The chickens have come home to roost | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

The chickens have come home to roost

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mapango, Jan 9, 2011.

 1. mapango

  mapango Member

  #1
  Jan 9, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 88
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Mwaka 2001 baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2000, chama cha CUF kilifanya maandamano ya kupinga matokeo ya uchaguzi mkuu kule Zanzibar, kwa bahati mbaya jeshi la polisi kupitia amri za wakuu wao BWM/OAL na OM wakafanya mauaji ya watu wasiopongua 23 (kwa taarifa za serikali) na 60 (kwa taarifa zisizo rasmi). Wakati ule viongozi wa vyama vyengine vya upinzani hawakuona umuhimu wa kuungana na wenzao wa Zanzibar kulaani mauaji yale kwa vitendo, pengine ingesaidia kuipa funzo serikali ya CCM kuwa damu wa Mtanzania yeyote ile kwetu ni thamani. Kosa hili ndio lililoipa serikali ya CCM uzoefu na ujasiri wa kuwauwa watanzania, na ndio leo tunaona yaliyotokea Arusha. Ubaguzi ni adui mkubwa katika kudai haki, wengine walikaa kimya kwa sababu wahanga wa mauaji yale ni wazanzibari, wengine wakasema ni waislam, lakini CCM wao walichokuwa wanalinda ni utawala wao, sasa inapokuja hata kwa mtanganyika au mkristo kama anahatarisha utawala wao lazima watamshughulikia kwa mtindo huo huo, ilimradi madaraka yabaki kwao. Funzo hili lazima tulichukue na tuwe wamoja katika kudai haki za watanzania na kupinga udhalimu kwa watanzania bila ya kuaangalia ni nani ameonewa/amedhulumiwa. Na hii sera sio ya JK tofuati na wengi wanavyodhani, ni sera ya CCM, kwani wakati ule wa mauaji ya Zanzibar, JK hakuwa rais wa Tanzania. Hata mtoto wa mkulima akiwa rais kutoka CCM atafanya hivyo hivyo!,
  "CCM ni maradhi ambayo, yeyote akiugua anakuwa fisadi na muuwaji".

  Poleni wafiwa wetu, na wale lojeruhiwa
  Kwa kudai haki yetu, wamekufa maridhawa
  hatutasahau katu, kwa haya tunofanyiwa
  kwa damu ya watu wetu, uhuru tutapatiwa
   
Loading...