Kuna watu hapa michezo kama hii hawajawahi kuiona na kama wamesikia basi si kwa kufikiria kama ni michezo ya jasiri wa hali yajuu hadi mtu kufa shujaa. Wachezaji wa mpira Tanzania hawajitumi pamoja na kuwa na vipaji, hii ni kutokana na athari za kuzoeleka michezo ya ridhaa nchini. Nchi tajiri wachezaji ni matajiri kufikikia kiwango cha wao pia kuwa na hisa katika timu kubwa ni kutokana ni kucheza kwa kufa na kupona hapo ndo $$$ mchezaji atakuwa amenasa.
Si michezo tu, ila pia katika shughuli na kazi za kawaida watanzania hatujitumi. Waliobahatika kutembembelea mataifa makubwa na kuishi na k ufanya kazi nao wanapata picha kamili ya uwajibikaji na wameendelea kutokana na hayo. Sio ni walalamikaji wa kutaka kupandishiwa mishahara ambayo haiwiani na uwajkibikaji. Hayo ndiyo yaliyosababisha mashirika ya uma kusambaratika.
Kwa hili la watz kuwa wavivu sikubaliani nalo. Na hilo la mashirika ya umma kufa kwa sababu ya watz kuwa wavivu pia sikubaliani nalo.
Ninachojua ni viongozi wetu kutufuata sheria na uwajibikaji. Mtu anaboronga hapa anamishiwa sehemu nyingine akaboronge.