THRDC: Mpaka sasa hatujui Boniface Mwangi (Kenya) na Agather Atuhaire (Uganda) wako wapi

Nyakijooga

JF-Expert Member
Joined
Dec 9, 2018
Posts
427
Reaction score
666
Mratibu Kitaifa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) Wakili Onesmo Olengurumwa, amelishauri Jeshi la Polisi kutoa taarifa kwa umma juu ya wapi walipo Wanahabari Boniface Mwangi kutoka Kenya na Agatha Atuhaire wa Uganda ili kuepusha taharuki zozote zinazoweza kujitokeza kutokana na ukimya wao.

Your browser is not able to display this video.

Hayo ameyasema leo Mei 21,2025 Wakati akizungumza na waandishi wa habari, Jijiji Dar es salaam.

Wakili Olengurumwa amesema kuwa hapo jana zilitolewa taarifa kuwa wanahabari hao wamerudishwa kwenye nchi zao jambo ambalo halikufanyika, hivyo amelisihi jeshi hilo kuwa kama kuna kesi zinazowakabili wanahabari hao taratibu za kisheria zifuatwe ili wafikishwe mahakamani na kama hakuna warudishwe kwenye nchi zao.

Ameongeza kuwa kitendo cha kuwashikilia , kuzuia Mawakili kuwapa huduma kama wateja wao kunajenga imani nje ya nchi kuwa huenda nchi haiheshimu misingi ya sheria na Haki za Binadamu.

Amesema hambo hilo linatia Doa taifa na kuwa ingetumika zaidi Busara katika hilo.

Wanahabari Boniface Mwangi kutoka Kenya, na Agatha Atuhaire, mwanahabari na wakili kutoka Uganda, waliripotiwa kukamatwa na kushikiliwa katika Kituo cha Polisi Kati jijini Dar es Salaam, Tanzania kwa madai ya kutoa taarifa za uongo ili kuingia nchini ambapo walifika nchini Tanzania tarehe 18 Mei 2025.

Mei 19,2025, THRDC ilitoa wito kwa jeshi la Polisi kuheshimu viwango vya kimataifa vya haki za binadamu vinavyohusu watu walioko kizuizini.

Chanzo : Watetezi tv
 
Kazi kweli kweli, naona kila mtu atafikiwa kwa majira yake...
 
Kuna mtu aliwahi kuandika humu kwamba, Kule kwenye kampuni kuna mtu anaviziwa ajae kwenye mfumo...
britanicca na yoga Semeni kitu
 
kama ya Mdude, they are gone. Kwa tamk la Samia juzi aliwapa go ahead kutekeleza lolote
 
Kuna anayetisha watu ili ashinde uchaguzi. Keshaona Tundu Lisu anaweza kukalia kiti kama sheria za upendeleo zikifutwa
 
Nchi yangu bhana inaraha Sana,, inamaana tulikuwa hatujui kama waliyoyafanya ni kosa kisheria kwa mujibu wa taratibu na murua wa kiuhamiaji kwa nchi yetu! basi Kuna kila sababu yakutojua wako wapi, maana nguvu ya watetez ipo social media na sio actual ground! Itunzwe Amani ya afrika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…