2 milimita?how durable is that thing?
Sent using
Jamii Forums mobile app
Durability is subjective implying that several factors come in play. Handling, weather, power stability, etc.
Kwa tz bado tuna changamoto nyingi za kutufanya hivi vitu viwe less durable.
Mathalan tv za hapa kwenye picha zote ni samsung. Ya kwanza morden ya pili classic. Kwa nyumba yenye familia yenye watoto watundu watundu na umeme wa tanesco usiotabirika hiyo classic ni bora kuliko hiyo modern.
Hivi modern ni show off kwa huku bongo mana huwa mazingira sio rafiki ya kuvifanya vidumu.
Ila pia pesa ya kununua genuine modern nyembamba brand kama samaung au lg below 10mm nchi 37 kwenda juu ni kubwa sana. Kuna nchi 40 inayouzwa 2.3m kule jumia. Ni UHD. Sijui ni vijana wangapi wanaopenda modern wanaweza kujitosa kubeba kitu kama hiyo kwenye nyumba ya kupanga yenye mke na watoto wawili watundu. Ukiitaka QLED kuanzia nchi 37 samsung au lg ndo ujipange zaidi.
So just a matter of choice. Ni kama magari tu. Unaweza nunua lenye mvuto ila linakunywa mafuta kama ng'ombe wa maziwa anavyokunywa maji.
Kwenye tv muonekano kila unavyozidi kuwa na mvuto ndio handling inabidi kuwa angalifu zaidi. Vioo vyake vikiminywa vinatengeneza mistari. Sasa sijui tutaanza kuletewa tv screen protector kama zile za simu? Hii itakuwa kama kurudi kwenye plasma.
Courtesy of
miamiatz