Thinking Aloud: Hongera JF kulisaidia Taifa, "Atakuwa anaingia JF in person na kutusoma!". 2021 let's be more responsible, more strategic

Kundi lako ni lipi.
 
Kwanza mtoto akiwa tumboni(?),Kuna vitu hategemei toka kwa mama.Mfano damu.So inatuuma kupotosha.
 
Wanabodi, mimi ni miongoni mwa wana jf, tuliandika mengi kumhusu rais wetu, Dr. John Pombe Joseph Magufuli, hivyo kipindi hiki cha maombolezo, napitia baadhi ya mabandiko kwa ajili ya kumuoga rasmi.
Japo umetangulia, lakini kauli zako, maono yako na kile ulichokiamini, kitabaki na sisi Milele.
Sisi tulikupenda, lakini Mungu amekupenda zaidi.
Bwana Alitoa, Bwana Ametwaa, Jina Lake Lihimidiwe!.
Raha ya Milele Umpe Ee Bwana, na Mwanga wa Milele, Umuangazie, Apumzike kwa Amani...Amina x 3.
RIP Dr. John Pombe Joseph Magufuli
Buriani ya kuonana...
Paskali
 
Uhonyala.
 
Pasco, waingereza wanasema, "you have said it all".
It takes generations to get such a visionary and strategic leader. Ila pia waswahili tuna msemo, watu wazuri huwa hawadumu kwa muda mrefu.
Kwa ufupi sana, JPM atabaki kukumbukwa kwa yale aliyosema na kutenda. Kuna mengi kafanya kwa niaba ya waliomtangulia (kuijenga Dodoma yenye hadhi na mkao wa Makao Makuu ya Serikali, Ujenzi wa bwawa la Nyerere kufua umeme), na kuna mengine kafanya kama matamanio yake kwa Watanzania kama ujenzi wa hospitali za rufaa karibu kila mkoa, ukarabati wa mashule ya sekondari, kuipa vifaa vya kisasa JKCI na Muhimbili ili kupunguza gharama za tiba kwa Watanzania kwenda nje kutibiwa.
JPM aliwaweka "watu kati", ili Tanzania ipate hisa kwenye mgodi wa Barrick na Bart Airtel;

Kwa hakika kuna mengi ya kumsemea kwa mema, japo kuna wengine watamlaumu kwa ubaya; itoshe kuandika networth yake ni kubwa kwa maana ya mema aliyofanya yanakuwa ni mengi kuliko mabaya macheche ambayo kila binadamu anaweza kuwa nayo.

Faraja ya Mungu alie juu na iwe juu ya familia ya JPM, viongozi na Watanzania kwa ujumla. JPM, utabaki kuwa kiongozi bora kabisa kwa "legacy" uliyoiacha.

Kwaheri Mwl John Pombe Magufuli, kwaheri Dr. John Pombe Magufuli; Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 2015-2021
 
Japo hili ni wazi la siku nyingi lakini bado liko valid, leo serikali ime recognises rasmi uwepo wa jf, kwa Waziri wa habari kutembelea jf, hivyo hapa nakumbushia tuu kuwa jf na sisi tumo!.
Hongera sana Mkuu Maxence Melo , this is the beginning of government official recognition.
Ile the JF spirit ya "be the first to know" worked very well hata juzi kwenye hili tukio la Ubalozi wa Ufaransa ni JF ndio wa kwanza kutoa breaking news tangu jamaa akiwa Salender bridge.

Big up Maxence Melo,
Big up wana Jf.
Let's keep up the jf spirit
Long Live JF
P
 
We mzee hulali?😂 congrats maxence my blooh
 
Kama naniliu alikuwa anaingia jf in person, then hata nanilii humu anaingia!. Lets be more responsible, more objective, tumsaidie na kulisaidia Taifa letu.
P
 
Yule alikuwa anashuka mwenyewe jf in person, huyu sina uhakika sana, ila ikitokea na yeye anashuka huku in person, nina imani anaziona hoja zetu humu na atazifanyia kazi!.
Mungu ibariki Tanzania
P
 
Yule alikuwa anashuka mwenyewe jf in person, huyu sina uhakika sana, ila ikitokea na yeye anashuka huku in person, nina imani anaziona hoja zetu humu na atazifanyia kazi!.
Mungu ibariki Tanzania
P
Poa P for your advocacy inawezekana siku akasikia kilo chetu🤔
 
Rais Samia:

Huwa napitia Jamiiforums naangalia maoni yenu kule ndani, nasoma nnacheka,

Duh...!, kumbe na humu Mama huwa anaingia mwenyewe in person!.
Haya sasa Mama kasema mwenyewe!.
Angalieni bandiko hili mimi nilisema nini!.
I was damm right!.

P
 
Kuna baadhi ya vitu tunaviandika humu jf, kwenye baadhi ya hoja, tunaonekana kama tunajiandikia tuu for nothing, it's a wastage of time, money and resources, but believe it or not, it's not nothing, it's something na mfano hai ni bandiko hili, angalia nilishauri nini na angalia matokeo Mkutano Maalum wa Baraza la vyama vya siasa na wadau wa Demokrasia, January 3, 2024

Hivyo tuendelee kuandika na kushauri, baadhi ya hoja zetu humu zinasaidia.

Jf lets keep up.
Paskali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…