There is no template for relationship

I beg to differ , YES there is template in relationship, there is formula in relationship ....shida ya kwanza inaanzia hapo, kitendo cha kufikiri na kuamini kwamba hakuna template kwenye mahusiano ni dalili tosha kwamba itakuletea shida kichwani mwako jinsi ya kumudu mahusiano yako. Shida nyingine ni kwamba hata kwa wale/sisi tunaoamini kwamba there is template wengi hawajui jinsi ya kui apply hiyo template, na pia kuwa template hata iwe nzuri kiasi gani ni kitu kimoja, lakini kujua jinsi ya kuitumia na ifanye kazi vizuri ni kitu kingine.

I'll tell you bluntly, the biggest challenge that faces many people today especially young in managing their relationships is LACK OF SKILLS, maana yake ni kwamba wengi wanaingia kwenye mahusiano wakiwa HAWANA MAARIFA YOYOTE, ya jinsi ya kumudu mahusiano hayo, kwa lugha nyingine wanaingia 'bila template' kichwa kichwa huku wakitarajia mahusiano yawe supa... ni kichekesho, na tatizo hili wanalo hasa vijana wa kiume. Vijana wengi wanaingia kwenye mahusiano na wanatamani yawe poa while they are doing nothing, eti kisa? tarari yeye ni mwanaume!. Hili tutaliongelea siku nyingine. Yaani watu wanaingia kwenye mahusiano kama vile wanavyocheza michezo ya kubahatisha ya kamari (Betting) , huku wakitarajia matokeo bora, chukulia mfano rahisi sana... ukicheza kamari mara kumi unadhani una nafasi ngapi za kushida? (Zote, 1, 6, 10?) nikusaidie? Uzoefu unaonesha kwamba uwezekano wa kukosa zote ni mkubwa na kama ni kupata labda nafasi moja. Hii inamaanisha nini katika maisha yetu ya mahusiano? Mahusiano yako ni maisha yako kwanini unayabahatisha maisha yako kama unavyobet kamari?

Leo hii hakuna yeyote (Si raia wa kawaida, si serikali) akayeruhusu upewe ufunguo ili uendeshe gari bila kuthibitisha kwamba una SKILLS za kuendesha gari, uthibitisho wa kuwa na maarifa ya kuendesha gari ni pamoja na kupitia mafunzo ya driving school, kupata cheti na hatimaye leseni, kwa lugha nyingine hii ndiyo template yako ya kukuwezesha kuendesha gari. Sasa iweje leo unaingia kwenye mahusiano bila SKILLS, lazima utakwama, sio uchawi. Ni sawa na upewe ufunguo uendeshe gari wakati wewe hujui kuendesha gari, sote tunajua kitakachotokea.

Ukitaka kujua jinsi ambavyo vijana wengi hawana SKILLS za kumudu mahusiano yao angalia au sikiliza 'tones' ya zimulizi zao za kimahusiano utagundua masuala mawili 1) Watalalamika sana, 2) Watamlaumu mtu fulani, si wao bali ni UKOSEFU WA MAARIFA

NDUGU ZANGU BADALA YA KUPOTEZA MUDA KULALAMA, KULAUMU, KUSAGA MENO....GO OUT THERE AND GET SOME SKILLS SO THAT YOU CAN MANAGE AND ENJOY YOUR RELATIONSHIPS.

Ukikwama nitafute inbox tuyajenge

NDIYO MAHUSIANO YANA TEMPLATE
 
Broh hongera. Your way of thinking pengine inaweza patia wadau maarifa mapya juu ya mahusiano. Usisite kutupa darasa pindi upatapo nafasi.
 
una haki ya kujiita Mchanya........ napenda sana mtu anaewaza positive siku zote!


labda kwa kuongezea, watu wanaingia kwenye mahusiano na too much expectation bila kuweka juhudi zao ili kuyafanya mahusiano yao yawe bora!.....

lkn pia kuna tatizo la kutoridhika, mtu akiona ndoa flani imesimama anajua labda ni kwa sababu wana match or ni soulmate and whatever, wakati uhalisia ni watu wameridhika na hali zao, hivyo wamewekeza nguvu na juhudi katika kukabiliana na changamoto wanazokumbana nazo!......


lastly, hatuna mentors kwenye maeneo mengi ya kimaisha including relationships, na hili ni janga kubwa sana mpaka makanisani (kwetu sisi watu wa church)...... mtu anakua yupo yupo tu inafikia hatua anafanya maamuzi hana mtu wa kumwomba ushauri, very sad!.....


Heaven Sent atamalizia......
 
Nakubaliana na hili bandiko, ila kuna Jambo kama jamii ingebadili mtazamo labda ingesaidia mabinti kupata wenza wao sahihi muda ukifika maana kuna ile social pressure ambayo mabinti wanapitia 25+ kwamba mbona hujaolewa? Mpaka sahivi huna hata mchumba? Inapelekea mdada wa watu aolewe na mtu ambaye hawajajuana vizuri hajui upande wa pili wa mpenzi wake weaknesses, strength etc.... Badae ndio unasikia ndoa chali baada ya muda mfupi
 
Tatizo wasiojua wanaongea sana, na wanao jua wapo kimya tu. Wenye uelewa wako busy, na wasio na uelewa ndio wanatoa darasa. Hii inachnagia kuongeza ugumu kwenye sekta ya mahusiano.

Vingi ambavyo inabidi viwekwe wazi, vinafichwa sana. Alaf vinavyostahili kufichwa ndio vinawekwa bayana.
 
Late marriages are better than forced marriages
 
ni desturi ya wanaojua kukaa kimya, sijui kwanini iko hivi!...... ndio mana nikasema laiti kila kijana angekua na mentor wake jamii hii ingebadilika kwa kiasi kikubwa sana!


ngoja mimi nijitolee kuwa mentor wa Saint Anne ,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…