Thamani ya maneno POLE na SAMAHANI katika Mahusiano

Kuomba msamaha ni kusema "YAISHE" zaidi ya hapo usitegemee "SAMAHANI"...!
yaishe inamaana bado unali moyoni au hujakubali kosa unajaribu tu kulizima lisilete ugonvi hapo hujatatua tatizo unamuacha mwenzio na maswali mengi.la sivyo na yeye akikwambia yaishe bila kukuomba msamaha inabidi ukubali
 
Kuomba msamaha ni kusema "YAISHE" zaidi ya hapo usitegemee "SAMAHANI"...!

heh, haya makubwa kweli.
Na yaishe hiyo utakuta baada ya wiki au mwezi ameyarudia yale yale alosema yaishe.
Cc Asprin
 
Last edited by a moderator:
kwa mwanaume timamu akigundua kosa lake huomba msamaha. Na hiyo ni akili ndogo sn yenye matokeo makubwa sn.
 
Wanaume tuna namna ya kuomba msamaha lakini sio kutamka bayana "naomba unisamehe". Hilo halipo. Hayo ya kutamka namna hiyo ni kwa akina mama. Kama ndio mfumo dume sina uhakika lakini ndivyo ilivyo! Namna ya kuomba msamaha inaweza kuwa more caring, kufanya vitu ambavyo unajua dhahiri mwanamke anafurahia etc.

Aisee we jamaa una akili sana!

Ngoja niwape scenario fulani:

Hv Rais akikosea anaomba msamaha? Unaijua msemo wa kiswahili kua '..mkubwa hakosei..'?

Damn it! Don't force 'sorry' out of your man! It isn't proper!
Ikitokea amekosea, ukagundua hilo ukamweleza akawa mpole elewa that the dude is sorry. Be patient,he will show it kwenye matendo yake from that moment on!

Sasa jidai kukomaa aombe msamaha uone! While you are at it, you are likely to over step your boundary and the dude will stop being humble and quite! Ndipo kichapo kinapoibukaga, ama kufokewa!

Get it, the dude makes a mistake that hurts you, approach him gently and humbly and speak sense into him respectfully then leave him alone.

Usipofuata ushauri wangu, siku moja utakuja kutoa ushuhuda jinsi ulivyoipata hiyo ngeu hapo usoni

N:B Siungi mkono 'domestic violence' but women stop sparking things around the house!
 
you are definately violent... why not say sorry wewe kwa kigezo cha uanaume...chaii ..namuonea huruma mpenzi wako
 
you are definately violent... why not say sorry wewe kwa kigezo cha uanaume...chaii ..namuonea huruma mpenzi wako

aisee nakuonea huruma unavyomuonea huruma mpenzi wangu anae-injoi kila mara utamsikia '..honey,you are the best. You make me the happiest woman in the world. In your absence, whenever I remember you its a mixture of feelings, I smile contentedly and become horny at the same time...'

She doesn't sound to me as e person who deserves your huruma
 
hahahahahaha...we ni kichaa kidogo kwa kweli... eti smile contentedly...
 
Hii samahani inafariji Sana Japo nshakutana na mdada hata iweje haombi msamaha anachofanya ni arguments tu.Mapenzi yakuwa magumu Sana.Ila ukikutana na mapenzi wanatumia vyema Maneno"pole,asante na samahani"mahusiano yao hudumu Sana.
 
Mwanaume kumuomba msamaha mwanamke ni kujishusha na ni udhaifu wa hali ya juu kabisa....ni heri nipigwe risasi ya kichwa nife kuliko kumtamkia neno SAMAHANI mwanamke......
 
Na huongeza mapenzi kweli kweli, mie kuomba samahani naona inaniongezea maksi kwenye mapenzi, maana mwenzangu atajua kuwa nina mapenzi ya dhati ndio maana naomba samahani. Wenye michepuko ndio hawaombi samahani maana wanajua kuna mbadala wa huduma
 
kuna ukweli sana katika hilo.
 
Poleni wadau wa MMU,

Ukweli neno samahani ni dogo sana ila ni gumu sana kulitamka kwa mwenzio kwa kuhisi labda atakuzarau au kujihisi heshima yako itapungua,neno hili huwa ni gumu sana kulitamka kwa watu wazima hususani baba, mama au mtu yeyote alie kuzidi umri sijui kwanini huwa gumu na wakati anamakosa kweli.

Narudi kwa upande wa wapenzi,huku nako pia ni ligumu kulitumia neno hili hususani sisi wanaume,ila sio wote hata wenzetu nao pia huwa wagumu kuomba msamaha kama kakosa tena kama kashakuchoka ndo utajuta kabisa kumfamu.

Mfano mzuri ni rafiki yangu na mpenzi wake wamechuniana kisa tu msichana kashindwa kumuomba mshikaji msamaha,kosa lenyewe liko hivi jamaa kampigia msichana simu mida ya saa saba hivi, kumjulia hali lakini simu ilikuwa inaita pasipo kupokewa.

Akajaribu mara kibao lakini holla,ikabidi jamaa amsikilizie kwa sababu atakuta missed call lakini msichana kawa kimya,akampigia tena saa kumi nayo kimya,ikabidi jamaa akae kimya maybe ipo chaji cha ajabu mpaka siku inaisha msichana hakumpigia simu mshikaji.

Kesho yake jamaa akampigia simu saa nne asubuhi ikapokelewa ikabidi amuulize vizuri tu,cha ajabu tena eti msichana anamjibu simpo tu mshikaji ,eti hakuwa na vocha,jamaa akamwambia basi si ungenitumia hata tafazali nipigie, msichana kawaka amkamjibu hivi,nimekwambia sikuwa na vocha.

Hunielewi jamaaa akashangaa sana iweje msichana awe ndiyo mkali wa kumkaripia mchizi ili hali.yeye ndo mwenye makosa ikabidi jamaa amulize mbona unanijibu hivo,msichana akamwambia ulitaka nikujibu vipi.

Mchizi hoi akawa mpole akamwambia basi siku ukiwa na vocha nitafute,msichana akasema sitakuwa nazo mpaka mwakani.

Sasa wadau hapo nani mwenye makosa,maana mpaka sasa hivi watu hawaongei kila mtu anajua yeye yuko sahihi.Je jamaa aendelee kuwa kimya au amtafute na akimtafuta aanzeje kuomba msamaha.

Karibuni.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom