This is what we call smart dating

Alvin A.

JF-Expert Member
Oct 14, 2016
2,727
3,629
Hakuna mwanaume aliye single ambaye kila siku akitoka nyumbani kwake anajisemea ngoja nitafute mke kama vile anavyotafuta funguo, simu au fedha aliyopoteza. Haipo hiyo.
.
Mwanaume siku zote anataka awe na mwanamke katika uchumba na katika safari hiyo ya mahusiano wazo la kukuoa wewe au mwingine humjia kutokana na namna alivyo-experience mahusiano hayo.
.
Na pale mwanaume anapokuchagua wewe, huwa ni wewe tu anayekuhitaji. Wala mwanamke hutatumia nguvu nyingi kuyafanya mahusiano hayo yanyooke. Sasa baadhi ya wanawake wamejipa hadi kazi ya ushushushu wa kutafuta ni nani anatoka na mwanaume wake, na wanapobaini unakuta wanamchimba hadi mkwara huyo wanaembaini. Hiyo haisaidii kama mwanaume mwenyewe hana jitihada ya kusimamia mahusiano hayo.
.
Ndiyo maana mahusiano mengi yaliyosimama ni yale ambayo mwanaume ameamua kuyasimamia kidete kuhakikisha mwanamke wake anayo furaha.
.
Wanawake wengi labda kwa kunogewa na mahusiano wamekuwa wakijiachia mno, kuwa-post mabae zao kwenye mitandao ya kijamii na wengine kufikia hatua ya kuwazalia kabisa wakiamini kuwa hao ndio tayari Wanaume zao wa ndoa. Lakini baadae kinachokujaga kuwatokea anajua Mungu mwenyewe.
.
Dada zetu wajifunze kuwa na uvumilivu, unapokuwa na mwanaume kwenye mahusiano usijione kama ndio umeshafika, ukahamisha na akili zako zote bila kufikiria mustakabali wa maisha yako. Jifunze kuwa na kifua cha kuficha mambo mpaka pale utakapoona kuna uelekeo chanya wa mahusiano hayo.
.
Unavyoingia katika mahusiano, beba na akili zako, usiziache nyuma. Ni rahisi mno kufahamu
u-serious wa mtu katika mahusiano endapo utashirikisha akili yako.
.
Usijichukulie majukumu ya kuwa Mke wakati bado hata hujaolewa. Maisha hayaendi hivyo. Na unavyoona mahala ulipo hapaeleweki, ondoka mapema kabla mambo hayajakuharibikia.
.
Nimeshawahi kusema kwamba, MALENGO YA MAHUSIANO hayahusiani na kupiga selfie pamoja, kukumbatiana, kushikana mikono, kupelekana maeneo ya starehe na kuvaa nguo zinazofanana.
.
Hizo mbwembwe waachieni vijana wa Vyuoni. MALENGO YA MAHUSIANO ni kuwa muaminifu na mkweli, kuwa committed, kushirikiana pamoja ili kuweza kufikia ndoto za ku-win ECONOMIC FREEDOM, kujijenga kuwa bora zaidi na kusaidiana kwa pamoja kuwa karibu na MUNGU.

Na mambo ya kupayukapayuka kuhusiana na mpenzi wako anapokukosea waachie akina Mwajuma Ndala Ndefu

Hope tumeelewana.
FB_IMG_1571034349791.jpeg
 
Mwenye masikio na asikie.

Toka utandawazi ulipoingia ndipo shida hizi zilipoanzia. Na hizi smartphone hizi!
Mtu akipata bwana, basi atamtupia kila kona ya kila mtandao ili watu wamuone bila kujua kuwa mambo hubadilika.

Sasa mambo yanapobadilika ndipo kwa aibu na hasira za huzuni, huanza kushambuliana kwa matusi mitandaoni.

Mungu atusaidie sana aisee
 
Ni kweli alichosema Mtoa Mada, hata mm wakati nasoma kidato cha Pili kuna Dada nilikuwa nampenda sana sema akazingua, nikaona isiwe kesi nikamtafuna rafiki yake
 
Uzi wa pili nakutana na hii comment
Ni kweli alichosema Mtoa Mada, hata mm wakati nasoma kidato cha Pili kuna Dada nilikuwa nampenda sana sema akazingua, nikaona isiwe kesi nikamtafuna rafiki yake
Kweli itakuwa alikuzingua vilivyo ukautulia mzigo pembeni yake. Pole sana.
 
Mwenye masikio na asikie.

Toka utandawazi ulipoingia ndipo shida hizi zilipoanzia. Na hizi smartphone hizi!
Mtu akipata bwana, basi atamtupia kila kona ya kila mtandao ili watu wamuone bila kujua kuwa mambo hubadilika.

Sasa mambo yanapobadilika ndipo kwa aibu na hasira za huzuni, huanza kushambuliana kwa matusi mitandaoni.

Mungu atusaidie sana aisee
Usimuhusishe Mungu na huo ukumbafu.
 
Mwenye masikio na asikie.

Toka utandawazi ulipoingia ndipo shida hizi zilipoanzia. Na hizi smartphone hizi!
Mtu akipata bwana, basi atamtupia kila kona ya kila mtandao ili watu wamuone bila kujua kuwa mambo hubadilika.

Sasa mambo yanapobadilika ndipo kwa aibu na hasira za huzuni, huanza kushambuliana kwa matusi mitandaoni.

Mungu atusaidie sana aisee
Yeah, wasikie na waelewe
 
Back
Top Bottom