Umesahau USA!
USA ina matatizo mengi ya racism kama sehemu nyingine, lakini huwezi kusema iko katika top ten ya racist countries in the world.
USA ni mfano wa jinsi gani racism inaweza kupigwa vita.
Baada ya kizazi cha hawa wanaoitwa "Baby Boomers" kuisha, racism itakuwa suala la historia Zaidi sehemu nyingi USA.
Jana nilienda kwenye "Dollar Store" moja karibu na kwangu. Huwa napenda kwenda kununua former bestsellers on the NY Times lists fiction/ nonfiction at a very discounted price. Nikakuta watu wamejipanga kwenye mstari wa checkout, working class people, weusi kwa weupe. Wale weusi wakaanza kuongelea jinsi bili za maji zinavyopanda, spontaneously wale weupe wakadakia - with that ever so present American instantaneous overfamiliarily - kuchangia mazungumzo hayo kwa kuelezea na wao jinsi bili zao za maji zilivyopanda.
Nikaona hapa ndoto ya Dr. Martin Luther King Jr. kidogo inatimia. Watu wanakubali kuwa pamoja na kushirikiana kutokana na matatizo yao ya pamoja ya uchumi. Hili linachukua umuhimu mkubwa kuliko race sehemu nyingi. Hususan kadiri muda unavyokwenda.
I am not so sure it is that easy in Russia. First of all blacks do not even exists as a sizable part of the citizenry, hence relegated to the peculiar subset of main society.
For that very reason, one cannot compare the US with any nation save for perhaps Brazil - which it far outpaces on the civil rights front-
Kuna watu wanabaguliwa kwa kuwa weusi wakiwa Africa Zaidi ya hata wanavyobaguliwa kwa kuwa weusi wakiwa Marekani!
Tatizo kubwa ilililonalo Marekani ni kwamba wao wanajiona kwamba ni Super nation na kwamba wanaweza kuwanyooshea vidole watu wengine, ukweli ni kwamba hakuna jamii Duniani ambapo watu wa aina fulani hawabaguliwi ila tatizo linapokuja fulani kujiona kwamba yeye ni mtakatifu wakati yeye mwenyewe hayuko kamili hiyo ndiyo shida aliyo nayo USA!
Ni mara ngapi Marekani inasema Urusi kuna Ubaguzi ingawaje hakuna wakulipinga hilo lkn Marekani anapata wapi uhalali wa kunyooshea Urusi au nchi nyingine yoyote Duniani khs Ubaguzi wakati mpaka leo hii asilimia zaidi 80 ya watu walio jela ni weusi wakati weusi ni asilimia 20 tu ya Wamarekani?
Kama kuna wageni wanakuwa attacked Urusi kwa ajili tu ya rangi yao ambapo ni kweli inatokea sana Urusi na sehemu nyingine lkn pia Marekani watu wanapigwa risasi kila siku kwa kuwa tu weusi ni hivi majuzi weusi wamepigwa risasi kanisani kwa sababu tu ni weusi ni mara ngapi tunasikia vijana weusi wanapigwa risasi na Polisi Marekani tena juzi mtoto wa miaka 12 alipigwa risasi na Polisi na uchunguzi unaonyesha walioufanya wenyewe Marekani kwamba ni rangi yake tu ndio iliyopelekea apigwe Risasi?
Hata Hollywood ni Wabaguzi akina Will Smith, Beyonce &Co. juzi kati hapa hata walisusia Oscar kwa sababu ya Ubaguzi wa mtu mweusi?
Hivyo nchi zote zina Ubaguzi na kila jamii ina mtu ambaye inamchukia na hakuna mwenye uhalali wa kumnyooshea mwingine kidole kwamba wewe ni mbaguzi zaidi, bali ni wote kama Binadamu tuungane na kujaribu kutatua tatizo na siyo kunyoosheana vidole na kutoa top ten sijui nani mbaguzi klk mwingine, huwo ndiyo ujumbe wangu!
mkuu umenena vyema sana na hivyo ndivyo ilivyo kilichobak hapo ni suala la uelewa.Marekani, kama nilivyosema, ina matatizo yake ya ubaguzi.
Lakini, imeweza kuweka misingi imara ya kupinga ubaguzi. Misingi ambayo hata Tanzania hatuna.
Marekani wana sheria kali za kupinga ubaguzi, si wa rangi tu, mpaka age discrimination, gender discrimination etc.Kuanzia Civil Rights mpaka Equal Employment Opportunity Zaidi ya hapo, suala la kuwa mbaguzi wa rangi ni suala la aibu kijamii. Ukiwa mbaguzi Marekani una side na the wrong side of history, the losing side. Ndiyo maana hata wanaofanya ubaguzi hawawezi kufanya ubaguzi wa wazi.
Tanzania mtu anaweza kuweka tangazo kwenye gazeti kwamba anatafuta mtu wa kuuza dukani, lakini lazima awe anaongea Gujarat. Marekani that is a violation of the Equal Opportunity Employment Act. Sisi hata hatuna hilo. Licha ya hilo, juzi mbunge kafura katoa kauli za kibaguzi bungeni kusema mtu mwingine si Mtanzania on the basis of color of skin, lakini hata sikusikia kwamba imezua mjadala.
Wiki kama mbili zilizopita, nilishangaa kuona tangazo la kazi ya kawaida limeweka sharti la umri, nakumbuka ulikuwa miaka 25 kama sikosei. Kazi yenyewe ya kutumia akili wala huwezi kusema mtu Zaidi ya umri huo hataweza, nikashangaa sana kuona hii blatant age discrimination. Nikasema Marekani habari ya ubaguzi wa umri wa wazi kama huu mtu anakushtaki na kukutoa mamilioni ya dola.
Marekani ina tatizo la "American Exceptionalism/ Superpower status" kama ulivyosema. Hii inaweza ilikuwa kweli zamani, lakini muda unavyozidi kwenda inazidi kuwa hadithi ya wanasiasa kuliko ukweli wa mambo.
Tofauti ya sehemu kama Marekani na China kwa mfano -China nao wabaguzi sana tu- ni kwamba, wakati Marekani ina tatizo la kujidai ina exceptionalism, watu watalisema hilo kama ni tatizo na kuliandikia mpaka vitabu. Kuna kitabu kimoja kizuri sana kinaongelea hilo cha Nancy Sodenberg kinaitwa "The Superpower Myth: The Use and Misuse of American Might". Kitabu kinaponda Marekani kujitutumua u superpower lakini kimepata mpaka foreword ya Bill Clinton, mtu aliyekuwa rais wa Marekani.
Nitafutie kitabu kama hicho cha Mchina kinachoisema China kwa kukalia kwa nguvu visiwa vya South China Sea, ambacho kina foreword ya Deng Xiaoping kwa mfano.
I can guarantee you, hakuna! Ukitaka kuandika kitabu critical tu, Communist party inakufunga.
Hapo tunaona kitu kingine muhimu kuhusu Marekani. Marekani inathamini sana pluralism kiasi kwamba huwezi kusema Marekani iko hivi au vile. Kwa sababu ukisema kuna watu wanaonadi sana Marekani kuwa Superpower na kuingilia mambo pengine, kuna wengine pia hawataki kabisa Marekani ijiingize katika mambo ya nchi nyingine.
Ukisema kuna Donald Trump racist, wengine watakwambia kuna Jimmy Carter mchungaji asiyetaka racism so much mpaka Waisraeli wamemuona anajiweka na Wapalestina, kitu ambacho hakikutegemewa kwa mchungaji.
Kwa hiyo Marekani just defies these simplistic categorization because it is too complex, too diverse and too experimental to be fitted into any of the old world categorizations.
Marekani, kama nilivyosema, ina matatizo yake ya ubaguzi.
Lakini, imeweza kuweka misingi imara ya kupinga ubaguzi. Misingi ambayo hata Tanzania hatuna.
Marekani wana sheria kali za kupinga ubaguzi, si wa rangi tu, mpaka age discrimination, gender discrimination etc.Kuanzia Civil Rights mpaka Equal Employment Opportunity Zaidi ya hapo, suala la kuwa mbaguzi wa rangi ni suala la aibu kijamii. Ukiwa mbaguzi Marekani una side na the wrong side of history, the losing side. Ndiyo maana hata wanaofanya ubaguzi hawawezi kufanya ubaguzi wa wazi.
