Nyakijooga
JF-Expert Member
- Dec 9, 2018
- 427
- 666
Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) umelaani suala la Jeshi la Polisi kuwashikilia kwa zaidi ya saa 24 waandishi wawili wa habari mkoani Arusha bila kuwapa dhamana.
Waandishi hao ni Baraka Lucas wa Jambo TV na Ezekiel Mollel wa Manara TV, ambao walikamatwa Septemba 6, 2025, wakituhumiwa kuendesha televisheni mtandaoni bila leseni kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).
Akizungumza na waandishi wa habari Septemba 10, 2025, Mratibu Kitaifa wa THRDC, Wakili Onesmo Olengurumwa amesema kuwa kuwashikilia waandishi hao kwa zaidi ya saa 24 bila kuwapa dhamana wakati makosa yao yanadhaminika ni ukiukaji wa sheria za nchi.
Olengurumwa ameendelea kufafanua kuwa, mtu yoyote anayefikishwa kituo cha polisi ana haki ya kufikishwa mahakamani kwa ajili ya kusomewa mashtaka yanayomkabili, na hatua ya kushikilia waandishi bila kufuata taratibu hizo ni kinyume na misingi ya haki za binadamu na utawala wa sheria.
THRDC imetoa wito kwa mamlaka husika kuhakikishawanahabari wanapata haki zao zote za kimsingi na bila kukiuka taratibu za kisheria.