The SGR War: Magufugame vs Musevenyatta ni Vita Kubwa!. It is a Win Lose War!. When One Wins, the Other Lose, No Win Win Situation!.

Of course yes. But you need to work hard to convince the jurry to enter conviction relying on such kind of Evidence. It has alot of tests to be proved. Not easy at all.
Absolutely true, but the point is, with a good lawyer several heads have been convicted against this "weak" evidence as you have put it!
 
Haya mabandiko marefu tabu sana. Unatafuta pointi mpaka kuipata shatoka jasho tele.

Nimepitsha macho tu mahali nikakuta sehemu inasema "hakuna aliyejua Magufuli kwenda Rwanda, nk...) Mara hii umeme wa maporomoko ya Rusumo huyakumbuki?

Mengine sikusoma, lakini kutokana na kichwa cha habari kuna ninayounga mkono kuhusu 'vita'.

Siyo siri hata kidogo kuwa kuna vita, sio iliyoanza leo. Ni vita ya siku nyingi, na inapiganwa kwa njia mbalimbali.

Rwanda na Uganda ni Jiografia tu ndio inayoamua. Rwanda hadi leo hii anafanya biashara nyingi zaidi na Kenya kuliko Tanzania. Baadhi ya mizigo yake bado anapitisha Mombasa, hii sio kwa sababu anapenda kufanya hivyo, ni kwa sababu ya ubovu uliokuwepo bandarini Dar es Salaam.. Reli ilipong'olewa Kibera, Uganda wakakimbilia Da es Salaam, pamoja na kuwa ni njia ndefu.

Kenya waliofanya Mikutano yao mikubwa mwaka 2015, kama ule wa waJapan TICAD (nadhani inaitwa), walitegemea Magufuli wa wote wa Africa Masharika watakuwepo. Jamaa akamtuma Mama Samia. Wakaanza kulalamika tokea hapo.

Siku zote, inaeleweka, mipango ni kuifanya Nairobi iwe ndio Kitovu (Hub/ Gateway) ya eneo hili. Kiwe kitovu cha biashara, hata zile haramu. "Mabeberu", ndio na mimi ngoja nitumie neno hilo, wako 'bize' sana kuwekeza huko wakilenga kufaidika na ukanda wote huu. Ukiona jamaa wanaporomosha ma-godown na miundo mbinu za 'Logistics', usidhani hawajui wanachofanya.
Ile EPA, si unaikumbuka?..., basi iweke kwenye mipango na anza kuwaza makubwa.

Magufuli, hapana hata Kikwete wote walijihami. Mashirika mengi ya Kimataifa yanaweka ofisi huko, ili waje wafanye kazi hadi huku. Sawa, Mbongo kaweka kodi. Ukija hapa na kufanya kiconsultancy chako siku mbili tatu, lipia kibali na kodi kila unapotaka kuja hapa. Jamaa hawajaacha kulia.

Hivi Paskali, mbona unajifanya msahaulifu hivyo? Hata yule ng'ombe aliyekufa humkumbuki? The Coalision of the Willing. Hiyo ilikuwa ni vita ya wazi iliyolengwa kumtandika Kikwete. Kwa bahati nzuri sana aliipangua na mpango mzima ukasambaratika.

Bandari ya Bagamoyo waliiogopa sana, kwa maana ililenga kuiondoa kabisa Mombasa. Sasa watakuwa wamevuta pumzi.
Ile Barabara ya "kwenda Burundi" tokea Mombasa bila shaka huijui Paskali. Kuna siku waliandika "Wanajenga barabara ya kwenda Burundi.
Habari hiyo ilichapishwa katika kijarida chao cha siku zote 'The East African'. Sasa wanamsherehekea Tshekedi...

Nami ntaandika gazeti kama lako? Hapana...
 
Rwanda secures dry port in Kenya

Duh...!, this is very bad to our SGR, maadam tuliisha sainiana nao mkataba, they have to honor it. Huku kutaka kuunda ka coalition of the willing kangine, it did work well with JK, but it won't work well with JPM, ikibidi, tutawaadabisha, wasituletee mchezo!.

P
 
Wanabodi, Tanzania ni nchi yetu sote, viongozi wetu wana wajibu wa kutusikiliza sisi wananchi wao tunasema nini na kushauri nini, kama ushauri wetu ni mzuri, wauzingatie, kama ni ushauri wa hovyo, wau puuzie.

Ushauri huu ulitolewa miaka 3 iliyopita, ulipuuzwa!. Leo Spika kaenda China, akaonyeshwa na Wachina umuhimu wa bandari ya Bagamoyo, sasa ndio leo, Spika wetu anaongea Bungeni!.

Yaani kuna vitu wakishauri kina yakhe, vina puuziwa, lakini akishauri mchina, ndio Spika anaelewa!.
P
 
Mkuu kavulata , kwanza asante kwa mawazo yako. Sii wengi humu wanajua how SGR can operate profitably!. Ili SGR iweze kuleta faida ni lazima iwe na kitu kinachoitwa linkages. Mfano hiki kipande cha Dar Moro ambacho kiko tayari, kiteendeshwa kwa hasara muda wote hadi SGR itakapo link na Rwanda, Burundi, Uganda na DRC.

Karibu mitaa hii

Pia kasome
P
 
Sad
 
Kiukweli kabisa, huyu mtu aliyeifanya kazi hii, akitokea kuja kuchaguliwa kuwa Mwakilishi wa Tanzania ndani ya EALA, you can just imagine atafanya nini!. Kama amaweza kufanya yote haya akiwa just a journalist, akitokea akawa mbumbe wa kitu kama EALA, si Tanzania itapaa?. Au mnasemaje wanabodi?.
P
 
Hili jina sasa limebadilikablimekuwa SAMIGAME VS MUSERUTO
P
 
Kwenye mambo ya SGR, Watanzania tunapaswa kuambiwa tuu ukweli wa kila kitu!, serikali yetu lazima iwe very transparent see through kwenye kila kitu including mikataba na financial maters kufuatia kuwahi kupigwa huko nyuma kwenye rada, kwenye ndege, kwenye meli na sasa kwenye reli
Maswali haya yajibiwe kikamilifu
Maswali haya yanahitaji majibu ya kina na sio blah blah!.
Kama mtu kuuliza maswali kama haya, kutapelekea kuhojiwa uzalendo wake, mimi naomba kutumia kinga ya kihabari na kanuni ya kwanza ya mwandishi wa habari no seek the truth, and write nothing but the truth!, kuna kitu ninadhamiria sio tuu kuandika bali kukitengenezea a video documentary ya safari ya SGR ya Tanzania, tulipotoka, tulipo na tunapokwenda, ili huko mbele, likija kujitokeza liji white elephant fulani hivi ambalo sijui kama ni mimi tuu naliona, angalau dhamira yangu isinisute, niliona kabla, nikasema kabla, nikaandaa documentary kabla, nikaonyesha kabla, ili angalau jamii ya Watanzania wajue kuna watu waliona kabla na walisema kabla!.

Na labda kuwasaidia Watanzania wenzangu wasio jua, kwenye ile kashfa ya rada, BAE walikiri kutoa mlungula wa kickbacks, lakini sheria yao inawaruhusu non disclosure ya waliowapa mlungula, ilo usipoteze wateja wapya wapenda mlungula, kibiashara mlungula wa 10% ni halali!, ila ikijulikana kuwa umetoa mlungula, unapaswa ama uwataje uliowapa mlungungula, wakamuliwe wautapike huo mlingula, ama uwahifadhi usiwataje, na badala yake utozwe faini kwa uliowapa mlungula, na kuurejesha ule mlungula, na hicho ndicho kilichofanywa na BAE, kuwahifadhi waliowapa mlungula, na badala yake ikakubali kulipa faini na ndipo tukarejeshewa ile chenji ya rada.

Hii maana yake, kuna viongozi wetu walikula mlungula BAE akawakingia kifua kuwahifadhi kwa kulipia faini na ule mlungula ukarudishwa nchini kama chenji ya rada, endapo BAE wasinge wakingia kifua kuwahifadhi na kuwalinda, amini usiamini, hayo majina ya waliopokea mlungula na kuzihifadhi fedha zao kule Credit Suisse, yangetoka, Watanzania msinge amini macho na masikio yenu!.

Kashfa hii iliobuka kwasababu tuu kulitokea lijinga limoja, mgao wake yeye ukauhifadhi visiwa fulani ambavyo viko chini ya milki ya Uingereza, ndipo Muingereza akabaini, lakini kama wote wange bank Swiss banks, kule fedha zao ni very secure, hata bank manager, hajui majina ya customers na clients ni secret codes tuu zinatembea, hivyo wala kashfa ya rada isinge ibuka!.

Hivyo watu tunaoulizia kuhusu haya mabenewa, naomba mtuelewe ni wazalendo wa kweli wa nchi hii!.

Paskali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…