VERBOSE
JF-Expert Member
- Sep 12, 2022
- 8,145
- 12,746
Story ya movie ya The Dutchman (2025) kuna namna fulani km imenigusa. Jinsi ilivyoanzia mpaka ilivyoishia.
Kuacha maelezo mengi km umeiangalia hii movie kuna kitu inasimulia kwa wale watu wanaopenda kulala lala na wapenzi tofauti tofauti wanapewa funzo.
Huyo manzi unaemuona hapo juu ameigiza humo km Lula (demon) ambae alienda kumtongoza huyo mwamba hapo anaitwa Clay Williams, then wakaenda kufanya yao Clay Williams akamkaza vizuri tu huyo demon lady 'Lula'.
Kilichonishtua ni pale Clay Williams alipomaliza kufanya mapenzi na huyo demon 'Lula' akaenda kujiangalia kwenye kioo na kuanza kujilaumu kwamba amefanya nini hiki? Hili ni jambo ambalo linawakuta wanaume wengi wakishamaliza kufanya ndio akili zinarudi.
Ghafla 'Lula' akawa km amekuja kwa nyuma ya Clay wakati huo Clay anajitazama kwenye kioo, sasa producer anatuonyesha kwamba yule 'Lula' (demon) ni Kibibi fulani hivi Kikongwe kilichojichokea balaa. Nikasema inamaana jamaa kafanya mapenzi na kile Kikongwe na kila akikiangalia anamuona ni Manzi fulani mzuri hatari, akageuka hapa producer anatuonyesha 'Lula' mzuri sio Kikongwe.
Paliponishtua ni hapo kwenye Kioo yule 'Lula' anaonekana ni Kikongwe balaa ila Clay alipogeuka nyuma anamuona Manzi fulani mkali hatari. Oya nimeshtuka sana.
View: https://www.youtube.com/watch?v=KDfXbmazRG8
Itafute na wewe ujithibitishie.
Ni nzuri ukiangalia huku unakunywa bia taratibu utajifunza kitu.