Tanzania mtu anaweza kuweka tangazo kwenye gazeti kwamba anatafuta mtu wa kuuza dukani, lakini lazima awe anaongea Gujarat. Marekani that is a violation of the Equal Opportunity Employment Act. Sisi hata hatuna hilo. Licha ya hilo, juzi mbunge kafura katoa kauli za kibaguzi bungeni kusema mtu mwingine si Mtanzania on the basis of color of skin, lakini hata sikusikia kwamba imezua mjadala.
Wiki kama mbili zilizopita, nilishangaa kuona tangazo la kazi ya kawaida limeweka sharti la umri, nakumbuka ulikuwa miaka 25 kama sikosei. Kazi yenyewe ya kutumia akili wala huwezi kusema mtu Zaidi ya umri huo hataweza, nikashangaa sana kuona hii blatant age discrimination. Nikasema Marekani habari ya ubaguzi wa umri wa wazi kama huu mtu anakushtaki na kukutoa mamilioni ya dola.
Marekani ina tatizo la "American Exceptionalism/ Superpower status" kama ulivyosema. Hii inaweza ilikuwa kweli zamani, lakini muda unavyozidi kwenda inazidi kuwa hadithi ya wanasiasa kuliko ukweli wa mambo.
Tofauti ya sehemu kama Marekani na China kwa mfano -China nao wabaguzi sana tu- ni kwamba, wakati Marekani ina tatizo la kujidai ina exceptionalism, watu watalisema hilo kama ni tatizo na kuliandikia mpaka vitabu. Kuna kitabu kimoja kizuri sana kinaongelea hilo cha Nancy Sodenberg kinaitwa "The Superpower Myth: The Use and Misuse of American Might". Kitabu kinaponda Marekani kujitutumua u superpower lakini kimepata mpaka foreword ya Bill Clinton, mtu aliyekuwa rais wa Marekani.
Nitafutie kitabu kama hicho cha Mchina kinachoisema China kwa kukalia kwa nguvu visiwa vya South China Sea, ambacho kina foreword ya Deng Xiaoping kwa mfano.
I can guarantee you, hakuna! Ukitaka kuandika kitabu critical tu, Communist party inakufunga.
Hapo tunaona kitu kingine muhimu kuhusu Marekani. Marekani inathamini sana pluralism kiasi kwamba huwezi kusema Marekani iko hivi au vile. Kwa sababu ukisema kuna watu wanaonadi sana Marekani kuwa Superpower na kuingilia mambo pengine, kuna wengine pia hawataki kabisa Marekani ijiingize katika mambo ya nchi nyingine.
Ukisema kuna Donald Trump racist, wengine watakwambia kuna Jimmy Carter mchungaji asiyetaka racism so much mpaka Waisraeli wamemuona anajiweka na Wapalestina, kitu ambacho hakikutegemewa kwa mchungaji.
Kwa hiyo Marekani just defies these simplistic categorization because it is too complex, too diverse and too experimental to be fitted into any of the old world categorizations.
hiyo ya kusoma makongo na kutibiwa sijui wapi huko kwa wahindi tu bali hata kwa watz weusi wenye fedha zao hawapeleki watoto wao huko, hapa bugando na sekou toure hospital tunapishana na wahindi kibao kutafuta tiba. njoo pamba sec, mwanza sec uone wahindi wanapiga book.Ndiyo nakwambia hiyo ndiyo maana ya Ubaguzi, kama hauna Power hauwezi kuwa mbaguzi utambagua nani? na kivipi? Ulishawahi kukutana na Muhindi hapa TanZania analalamika kubaguliwa? Lkn ni Watz wangapi wanalalamika kubaguliwa na Wahindi hapa hapa TanZania ingawaje sisi ni asilimia zaidi ya 98% ya Watz wakati Wahindi wote hawafiki hata laki tano?
Utambaguaje mtu unayemtegemea akupe mkate wako wa kila siku uishi?
Bakhresa hawezi kulalamika kubaguliwa TanZania kwa maana hakuna anayemgabua, ni nani anambagua Bakhresa na kivipi? na huwo Ubaguzi unamuathiri Bakhresa nini? Utambaguaje mtu ambaye ndiyo anakuajiri yaani unamuhitaji ili uishi?
Mtu anayebaguliwa ina maana ananyimwa haki zake za msingi kuishi kikamilifu kama binadamu wengine ktk jamii yake na hii ikiwa ni pamoja na haki ya kufanya kazi, makazi, huduma za Afya na hapa kwa mfano ni lini ulisikia Muhindia anakwenda kutibiwa Muhimbili, Mwananyamala au sijui Kriuki Memorial? lkn ni Watz wangapi weusi kama mimi tunakwenda kutibiwa Hindu mandal, Aga Khan au Regency? mambo ya Elimu ni lini ulisikia Muhindi anang'ang'ania kusoma Makongo, sijui Turiani lkn ni Watz wangapi weusi tunajazana Shule za Wahindi kama Shabaan Robert, Al Muntazir, n.k , ustawi jamii ni lini ulisikia Muhindi au Mwarabu TZ amezuia kuingia club au Hotelini? Lkn ni mara ngapi tunasikia Watz weusi kama mimi wanalia kuzuia kuingia Hoteli za Wahindi? Hata coco beach tu kuna kipindi hapo nyuma Wahindi walikuwa na sehemu yao watu walilalamika lkn mbona hakuna Muhindi aliyekuwa anang'ang'ania kuja sehemu za kwetu na kudai kuwa anabaguliwa?
Sasa utasema je mtu mwenye access na mambo yote haya anabaguliwa na mtu asiye na kitu?
hiyo ya kusoma makongo na kutibiwa sijui wapi huko kwa wahindi tu bali hata kwa watz weusi wenye fedha zao hawapeleki watoto wao huko, hapa bugando na sekou toure hospital tunapishana na wahindi kibao kutafuta tiba. njoo pamba sec, mwanza sec uone wahindi wanapiga book.
marekani ni wabaguzi sawa lakin tz ni wabaguzi zaidi, nenda kwenye ofisi ya mhaya unatafuta kazi afu kuna mhaya mwingine anataka hiyo kazi, Trump alitoa maneno ya kibaguzi ila kwa kuwa marekani inapinga ubaguzi nadhani ulishuhudia reactions ikiwemo na mkuu wa nchi kukemea, mama yule wa zanzibar marehemu kaongea ubaguzi bungeni huku akishangiliwa na wabunge wenzie, spika na mawaziri, nadhani na rais alikuwa anashangilia kule alikokuwa na ndo maana hakukea tabia ile
Kama nilivyosema hakuna nchi iliyokamilika na kwanza kama kuna mfano ambao tunaweza kutafuta kuhusu ukamilifu wa au nchi inayokaribia ukamilifu Marekani haiwezi kuwemo hata kwenye top 10 za nchi zote Duniani!
Na hayo yote uliyosema khs Uchina au nchi yetu ni sawa lkn tofauti ni kwamba sijawahi kusikia Wachina au sisi tukisema kwamba sisi ni jamii bora Duniani na kuwanyooshea wengine kidole, Uchina pmj na matatizo yake yote kama jamii inafahamu kwamba ina safari ndefu na ina changamoto nyingi na kila Kiongozi wa Uchina hulisema hilo na sijawahi kusikia Kiongozi wa Uchina akiinyoshea Marekani au nchi nyingie kidole kwamba hakuna Demokrasia au sijui unakosea kufanya hivi!
Ni ajabu sana unaisifia Marekani na kuisema Uchina kwamba inakalia kimabavu S. China Sea, na vipi kuhusu Marekani inakalia nchi ngapi kimabavu hapa Duniani? Marekani ina military base ngapi Dunia hii, Marekani imesababisha vita na vifo vya watu wangapi Dunia hii, Marekani imefanya coup de tat ngapi Dunia hii kuanzia covert operation irani, Guatemala, Chile mpaka Kongo ?Kuna vita vingapi vinaendelea hapa Duniani vilivyosababishwa na Marekani mpka upate uhalali wa kuishutumu Uchina kuikalia South China Sea tena Sea ambayo inashea mpaka wake kijiografia angalau wanaweza kuwa na sababu?
