DuaZaMama
JF-Expert Member
- Jun 2, 2025
- 1,882
- 4,129
Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) imewataka waandishi wa habari mkoani Tabora kufuata miiko na kanuni za uandishi wa habari kwa kuzingatia usawa, kuepuka matumizi mabaya ya lugha ili kudumisha mshikamano na amani hususani kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29,2025.
Wito huo umetolewa na Mkurugenzi Msaidizi Elimu kwa Umma na Mawasiliano kutoka THBUB, Zawadi Msalla wakati wa mafunzo kwa waandishi wa habari mkoani humo juu ya namna bora ya kutoa taarifa zao.
"Waandishi wa habari tumieni kalamu zenu vizuri ili kuijenga Tanzania yenye mshikamano ili kuweza hata kufanya Tanzania iwe kati ya nchi zinazohesabika kama kisiwa cha amani", amesema Zawadi.
Bi. Zawadi ameongezea kuwa waandishi wa habari wanayo nguvu kubwa kuijenga nchi yenye mshikamano na amani kupitia taarifa wanazotoa hivyo hawana budi kuzingatia misingi na weledi katika kazi zao.
Kwa upande wao, baadhi ya waandishi wa habari akiwemo Lubango Mleka na Maiko George, wamesema mafunzo hayo yamewaimarisha katika namna bora ya kuripoti kwa weledi na kwa kuzingatia misingi ya uandishi wa habari hususani kuelekea uchaguzi mkuu.
Chanzo: Jambo Tv