakula (table spoon). Kwa tiba ya maradhi mengi sugu utumie angalau dozi ya lita moja ya Aloe vera.

Unaweza kutumia Aloe vera hata kama huumwi ikawa ni kama kinga ya maradhi na kusafisha damu, kutoa bacteria, virusi, fangasi na sumu ya kemikali ya madawa ya hospitali au vyakula vya viwandani.
Aloe vera pia huwafaa sana walioathirika kwa ulevi wa pombe au madawa ya kulevya kwa sababu hutoa mwilini hamu na athari ya ulevi huu. Kemikali ya ulevi huingia hadi ndani ya damu na kumfanya mhusika kuwa madawa haya ni sehemu ya damu yake na hawezi kuishi bila ya kuyatumia. Ukisafisha damu na kutoa athari hii ya pombe au madawa ya kulevya basi yaweza kupunguza na kukata hamu ya ulevi.

Pia hutibu na kuvipa nafuu viungo vya ndani vilivyoathirika au kuharibika kutokana na ulevi huu kama vile mapafu na utumbo. Pia huwafaa wavutaji sigara.

ONYO:
Aloe vera haitakiwa kutumika kwa mama mjamzito.

Ukiwa na Swali lolote usikose kunitafuta
Unaweza kunitafuta kwa Mawasiliano Dr. MziziMkavu Email barua ya pepe. fewgoodman@hotmail.com What's App na Viber +905344508169
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom