The haunted house :(Nyumba chafu yenye mazingara)

The haunted house :(Nyumba chafu yenye mazingara)

tilmikha

JF-Expert Member
Joined
Feb 27, 2013
Posts
497
Reaction score
608
Wengi wetu tumekuwa tukilalamika kuwa nyumba zetu zimekua hazikaliki, vyumba pia vimekua havilaliki licha kua na farniture pamoja na mapambo mengi ya luxury au hata visivyo na luxury lakini usingizi umekua wa tabu mno.

Kwa mujibu wa Wikipedia haunted house ni nyumba ama jengo linalo aminika kuwa linakaliwa na roho za wafu (mizimu) waliopata kuishi ndani ya nyumba ama jengo husika. Binafsi siamni uwepo wa mizimu bali naamini uwepo wa majini ambao ndio chanzo kikuu cha haya mazingara yanayozikumba nyingi katika nyumba za watu.

Sayansi imeeleza kua matokeo ya haunted house ni zao la misinterpretation ya sauti za zilizopo ndani ya hizo nyumba ama ni kutokana na sumu ya kimaumbile ipatikanayo ndani ya hayo majumba ama majengo ambayo huwa yanaaminika kuwa haunted ambazo husababisha hallucinations kwa wakaazi wa hizo nyumba.

Mwaka wa 2005, uchunguzi wa Gallup ulionesha kuwa asilimia 37 ya wamarekani, asilimia 28 ya wakanada, na asilimia 40 ya wabrons walionesha imani kuwa nyumba zinaweza kuwa haunted. (Lyons, Linda 1 November 2015). Pia inasemekana katika kila wamarekani 4 watatu wanaamini huwepo wa mazingara (Gallup poll, retrieved 14 Feb 2010).

Mpendwa msomaji, hata wewe unaweza kudadisi watu wawili watatu juu ya suala hili la mauza uza ya nyumba basi utaona namna ya uso wa msimuliaji utakavyo sawijika na kujaa huzuni ukikumbuka madhila na mateso uyapatoyo katika nyumba alioijenga ama anayoilipia kodi kwa gharama kubwa kuliko maelezo. Wewe mchana kutwa unahangaika halafu usiku wasikia boda boda zikifukuzana juu ya paa la nyumba yako kweli patalalika? Ni mara ngapi umekua ukiomba alfajir ifike ili tu upone kutokana na mateso ya usiku kucha usioyajua chanzo chake?

Huyu ni baba ambae alikua akiishi na familia yake na kujaaliwa kupata watoto 3 wa kike, alielezewa na hii familia yake kuwa nyumba haikaliki ila alibisha mpaka siku moja alipoamka na kuwakuta watoto hawa wamenyolewa vipara na nywele kutokuonekana. Hivi hujasikia kutoka katika vyombo vya habari vya Zanzibar vikiripoti juu ya matukio ya nyumba kuungua moto ndani ya chumba kimoja tu hicho hicho.?!

Ni mpaka lini utakua mtumiaji wa antidepressants ndio upate usingizi? Jawabu utakua nayo wewe ila moja ya sababu inayoifanya nyumba kuwa haunted ni kutokukaliwa na watu kwa kipindi cha miezi mitatu hapo huwa makaazi ya majini, pili nyumba ambayo asili yake ilikua ina ugomvi halafu mmoja watu waliodhulumiwa huamua kuuitia majini hio nyumba ili isikalike.

Kwa upande wa nyumba kuungua moto, ukiacha sababu maarufu zinazojulikana za chanzo cha ajali za moto basi sababu nyengine ni uwepo wa aina ya majini waitwayo majusi ambao huwa wanaabudu moto.

Mnamo mwaka 2007 nilipatwa kuitwa moja katika nyumba ya wapangaji ambayo walikua wakilalamika kuwa nyumba imekua haikaliki, watoto wamekua hawalali na pia wamekua wakishuhudia mtu mzee akiwa anaranda randa ndani ya hio nyumba. Waliniambia waliwahi hata kuwakodi wavuta bangi ili waje wavutie nyumbani hapo ili hali itulie lakini hilo halikuwasaidia.

Sitaki kurefusha maelezo naamini na wewe utatusimulia mauza mauza uliowahi kuyapata. Ikiwa kweli hili tatizo lipo na wengi kama litakuwa limewagusa basi nitawafahamisha namna ya kufanya ili kuweza kuepukana na madhila haya na kama itakua halipo hili tatizo basi itakua Nice to know.
Enjoy your reading [emoji433]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kifupi tu wakati nipo kidato cha pili nilipanga getto mimi na mshikaji wangu, moja ya masharti ya ile nyumba ilikuwa usitwange usiku na usirudi zaidi ya saa tano na nusu usiku na ikatokea imefika saa sita ya usiku hujarudi basi usirudi kabisa...mambo ya vijana hapo ndio kama tuna week tu tangu tupange tukarudi saa saba, hatukugonga mlango tukaruka ukuta. Kwa kuwa chumba chetu kilikuwa uwani tukaona isiwe tabu, sasa wakati tushazama ndani, pale katikati ya ule uwa,kulikuwa na karo ambapo maraia wanaoshea vyombo vyao, pale palikuwa kakaa kiumbe mmoja mweupe kama karatasi na nguo zake zikiwa vivyo vivyo pia alikuwa na macho makubwa yanayong'aa kama paka, sura yake ndio iliyotukimbiza usiku ule, alikuwa na sura ndefu sana, pale alipokaa alikuwa akiangalia mlango wa kuingilia bafuni sasa alipohisi kuna watu ndo akageuka kutuangalia, nakumbuka tuliruka ukuta hatukurudi tena ktk nyumba ile, usiku huo tulikesha stand na vitu vyetu alienda kutuhamishia mwalimu wetu ambaye ndio alikuwa kama mzazi wetu mkoa ule
 
Dah pole sana wakati mwengine kwenye matatizo waweza kuwa zaidi ya Jet li, ila mkuu mlikua majasiri kweli nadhani mimi ningedondoka hapo hapo.

Aiseee .... ni kweli hii mkuu !?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dah pole sana wakati mwengine kwenye matatizo waweza kuwa zaidi ya Jet li, ila mkuu mlikua majasiri kweli nadhani mimi ningedondoka hapo hapo.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu ujasiri tuliupata baada ya kupewa masharti ya ile nyumba tukajua tu hapa ipo siku tutakutana na kizaa zaa maana si kwa masharti hayo mawili usitwange usiku na usirudi zaidi ya saa tano na nusu
 
Hizo nyumba za mauza uza mkuu nimezipitia karibu nusu ya maisha yangu, hata nyumba niishiyo sasa ilikuwa na mambo meusi meusi. Na mpaka sasa ni mimi ndio nimekaa hapo mwaka wa tatu sasa, wengi wanaishia miezi minne akikomaa sita kahama.
 
Hahaha ila hilo la usitwange usiku ndio limeniwacha hoi, ila mliwahi kuhoji sababu za masharti?
Mkuu ujasiri tuliupata baada ya kupewa masharti ya ile nyumba tukajua tu hapa ipo siku tutakutana na kizaa zaa maana si kwa masharti hayo mawili usitwange usiku na usirudi zaidi ya saa tano na nusu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Baadhi ya mambo niliyowahi kukutana nayo ktk nyumba za kupanga
Kuona vivuli vya watu, wanataka kumchukua mtoto wakati huo mwanangu ana miezi miwili tuu, nilifanikiwa kukarir maumbile yao na siku hiyo nilisikia hata mmoja akimwita mwenzie shangazi na asubuhi wa msaada wa mwenye nyumba niliwajua

Niliwahi kuamka nikakuta friji imetolewa chumbani imepelekwa sebleni

Kuna siku nilibanwa mbavu nikawa nashindwa hata kupumua ( hii ilikuwa kijijini mkoa wa morogoro) nilipofanikiwa kupambana na kuamka chandarua chote kilikuwa kama kimelowekwa kwenye damu kinavuja damu na mimi ile sehemu nilipokuwa nimebanwa kuna matundu kama ya kucha yamonitoboa..

Kuna kijiji kinaitwa mbigiri hukohuko morogoro nilienda kukusanya kuku huko, kwa bahati mbaya, ikatokea nikakosa ikanibidi nilale, doh usiku ulikuwa mwaka hiyo siku nilikula makofi,!nilitwa miguu, nilifinywa, niliwashwa, chumba kilikuwa jehamu ndogo, unakuja mwanga mkali kisha linakuja giza kisha unakula bonge la kofi, ile siku mlango sikuuona wa kukimbilia nimechezeshwa mpaka kunapambazuka na ilipofika saa kumi na mbili nikauona mlango niliondoka sikuaga mtu na pesa nilizowalipa hao wakunitafutia kuku nikasamehe, sijawahi rudi tena huko.

Tukio lingine la kushangaza ni huko uruguruni halihusiani na nyumba bali tulienda milimani na pikipiki, mwenyeji akasema huku mnakuja na pikipiki haya ila huku tunapanda hii (yale mabua ya mahindi) jamaa kakalia bua lake huyoo....
Ila yote na yote siamini katika hayo mambo na siyaogopi hata kidogo kwa sasa hasa mwanga maana ntamzibua na anaweza kufia ktk mikono yangu akiingia ktk 18
 
Kifupi tu wakati nipo kidato cha pili nilipanga getto mimi na mshikaji wangu, moja ya masharti ya ile nyumba ilikuwa usitwange usiku na usirudi zaidi ya saa tano na nusu usiku na ikatokea imefika saa sita ya usiku hujarudi basi usirudi kabisa...mambo ya vijana hapo ndio kama tuna week tu tangu tupange tukarudi saa saba, hatukugonga mlango tukaruka ukuta. Kwa kuwa chumba chetu kilikuwa uwani tukaona isiwe tabu, sasa wakati tushazama ndani, pale katikati ya ule uwa,kulikuwa na karo ambapo maraia wanaoshea vyombo vyao, pale palikuwa kakaa kiumbe mmoja mweupe kama karatasi na nguo zake zikiwa vivyo vivyo pia alikuwa na macho makubwa yanayong'aa kama paka, sura yake ndio iliyotukimbiza usiku ule, alikuwa na sura ndefu sana, pale alipokaa alikuwa akiangalia mlango wa kuingilia bafuni sasa alipohisi kuna watu ndo akageuka kutuangalia, nakumbuka tuliruka ukuta hatukurudi tena ktk nyumba ile, usiku huo tulikesha stand na vitu vyetu alienda kutuhamishia mwalimu wetu ambaye ndio alikuwa kama mzazi wetu mkoa ule
Kwa hio mlishindwa hata kumpa shkamoo?
Kweli nyie watoto wa siku hizi hamna adabu.

Maendeleo hayana chama
 
Naam ni kweli mkuu ilikuwa Iringa
Nakumbuka mnamo miaka mi4 iliyopita niliwahi kusafiri mkoani ki -biashara basi nikawa nimefikia katika nyumba ya rafiki yangu ambayo ilikuwa na wapangaji tupu "

Pia wenye nyumba waliamua kuacha chumba kimoja kwaajili ya mgeni " so awali hii mgeni wa wenye nyumba aliyekuwa ametembelea nyumba hiyo nilikuwa ni mimi ...
Basi bwana baada ya kulala siku kama 3 hivi " ..ilipotimu usiku wa siku hiyo ya 3 nikashtuka usingizini mlango wa chumba nilicholala ukiwa unagongwa kwa nguvu sana " Nikawa washa taa nakuuliza mgongaji ninani akajitaja jina kuwa ni moja ya wapangaji wa ile nyumba " nikaufungua mlango " .... nilipo ufungua nikakutana na sura za wapangaji wa nyumba nzima zikinitazama kwa hofu kuu ...

Nikawa nimekaa na wasikiliza sasa walichoniitia " wakaniuliza wewe bwana humu ndani umehifadhi kitu gani " nikauliza mimi !? Wakajibu ndio " nikawajibu zaidi ya begi langu la nguo na accessories za electronic kama simu na PC hakuna kingine ... wakaniambia mbona Tunasikia harufu kali sana inatoka huku chumbani kwako mpaka tume shindwa kulala " (Aisee nilipigwa na butwaa ) harufu !!! Ina wezekana kana vipi NYinyi muisikie halafu mimi nisiisikie " na wao wakashangaa ina maana hauisikii hebu acha masihara nikawajibu siisikii ndio "

Basi nikaona isiwe tabu " ikanibidi niwaruhusu watu kadhaa waingie ndani wapekue ili wajiridhishe kama kuna hicho wanacho dai kuwa kina nuka " ... jamaa walipo ingia wacha watafute lakini hawakukuta kitu " Sote kwa pamoja Tukazidi kupigwa na Butwaa " wakati huo mimi bado nilikuwa sisikii harufu yeyote ile " ila nikawa na wasi wasi What if ikikutwa maiti ya mtu humu ambayo iliwekwa. Na watu wakati mimi nikiwa sipo kwa lengo la kunikomoa " Aisee nilihisi kuelemewa na dunia yote

Basi baada ya jamaa kusearch na kukuta hakuna kitu " wakatoka nje " ghafla watu wote. wakaanza kudai kuwa ile harufu imetoweka " Mhhh mimi nikawa najionea mauza uza tu .... baada ya pale hakuna mtu Aliyelala story ikawa ni hiyo tu usiku kucha kwamba nyumba ile inamauza uza .... usiku ule ule nikatafuta namba ya boda boda nikapiga jamaa akanifuata nikabeba vilivyo vyangu nikawaambia wale wapangaji wa search begi langu tena .. kisha baada ya hilo zoezi kufanyika ..nikaondoka zangu kwenda kulala guest .

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom