Thinking Aloud: Hongera JF kulisaidia Taifa, "Atakuwa anaingia JF in person na kutusoma!". 2021 let's be more responsible, more strategic

Asante mkuu kwa kuonyesha ukweli.
Ni vizuri viongozi kupata mambo yanayotokea mitaani au hata kwenye taasisi, mapema kabla habari hazijavalishwa nguo na watendaji wahusika.

Kuzivalisha nguo habari, badala ya kuzifikisha zikiwa uchi au raw kama wanavyosema waswahili wa London, kunasaidia kufichua uhalisia wa habari zenyewe.

Hapa nampongeza sana Maxence Mello na jopo lake la JF maana wanatenda haki kwa umma wa kiTanzania.
Member humu akisema kuna mapungufu mahali, hiyo habari ikaonwa na kiongozi, na hatua stahiki kuchukuliwa, mbona sasa si ndiyo kuisaidia serikali moja kwa moja?

Kwa wenzetu habari ni mhimili wa nne.
 

Usiishie hapo mkuu
 
Wastaafu hustaafu moja kwa moja na kupumzika kwa kazi ngumu walizofanya muda mrefu lakini Pascal Mayalla alistaafu na kutuaga kwa mbwembwe akituachia masikitiko kuwa tutamkosa mwanahabari nguli ingawa tulijua anatafuta uteuzi ambao hawezi kupata akibaki humu JF. Ingawa mteuzi bado anaendelea na teuzi labda ameona uwezekano wa yeye kuteuliwa haupo, licha ya kuunga mkono juhudi muda mrefu, sasa ameamua kurudi kundini. We have heard your thinking aloud and hoping those in power have also heard your thinking and will take the necessary steps to visit JF without jeopardizing members and the Forum but make use of whatever they glean. Welcome back, Pascal njaa bado ipo, we have been missing you and your wisdom.
 
Naunga mkono hoja. Suala lingine ambalo JF ililishikia bango ni Makonda kuongoza kundi la WASIOJULIKANA ambao walikuwa wanateka na kuua. Mkuu amesikia, Makonda kakosa kazi halafu hata mauaji ya wananchi na utekaji vimepungua.

Kingine ni Kigwangalla kutokuwa Waziri. Huyu JF tulikuwa tunapiga left , right and centre kuwa hafai kuwa Waziri.
 

Hakuna watoa rushwa, wezi wa kura na wamwaga damu wanaweza kuwa wawakilishi wazuri, hasa hasa bunge lenyewe linapokuwa kibogoyo. Zaidi ya 50% ya wabunge wa ccm wamepata nafasi za kugombea kwa kutoa rushwa, na hayo tumeyaona kwa macho yetu. 60% ya wabunge wa ccm wametangazwa washindi kwa kura ambazo hazioani na matokeo halisi ya huko vituoni. Wangalau 20% tu ndio wako huko bungeni kwa ridhaa halisi ya wananchi, nao hawana nguvu ya maamuzi. Unapokuwa na bunge lililopatikana kwa njia ya kihalifu, unategemea ubora gani?
 

Unfortunately, wanachota busara humu bila acknoledgement kwa wachangiaji wa JF!!! Mambo mengi serikali inachota humu JF na kuyafanyia kazi!!! Vilaza wengi walioteuliwa na JIWE wanafaidika sana na michango ya JF katika utendaji wao.
 
Tena na hayati Mwalimu akawatandika viboko akina Samwel Sitta na wenzie walokuwa vinara wa mgomo pale UDSM.

Hilo la huyo DC kakosea na anastahiki kushtakiwa mahakamani.
 
Mkuu, mimi pia nakupongeza kwa jitihada zako kubwa katika kuelimisha jamii khasa hii ya hapa JF.

Ila kuna machache ya kuangalia kwa mwaka 2021.

1. Watu kuelewa "concept" au dhana kwamba malengo ya serikali hii na maono au Vision ya kiongozi wake ni yepi.

2. Viongozi wote wa serikali nao pia kuelewa dhana nzima ya malengo ya serikali.

Ukiangalia bado watu wajinga wengi kama hao wanaonunua hizo V8 kwa fedha za kodi za wananchi bila kutumia akili na kufikiri sawasawa kwamba ni fedha hizo zahitajika kupeleka maendeleo huko vijijini.

Ila kwa ujumla twatarajia mawazo na maoni mbalimbali yawe chanya na hasi yote kwa pamoja kupokelewa na hao wasaidizi wa kiongozi wetu na kumuelimisha kwamba kuna masuala ya msingi na ya kupita tu.
 
Hizi ngonjera tuu zakupotezea muda na kupunguzia hasira.
Hakuna kiongozi yeyote kwa sasa anaweza kujifunza kupitia JF, JF wanajifunza wale walio amua kutumia akili zao tuu.
Sasa kwa sasa nani anatumia akili yake aliyojakiwa na Mungu? Hakuna.
Eitha watatumia akili za kuazima toka kwa mteuzi wakati naye anatumia akili za nguvu za Giza.
 