Hivyo hayo yote uliyoyaorodhesha ni cosmetic tu na Marekani kama nchi ni wazuri sana kwenye mambo cosmetic, kujaribu kuwaonyesha wengine jinsi gani walivyokuwa wazuri na democratic lkn ukweli unabakiwa kuwa ikiwa kama Marekani ni moja kati ya nchi tajiri Duniani kiuchumi na lkn ni moja kazi ya unequaled countries hapa Duniani ukilinganisha na nchi ambazo ziko ngazi sawa ya kimaendeleo na Marekani, Marekani ndiyo nchi yenye homeless wengi klk nchi yoyote ile iliyo ngazi sawa kimaendeleo, ukija kwenye mambo ya afya wala ndiyo usiseme, mpaka leo hii Marekani inashutumiwa hata mashirika ya Kimataifa kama amnesty International kwa kunyonga watu, kuna wafungwa wengi Marekani wamefungwa zaidi ya Miaka 40 bila ya hatia na wengine walishanyongwa bila ya hatia lkn hiyo ni mada nyingine na ngumu!
Kama hujawahi kusikia Wachina wakisema wao ni jamii bora kabisa duniani, rudi kusoma historia ya China uelewe China ilipotoka na ilipo.
Wachina walianza kuendelea kisayansi kabla ya Ulaya. Wakagundua vitu vingi, ikiwemo gunpowder.
Kwa habari Zaidi soma Wiki hii hapa List of Chinese inventions - Wikipedia, the free encyclopedia
Kilichowaponza ni hiyo habari ya exceptionalism na kujiona wao ni superpower. Wachina walianza kuja Africa kabla ya wazungu, mfalme wao akapiga marufuku safari za nje, kwa kusema mnaenda kutafuta nini mashenzini huko wakati hapa kwetu China ndiyo kitovu cha dunia nzima.
Utasemaje China haijawahi kusema ndiyo kinara cha dunia?
Ukisema ni ajabu kwamba naisema China wakati Marekani inakalia nchi ngapi, wakati nishakuonyesha tofauti ya China na Marekani (Marekani wananchi wanaweza kumpiga vigongo rais katika protest, kumkatiza hotuba, wakti China ukifanya hivyo unanyongwa. So where is the comparison?
Unaweza kulinganisha Marekani na China kwa income inequality?
Unaweza kulinganisha Marekani na China kwa capital punishment?
Unataka tuchanbue habari kwa namba hapa?
hata kuoa mtoto wa rais, mtoto wa mengi ni sifa pia. kuoa mhaya je?! wanawake wahaya wanabaguliwa kuolewa katika nchi yaoNimekwisha sema ubaguzi ni Power na kama hauna Power hauwezi kuwa mbaguzi, na sisi kama watu weusi hatuna Power popote pale Dunia hii hata kwenye nchi yetu wenyewe hivyo hatuwezi kuwa wabaguzi!
Yaani hakuna mahali ambapo mgeni atajisikia kubaguliwa TanZania kwanza ni kinyume chake na atakachokiona na kukishuhudia ni hali ya kutukuzwa na kumfanya yeye bila hata ya kupenda kutubagua, kuanza kubagua, kama Mzungu, Mchina au hata Muhindi akija leo TZ kama hana hata chembe ya ubaguzi akiishi hapa kwetu sisi kama jamii tutamkumbusha kwamba unapaswa kutubagua na hatimaye ataanza kutubagua automatic!
Ni mara ngapi umesikia Mtz mweusi akilalamika kwamba hawezi kupata Mwanamke wa Kihindi au Kiarabu? Sasa ni lini ulisikia Muhindi au Mwarabu analalamika kwamba hawezi kupata mwanamke wa wa Kitanzania mweusi? Na kwa nini?
