Kwanza ndugu Yahya itoe hiyo kampuni ya ZUKU maana yenyewe haihusiki na mfumo huo maana ukiizungumzia zuku ni sawa na kuzungumzia DSTV hii ni kwa maelezo ya akina Mungi katika kipindi cha Malumbano ya hoja kupitia Itv,na nikukumbushe kuwa makampuni yaliyopewa leseni ni matatu tu yaani TING,STARTIMES,na BASIC TRANSMISION tu.
Swali langu la kwanza kwa akina Inocent Mungi,Mlikuwa mnafukuzwa na nani hadi kukimbia kuweka deadline ya analogia kuwa 31 dec 2012 hali makampuni mliyoyapa leseni yakiwa hayajajitosheleza kwenye usambazaji wa miundombinu yao?,hamuoni kuwa hiyo deadline mliyokuwa mnaitoa haikuwa inawahusu wananchi bali ilikuwa inawahusu makampuni mliyoyapatia leseni.?