1.Hii ni TFF pekee iliyotukumbusha kuwa bado
kuna viini vya ukabila nchi hii ambapo viongozi wakuu wa chombo hiki pamoja na asilimia kubwa ya wadau wengine ni wahaya.
Sitaki kuamini kuwa hii ni bahati mbaya na kimsingi ni kinyume cha misingi ya utawala bora hata kama wateuliwa wana vigezo
2. Hii ndio TFF pekee inayofanya maamuzi kwa kupiga ramli na ubashiri au kura wakati kanuni ziko wazi! Kesi za kuamuliwa kwa siku moja kama kanuni inazingatiwa, inaweza kuchukua majuma au miezi ilimradi ipindishwe au kuangalia upepo unavumaje. Rejea kesi za Geita na Polisi Tabora, Simba vs Kagera, Simba vs Azam kuhusu mkataba wa Singano,n.k. Kielelezo cha ubabaishaji TFF leo inaweza kuamua hivi, kesho ikaamua tofauti ktk jambo hilohilo! So huwezi kujua kosa ni lipi na haki ni ipi
3. Hii ndio TFF ambayo vyombo vyote vinaweza kukaa kwa pamoja kuamua jambo moja! Huelewi hasa ni chombo gani linachofanya maamuzi. Ktk sakata la Simba na pointi 3 za Kagera kikao cha rufaa kimehusisha Bodi ya Ligi, Kamati ya Masaa 72, Sekretarieti na Kamati ya nidhamu! Ajabu kabisa
4. Hii ndio TFF ambayo viongozi wake hasa Malinzi ameamua kufungia kila mtu anayempinga. TFF haina uvumilivu kwa wakosoaji wake. Iko tayari kutumia kinachoitwa kanuni pale tu zinapoainisha hukumu kwa wanaokosoa tu. Angetile alitumbuliwa siku moja baada ya Malinzi kuingia madarakani, Ndumbaro kafungiwa miaka 7, Muro, Manara na naamini wengi watafuata kama kuna atayempinga Malinzi. Hebu jiulize kwani watu zamani kipindi cha Ndolanga na Tenga walikuwa hawakosei? Kwa nini ni kipindi hiki tu ndio kila ukosoaji unaambatana na kufungiwa?
4. Ndio TFF iliyokumbwa na tuhuma kubwa kabisa za rushwa na upangaji matokeo ambapo viongozi wakuu wamehusishwa moja kwa moja na rushwa kiasi cha kuchunguzwa na TAKUKURU na baadhi kupandishwa mahakamani hata kama mtu anaweza kushinda kesi lkn wahenga walisema panapofuka moshi......
5. Ndio TFF ambayo kamati zake ni mbovu kiasi kuwa kamati inaweza kuendesha kikao bila kujali akidi au kushirikisha wajumbe ambao hawaruhusiwi! Hii ni kwa mujibu wa Katibu Mkuu Mwesiga alipoelezea 'uhuni' uliofanywa na Kamati ya Masaa 72 iliyoamua kuipa pointi 3 Simba kama ni kweli.Hii si habari nzuri kwa utawala wa soka.
Kwa sababu hizi na nyingine nyingi Malinzi asipewe kura kutawala muhula ujao, aliyofanya kwa miaka 4 inatosha na kubwa atakumbukwa kwa kufanya vizuri kuiandaa Serengeti Boys lakini hana cha kujivunia katika utawala na usimamizi wa soka. Wajumbe bila kujali itikadi za Usimba na Uyanga, au maslahi binafsi hasa wale wajumbe walioandaliwa kumpigia kura chondechonde utendeeni haki mpira wa nchi hii. Piga chini!!!