Ni kwa nini kwetu sisi kuoa Mwarabu, Muhindi, Mzungu au mgeni yoyote yule ni sifa kubwa na jambo la kujivunia klk kuoa wanawake wetu weusi lkn kwa jamii nyingine zote kuoa au kuolewa na sisi ni jambo la aibu na la kujificha?
hata kuoa mtoto wa rais, mtoto wa mengi ni sifa pia. kuoa mhaya je?! wanawake wahaya wanabaguliwa kuolewa katika nchi yao
Marekani ni nani?Kama kuna kitu Marekani anaweza kukifanya vizuri au sijui niseme Mzungu ni kudanganya watu, hayo yote ambayo wanaita Demokrasia ni uongo mtupu na una lengo moja tu la kupumbaza na kuendelea kutawala watu, nchi zote za Wazungu zinatawaliwa na maelite na tofauti tuu iliyopo kati ya maelite wakizungu na tuseme ya sehemu nyingine kama Uchina maelite Wakizungu wako clever wana experience kubwa sana na hii ni kutokana na mapinduzi yaliyofanywa huko nyuma kama mapinduzi ya Ufaransa na Napoleon na jamii zao hivyo wamejifunza na wanakwenda wakibadilika kulingana na muda!
Lkn lengo ni lile lile kutawala walio wengi, hivyo mambo sijui ya kuandamana, kuwa hacker wakati kiongozi akihutubia ni moja kati ya hizo mbinu za kuwafanya watawaliwa wajione kwamba wanaahueni na sababu kubwa ya wao maelite kuruhusu hayo mambo ni kwamba wanajua hayana madhara yoyote yale kwenye utawala wao na ndiyo maana maandamano yanaruhusiwa kwa kiasi fulani lkn wakiona kwamba yana madhara basi hata huyapiga marufuku na hutumia Polisi na nguvu mfano Genoa Italia ambako waandamanaji wengi waliumizwa na Polisi na wengine kukamatwa!
Kama maandamano yangekuwa na uwezo wa kubadilisha chochote kile maelite wa Kizungu wasinge yaruhusu na ndiyo maana Marekani akishaamua kwenda vitani haijalishi wananchi watapinga na kuandamana kiasi gani, vitani wataenda, Bush Wamarekani na Dunia nzima waliandamana mpaka kufanya show ya Bush kurushiwa kiatu lkn bado Marekani alipeleka majeshi vitani na mpaka leo hii hata UN wameshathibitisha kwamba ushahidi walioutoa akina Bush ulikuwa wa uongo hakuna hatua yoyote ile iliyochukuliwa kwa wahusika na bado Obama anaendelea kutumia majeshi kuvamia nchi nyingine kana kwamba hakuna kilichotokea kama Libya, Syria, Somalia, Mali, Chad, Irak, n.k
Hivyo tofauti ni kwamba watawala wa Kizungu ni wajanja na wanajua kuwadanganya na watawaliwa kwa vitu cosmetic kama sijui constitutional monarch lkn hakuna anayemchagua Mfalme wala anayeweza kumfukuza kazi, yeye pamoja na familia yake wanaishi kwa jasho la Wanachi wao na wao Wafalme na familia zao hawafanyi kazi!
Marekani ni nani?
Mzungu ni nani?
Wamarekani na wazingu kuanzia Winston Churchill mpaka H.L Mencken washaipaka demokrasia.
Wameandika vitabu.
Umesoma?
Au ndiyo unahakikisha habari za "if you wanna hide something from a nigga, put it in a book" ?
Kanjubai naona unashusha kiswahili kizuri , wafundishe na wenzio maana sijui kiswahili chao mwalimu wao nani hata akikaa bongo miaka 10hivi yule donald trumph anatoka russia/pakistan/india? maana kila siku wananchi wanamsapoti sana kwa kuhubiri ubaguzi na hakuna chombo chochote cha sheria kikichukua jukumu la kumkemea achilia mbali kumshitaki. vipi kuhusu wale wayahudi waki-export wahabeshi na kadhalika?
bila shak hiyo list yako imeandaliwa na wazungu.
Sasa ukiua si lazima na wewe uuawe? Tatizo liko wapi?
Huko China hata balozi wa nyumba kumi mweusi hakuna. At least US wana prez Jaluo, kuna black governors, senators, congressmen, sherrifs,etc
If you have the right brain and you are smart, then opportunities are plenty in the US.
Kitu gani hujaelewa? Nifafanue kipi?
Sijakuelewa unachomaanisha unaweza kufafanua, kama ukipenda!