Kaka pascal, rekebisha kidogo- sperm inakutana na ovum sio embryo.
Otherwise naunga mkono hoja.
Nadhani ilikuwa sahihi kusema sperm ikikutana na ovum kinatokea urutubishaji (fertilization) na muunganiko wa sperm na ovum unaunda zygote (a fertilized egg cell).
Tunakumbuka biolojia ya kidato cha nne, huchukua siku 8-14 kwa zygote kuwa implanted kwenye mfumo wa uzazi na kuwa embryo.

Nadhani context ya Kaka Paskali ni kujenga hoja na hoja yake ya voice from within kwa kuunganishwa na mchakato wa mbegu kuungana ina mashiko.

Naomba ku-declaire interest, nimesoma PCB kidato cha 5&6 hivyo huu mchango wa Paskali imenikumbusha vema madesa ya zamani.

Pengine nami nichangie kidogo kwa "akina fulani" wanaosoma kama wakipata nafasi; kuna wakati wanasoma na kuchukua hatua pale wakiona inafaa.
Wanaochangia hoja za kihalifu, hatua mpaka ya kuwakata hufanyika ili kuzuia uhalifu usikotee tena. Aliwahi kukamatwa Wilfred Rwakatare (wakati akiwa Mkurugenzi wa usalama wa CDM) kwa habari iliyotokea humu.

Rai yangu, kama wanasoma, iko haja wakaja na mifumo jumuishi ili mtoto azaliwe. Fertilizatin ku-form zygote ni hatua kubwa sana (wazo); ili embryo ambayo itakuwa implatent kukua na kutengeneza viungo vyote kwa mchakato automated wa mitosis cell division, na mtoto atokee akiwa na afya njema na ubongo wake umejengeka vema ni lazima mama apate quanititative & qualitative feeding kwenye miezi 9 ya mimba na psychological support. Na kuna wengine hali huwa si hali inalazimika kupewa bedrest ili mimba isitoke. Kwa kuwa sio kila mwanamke mwenye mimba anaweza kuwa treated equally, likewise in the course of service, kwa namna JF watu aina ya Paskali wanafikiri kwa sauti, sio kila sauti inatakiwa kusomwa ikaachwa tu, zingine zahitaji special case ku-extract kupata thamani ya wazo lenyewe.

Nimewahi kufika Mafinga na Mufini kuna miti mingi sana ya mbao, nguzo na mirunda. Kumbe miti hiyohiyo ya mikaritus, tungeweza ku-extract kutengeneza essential oil


Forex ngapi tungeingiza?? Inakuwaje Watanzania mashamba yapo na fursa za kuuza mafuta kama hayo ipo duniani then tumekaa. Hatujataka kusikilizana namna gani ya kuja na solution ya pamoja.

Hapa chini ni bei ya mafuta ya majani ya mchai-chai


Kwa ukubwa wa ardhu tuliyonayo, kuna hela za uwekezaji mwaka jana ziibaki TIB zaidi ya 88%; kwanini tuwekeza hata kwenye basics kama hizi ili kupata forex in the courss of creating employments??

Mimi huwa ni muumini wa kujenga mifumo inayoshabihiana. Tanzania tunakwama baadhi ya maeneo simlpy mifumo haiwasiliani, mifumo haina interdependability. Kuna watu kwa kuwa tu wako serikalini na wana hakika ya paycheck basi wamefunga akili zao kudhani they can function in the absense ya mifumo nje ya serikali.

Yesu wa Nazareth alisema, mkulima alipanda mbegu 4, moja ikafa hata bila kuota.
ya pili ikaota isipokuwa ikafa kwa mizizi kushindwa kupenya kwenye mwamba
ya tatu ikaota na baadae ikafa kwa kusongwa na miba
ya nne iliota na kuzaa matunda kwa kuanguka kwenye udongo mzuri. Udongo mzuri simply ulikuwa na rutuba ya kutosha ku-support mahitaji ya mmea kukua na kupata virutubisha na matunda ni outcome ya mmea kuhifadhi akiba yake baada ya kukua.

Tanzania itakuwa na kufika mbali kwa public sector tap na watu wa nje ya mfumo ya public na kujenga collaborative venture za kutengeneza solutions za nchi hii.

Kila la heri wana JF tunapokaribia kuvuka 2020 kuingia 2021. Mungu yuko nasi kwa rehema zake tutavuka.

Wasalaam

F
 
ma popoma utayajua kwa muandiko wao, ebu kapige mswaki ndo uje tajadili
 
ila una mastory mkuu inatakiwa uwe arround nikipiga zangu domple
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…