TIA Vs TAFORI

TIA Vs TAFORI

Dixionel

Member
Joined
Aug 12, 2012
Posts
13
Reaction score
0
Habarini ndugu zangu.

Mimi ni wa muda humu ila Nilipoteza Password na username, nikawa nasoma post na maoni tuu humu. Samahani kwa kutokuwa active humu!

Swala langu ni nimeitwa kwenye Interview mbili moja TIA- Tanzzania Institute of Accountancy na Nyingine ni TAFORI-Tanzania Forest Research Institute, sasa tatizo ni zote ni siku moja.

Mmoja ni Dar na nyingine ni Moro sasa sijui wapi pa kwenda kujaribu bahati yangu, labda kwa anayejua wapi ni afadhari.. TIA nafasi 4 ila wamitwa watu zaidi ya 300.. Tafori wamepiga simu tuu na nafasi ni mbili... TIA- mshahara ni TIASS 5 na Tafori ni PGSS 7.1 na hata sijui ndiyo sh. ngapi hizo.

Sasa naomba msaada wenu kwa hili, interview zote ni tarehe 25 April, mimi nipo Dar.

Naomba msaada wenu sana kwa hili..
 
mkuu kabla sijakujibu tafori umeomba nafasi gani?nipo tafori pia.
 
Nimeomba Information and Communication Technology Officer II mkuu
 
kwa hio unaweza kuja tafori,ingekua researcher ningekushauri vinginevyo.karibu.
 
kazi kweli.. yaani unaweza kusema haya ni majiribu .... kazi zinakuja kwa pamoja.. sasa unaweza kuchagua moja ukakosa ukaanza kulaani tuu.. Daaaah.. maisha haya..
 
kaka nipe zaidi basi.. maana bado nipo njia panda hapa....
 
kaka nipe zaidi basi.. maana bado nipo njia panda hapa....

nina uhakika ukipata utakaa HQ moro,then utakua unaenda vituoni kama kukiwa na tatizo linalobuhitaji,vituo viko 7
kibaha
lushoto
moshi
dom
tabora
simiyu/shinyanga
mufindi
 
mkuu kabla sijakujibu tafori umeomba nafasi gani?nipo tafori pia.

Mkuu TAFORI HQ ipo morogoro maeneo gani. I mean msamvu,kihonda mazimbu etc. Mana na mimi pia ni mhanga wa hiyo interview.
 
hii kiboko nafasi nne watu zaidi ya 300 yaani kusoma kote sasa tunaanza kuanza kuishi kwa imani inahuzunisha kweli kwel itafikia kipndi tutaanza kupishana na wanasiasa kwa waganga
 
My kaka, pole ila tambua imeshakaa hivyo basi ni lazima upige moyo konde na kuchagua mahala pa 1 na uende, fanya maamuzi mapema pata muda wa kujiweka sawa kwaajiri ya usaili. Mimi nakushauri nenda huko Tafori, ukifika tuliza bongo fanya interview, bongo isiwe slow sana, lazima uende na muda na umakini pia.

Nb: binafsi nakuombea ktk sala zangu nipo ktk maombi wiki hii ili uwe mmoja kati ya hao wanaokwenda kuajiriwa.
 
Nenda Morogoro ukatembee, huko TIA ni kamari...
 
Usiache TAFORI kaka

karibu Morogoro sana na ujisikie una wenyeji huku
 
mambo ya "TELL US ABOUT YOURSELF" go and tell people of Tafori who you are...
 
Nashukuru sana .. maana halo ni tete.... nitafanya maamuzi sahihi.....
 
ok hiyo ya mishahara tafuta kuna thread humu yaonesha hizo scale range...ila sijui kwa maoni yangu au ingekuwa mimi ningeenda tafori kwani idadi ya TIA ni kubwa sana japo ingekuwa siku tofauti huachi hata moja....mi pia niko ya TIA kwa IT officer ila watu wengi na naasi sita tuu ni balaaa aisee...so better tafori maana kwa simu u dnt expect watu wawe wengi sana kama huku tia
 
ok hiyo ya mishahara tafuta kuna thread humu yaonesha hizo scale range...ila sijui kwa maoni yangu au ingekuwa mimi ningeenda tafori kwani idadi ya TIA ni kubwa sana japo ingekuwa siku tofauti huachi hata moja....mi pia niko ya TIA kwa IT officer ila watu wengi na naasi sita tuu ni balaaa aisee...so better tafori maana kwa simu u dnt expect watu wawe wengi sana kama huku tia
Mbona Location yako ni dodoma kwani kuna TIA Dodoma?
 
Mbona Location yako ni dodoma kwani kuna TIA Dodoma?

ingekuwa kama sio TIA kuwa inagombewa ningekushauri TIA coz ngazi ya mishahara yao ni mizuri na kwa swala la kodi mishahara ya TIA ni exempt..coz sheria ya kukianziasha inaonesha kiko ndani ya taasisi na mamlaka za serikali zenye exempt kwa kodi kwa staff wake
 
Back
Top Bottom