TFF Yatangaza usajili kuanza rasmi juni 15

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,410
Waswahili wanasema, "Mwenye kisu kikali, ndiye mla nyama". Na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), limetoa kalenda ya msimu mpya wa mashindano na matukio ambako baada ya mapumziko ya wachazeji yanayoishia Juni 10, 2016.

Kalenda inaonesha kipindi kinachofuata sasa ni usajili unaotarajiwa kuanza Juni 15, 2016. Usajili huo unaanza na uhamisho wa wachezaji ambako utaanza Juni 15, 2016 hadi Julai 30, 2016.

Kwa mujibu wa Kalenda hiyo, timu ambazo hazishiriki Ligi Kuu ya Vodacom msimu wa 2016/2017 zitaanza kutangaza wachezaji walioachwa kuanzia Juni 15, 2016 hadi Juni 30, mwaka huu.

Kwa upande wa timu zitakazoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), watatumia kipindi cha Juni 15, 2016 hadi Juni 30, 2016 kutangaza usitishwaji mkataba wa wachezaji. Usajili wa utaanza Juni 15 hadi Agosti 6, kwa timu zinazoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.

Pingamizi itakuwa ni Agosti 7 hadi 14, 2016 kabla ya kuthibitisha usajili kwa hatua ya kwanza kati ya Agosti 15 na Agosti 19, 2016 wakati usajili hatua ya pili utaanza Agosti 17, 2016 hadi Septemba 7, 2016 na kitafuatiwa kipindi cha kipindi cha pingamzi hatua ya pili kuanzia Septemba 8 hadi Septemba 14, 2016.

Septemba 15 hadi Septemba 17, 2016 itakuwa ni kipindi cha kuthibitisha usajili hatua ya pili,

Ratiba hiyo inasema kwamba timu zinatakiwa kuandaliwa kuanzi Juni 15 2016 hadi Julai 15, 2016 ambako kuanzia Julai 16, 2016 hadi Agosti 14 ni kipindi cha mechi za kirafiki za ndani na nje. Ratiba ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara itatoka kati ya Julai 16 hadi Agosti 14.

 
Back
Top Bottom