TFF yatoa maamuzi sakata la Ramadhani Singano 'Messi' na timu yake Simba

brave one

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
4,876
7,366
Leo hii ndio siku ambayo sakata la Ramadhan Singano a.k.a Messi lilikua linasikilizwa kwenye ofisi za TFF ambapo pande mbili zilikutana chini ya TFF.

Baada ya kikao kirefu muafaka uliofikiwa chini ya TFF ni kwamba kuvunjwa kwa mikataba yote miwili ambayo inatofautiana. So, kikao kimeamua kwamba mkataba wa alionao Messi uvunjwe na mkataba walionao Simba uvunjwe waingie makubaliano mapya. Upande wa Singano haujakubaliana na maamuzi hayo kwasababu unamtaka yeye akubaliane na Simba tena.

Lakini kwa mujibu wake ni kwamba anatakiwa kuwa huru kama mkataba umevunjwa na sio kukubaliana upya na Simba. Singano anataka kuwa mchezaji huru ndio aamue mwenyewe kama kuongea na Simba au club nyingine.

Chanzo: Shaffih dauda
 
Maana ya kuvunja mkataba ni kwamba mtu upo huru kufanya maamuzi yeyote kwa utashi wako binafsi. Sasa hao TFF kwann wamlazimishe huyo singano afanye maamuzi wakati mkataba wameshavunja?

Binafsi simshauri singano aendelee na simba. Yatakuja makubwa mbeleni ambayo hataweza kuyaepuka kwasababu ameingia chini ya mkataba na haohao simba.
 
fununu zulizopo tff mkataba wa miaka 3 wa simba ndio wenye makosa , tff wameamua kutumia busara zaidi ili kutoweka wazi nani mwenye makosa
 
Wampe kilicho chake aende anakotaka na akikubali kusaini upya iwe hiari yake yeye sio alazimishwe.
 
Yaani hawa tff, sasa huo ndio uamuzi gani??!! na inaoneka Messi ameshinda kwenye hili, sasa ili kuwasaidia simba ina bidi walete magumashi mengine, yaani ni shida tu kumbe kina hans walikuw wana mtisha dogo tu, kumbe wao ndio magumashi!!! kweli soka la bongo sina hamu nalo. Na siku zote mwisho wa ubaya ni aibu.
 
Hapo ndo mtu unaona upuuzi wa shirikisho letu na mpira kwa ujumla TZ...Hivi utasemaje wavunje mikataba wote?? Hapo lazima mmoja yuko makosani na mwingine yuko sahihi...haiwezekani kuwa suluhu...no no no...TFF wawe wakweli la sivyo wataharibu soka letu...mwenye makosa achukuliwe hatua...kusema wote wavunje mikataba ni kutaka kusema kuwa wote wana makosa kitu ambacho si sahihi au kuwa wote wako sahihi kitu ambacho si kweli...yani Soka Bongo TFF mnaboa sana jaman
 
makosa yapo kwq simba ila tff imeilinda timu ya simba

fununu zulizopo tff mkataba wa miaka 3 wa simba ndio wenye makosa , tff wameamua kutumia busara zaidi ili kutoweka wazi nani mwenye makosa

Tatizo la uongozi huu unalindana sana na pia akina kabourou wamemzidi maarifa Jamal Malinzi na sitashangaa nkiskia kikao hicho kiliinjiniwa na simba. Warudi katika kanuni aliearibu ndo apewe adhabu ili iwe fundisho na je sputanza walikwepo?
 
Last edited by a moderator:
Kwa nn simba wanamng'ang'ania? Si wamuache akatafute maisha club ingine!
 
nawapongeza tff kuamua ukweli mtoto yatima kanasuriwa kwa
mujahidina
nasikia kuna baadhi nao kama singano mikataba yao inaisha mwakani lakini inaonyesha 2018 ndio simba hiyo
 
ingekuwa simba ndo imeshinda kesi, singano angechukuliwa hatua ila kwa kuwa singano ndio kashinda ndipo yakatolewa maamuzi hayo...
 
fununu zulizopo tff mkataba wa miaka 3 wa simba ndio wenye makosa , tff wameamua kutumia busara zaidi ili kutoweka wazi nani mwenye makosa

Hapa hakuna kutumia busara hata kidogo. Yaani wameficha jinai halafu tunawasifu wametumia busara? Hili suala ilibidi liende kwenye vyombo vya sheria ili kutoa onyo wa wapuuzi wengine wasijaribu kufanya forgery. Simba wameforge mkataba na kuongeza mwaka mwingine mmoja. Huu ni uhuni na ni jinai.

Tiba
 
Huu ujanja unafika mwisho kama wa Blatter. Zoezi lianzie kwa Blatter hadi kwa wahaini wanaojita viongozi wa club
 
Back
Top Bottom