Hii kesi ya kizushi sana, wanasema pia kuwa alikuwa high on crack cocaine wakati anatekeleza hayo mauaji, sasa sijui alipata wapi hizo nguvu. Baadhi ya victims walionyesha struggling wakati wanakuwa attacked, ila Jamaa hakuwa na alama zozote kuashiria hali yoyote ya kuparuana na mtu.
Bado katika maelezo yake alivyopiga simu emergency, alitoa taarifa kwamba mmoja alikuwa bado mzima ambapo alienda kufia hospitali baadae, sasa kama hakutaka kubakiza ushahidi kwanini hakummalizia na huyo pia?
Jurors wenyewe kuna wengine walikiri kuwa 'confused', ukiangalia documentary utaelewa vizuri. Na walihoji baadae kwanini hawakupewa nafasi ya kuchagua hukumu, wala kutaarifiwa kwamba adhabu ya kifo haikuwa kati ya options.
Hii issue imejaa mizengwe sana.