Mwalufunamba
JF-Expert Member
- Jun 12, 2012
- 211
- 129
Ni jambo lilisilo vutia kwa viongozi na wanachama wa CHADEMA. Ni habari zenye viwango vya kuvunja moyo lakini kwa kujua kunatupa nguvu ya kusonga mbele kwasababu kama Chama inapasa kujipanga upya. CHADEMA wanaamiwa sana na wananchi, mioyo ya watu walio wengi ipo kwa CHADEMA. Ikumbukwe kuwa Stephen Wasira alisema CHADEMA itakufa kabla ya 2015 (alijua nini alichosema), kauli hii iliwafanya CHADEMA wawe makini wakizidi kuchukua tahadhari hatua kwa hatua
mara amebadilisha kauli yake na kusema CHADEMA haitakufa kabla ya 2015 (ni kauli ya kuwapumbaza wanachama na viongozi ili wajisahau).
Matukio ya kiajabu-ajabu dhidi ya CHADEMA
Patakuwa na matukio ya ajabu ajabu ikiwa ni mfulululizo wa zaidi ya yale ya kufunguliwa mashitaka na mabomu kila baada ya miezi mawili au mitatu. Lengo kifanya CHADEMA isiwe stable at ALL the time. Mamluki wa CCM waliopo CHADEMA na wasio mamluki watatumika. Ndiyo maana mwanaJF mmoja alitoa tahadhari juu ya Kurugenzi ya Usalama ya CHADEMA kuhakikisha wanajua nani, muda gani na kwa kusudi gani amefika pale Makao Makuu ya Chama. Tahadhari ile ilikuwa inamaana kubwa sana. Labda kwa nyongeza niseme viongozi wa CHADEMA zitunzeni sana diary zenu na tiketi zenu. Toka katika diary zitachukuliwa taarifa za kukivuruga Chama na tiketi na risiti za hoteli mlizolala zitakuwa msaada katika utetezi wa kesi mtakazobambikiwa kiufundi zaidi. Pia kuna wanawake watatumika kuivuruga CHADEMA, mission to love for destruction/rendering something to powerless (its like from CCM with love)
Mgawanyo wa majimbo na kata.
CCM imetumia wataalamu wa serikali na idara nyeti za serikali kupata na kuzitumia taarifa ili CHADEMA isishinde uchaguzi wa mwaka 2015. Wametumia taarifa za sensa ya 2012, matokeo ya uchaguzi 2014 kwa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu wa 2015 katika kuhakikisha wanaifanya Tume ya Uchaguzi ya Taifa itangaze majimbo mapya na kata mpya ambayo/zo yataongeza idadi ya wabunge na madiwani wa CCM. Utafiti huo umeangalia ni maeneo ya gani based on vituo vya uchaguzi ni wapi CCM walishindwa na CHADEMA walishinda, nini mtazamo wa wanachi kwasasa kisha jimbo husika litagawanywa; upande walioshinda CHADEMA litakuwa jimbo moja na walikoshinda CCM litakuwa jimbo jingine. Tegemeeni majimbo mengi na kata nyingi mpya kutangazwa kabla ya uchaguzi wa 2015. Uwezekano ni mkubwa kwa majimbo ya Dar es salaam, Mwanza na Mbeya kuganywa kwanza.
Katiba mpya na mipango
Serikali tatu na ulazima kutengeneza Katiba ya Tanganyika huenda ikawa kikwazo katika kukamilisha mpango wa hapo juu lakini si kizuizi. Kwa kuanzia CCM watafanya kila liwezekanalo kuihujumu ama kuwa vipengele ambavyo vitawafaidia wao. Ili kulivuruga zoezi la kupata Katiba mpya kuna uwezekano wa CCM kwa kutumia uwingi wao katika Bunge la Katiba kukataa matakwa ya wananchi na kuweka ya CCM, matokeo yake ni wananchi kupiga kura ama ya kuikataa Katiba mpya ama kuikubali ambavyo vyote vitaifaidia CCM. Waliyoyataka ama yapo kwenye Katiba mpya au kurudi kwenye kuitumia ya zamani vyote ni faida kwa CCM.
Uwepo wa mamluki
Ndani ya CHADEMA kwasasa kuna viongozi kadhaa ambao ni mamluki wa CCM ( ukweli ni kuwa ilikuwa waongezeke endapo uchaguzi ungefanyika mwaka huu). Katika viongozi wa Kanda walioteuliwa pia wapo mamluki. Mfano halisi ni Mwaisumbe ambaye ni mratibu wa CHADEMA kanda ya Nyanda za Juu kusini. Mwaisumbe mwaka 2010 aliingia katika kinyanganyiro kura za maoni za CCM Mbeya mjini akashindwa nab ado anamapenzi na CCM. Baadaye akasema amejiunga na CHADEMA (wakati huo kikazi yuko Iringa akiwa ni mwajiriwa wa Kanisa la Baptisti-Iringa). Huyu ndugu anampango wa kugombea Ubunge jimbo la Mbeya mjini kwa tiketi ya CHADEMA; kama atapata nafasi hiyo ya kuwa mgombea tegemeeni nafasi hiyo ataitosa kwa style zaidi ya ile ya Shitambala alivyofanya kwa Jimbo la Mbeya vijijini. Katika kikao kimojawapo cha Kanda, kuliletwa hoja yenye ushahidi kuwa mmoja wa viongozi (ambaye naye imetajwa kuwa ni mamluki) amehusika kuzifuja pesa za Chama, jibu la Mwaisumbe ni kuwa hiyo siyo ajenda ya kikao chetu cha leo. Na haijawahi kujadiliwa tena. Kama haitoshi familia yake wako CCM ambao ni wakazi wa Simike, kata ya Nzovwe, Manispaa ya Mbeya. Kutokana kuifanyia kazi CCM kwa mlango wa nyuma akiwa CHADEMA, dada yake anategemea kupewa ukuu wa mkoa si muda mrefu toka sasa. Dada yake huyo anayeishi Iringa amekuwa akipewa fursa mbalimbali za kushiriki semina na majukumu ili kumuaandaa kwa kazi hizo.
Kununuliwa kwa viongozi
Kama ilivyokuwa kwa Shitambala na namna alivyotumika kuihujumu CHADEMA kwa mlango wa nyuma, ndivyo alivyo Mwambingija (a.k.a. Mzee wa upako) ambaye amekwisha kununuliwa na CCM lakini anaoneka kama vile anaifanyia kazi CHADEMA. Yako mengi yenye ushahidi wa wazi huyu jamaa anavyoitumikia CCM, mfano kabla kusitishwa uchaguzi wa ndani wa CHADEMA, Mwambigija aliwapanga viongozi mamluki (alitengeneza mtandao wa wana-CCM ndani ya CHADEMA). Kitendo cha kuahirishwa uchaguzi basi kimeuchelewasha mpango huo. Pia alikuwa miongoni mwa walioshiriki kikao na Pinda alichofanya na wanaCCM wa Mbeya. Alijipanga kuwa miongoni mwa viongozi wa Kanda, kitendo alichofanikisha kwa kuchaguliwa kuwa mhamasishaji wa CHADEMA. Mwambigija analishwa na CCM kwasasa kwa mlango wa nyuma.
Kuvunjika moyo kwa wanachama/viongozi na kuipigia kura ccm
Kutokana na kuwepo kwa wimbi kubwa la viongozi waliotumainiwa wa CHADEMA kurudi CCM hapo 2014 au 2015, wananchi ambao ni ndiyo nguvu ya CHADEMA watavunjika moyo kwa kiasi kikubwa mno hata kushindwa kupiga kura na wengine kuipigia kura CCM. Tumaini la wananchi kwa CHADEMA ni kubwa mno, kuwavunja moyo kwa style hii kuitaihakikishia CCM ushindi wa kirahisi wa namna zote kihalali na kihujuma.
Umakini wa viongozi wa CHADEMA Makao Makuu na kwingine unahitajika sana. Tahadhari nyingi zimetolewa, zisipuuzwe, na hata hii isipuuzwe.