TFF wajitathimini na Ratiba ya Yanga ilivyokuwa ngumu mbele yao

Ujinga mtupu

JF-Expert Member
Aug 16, 2017
851
1,887
Yanga wametua mchana huu kutoka Tunisia kupitia Dubai na wanatarajia kwenda Mwanza leo saa moja usiku tayari kwa mchezo wa Jumapili dhidi ya Kagera Sugar.

Wachezaji wote wamerudi isipokuwa Aziz Ki ambaye hadi kocha Nabi anamalizia msafara wao hakuonekana na kuibua shangwe za mashabiki wakihoji mchezaji huyo yupo wapi?

Aziz Ki amefungiwa mechi tatu na faini laki tano kwa kosa kutosalimiana na wachezaji wenzake kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Simba uliomalizika kwa sare ya bao 1-1.

TFF tunaomba mmliangalie hili suala la wachezaji kutopumzika na wanarudi mnawaunganishia mechi zingine, wakati mwaka jana kuna timu ilikuwa na viporo hadi saba vilifika.

Lengo yawezekana ni kuidhoofisha Yanga na kushindwa kuendelea na 'unbeaten' zake.
 
Yanga
1668183277591.jpg
 
Kwani Azizi Ki alifungiwa peke yake ofsa?

Imagine mtu kama chama pengo lake pale Simba na bado husikii makolo wakiilaumu TFF
 
Acha tu watu wacheze tujue Kati ya Simba na yanga nani ana timu Bora

Maana simba naye ataanza kulalamika tukipewa vipolo.

Wacha kipigwe mwanza hatujawai kukosa point pale

Nataka kipigwe now Ili tujikite kileleni kabisa tukianza safari mwezi wa 2 mwakani ikifika mwezi 3 tushatangaza ubingwa wa ndani!!
 
Kwani Azizi Ki alifungiwa peke yake ofsa?

Imagine mtu kama chama pengo lake pale Simba na bado husikii makolo wakiilaumu TFF
Yaani Makolo wailalamikie TFF?
Hii hii TFF ya Karia??
Hauko serious wewe...
 
Yanga wamecheza jumatano kwa hiyo kuchelewa kwao kurudi hakuwahusu TFF. Kuunga unga ndege na kuchelewa kurudi sio kosa la TFF, mlitakiwa baada ya mechi muanze kurudi na ndege yenu .
Yanga wamecheza Jumatano usiku ndio, wakalala, Alhamis mchana wakaanza safari ya kurudi wakafika Dubai wakalala, asubuhi wakabadili ndege
 
Yanga wamecheza jumatano kwa hiyo kuchelewa kwao kurudi hakuwahusu TFF. Kuunga unga ndege na kuchelewa kurudi sio kosa la TFF, mlitakiwa baada ya mechi muanze kurudi na ndege yenu .
man duga, Yanga wamecheza Jumatano usiku, wakalala, Aalhamisi mchana wakaonza safari kurudi wakafika hadi Dubai wakalala ili kesho yake waunganishe ndege na kufika Dar mchana.

Hawakupumzika, usiku wameunga kwenda Mwanza. Ruti yao iliwalazimu kufika hivyo, wewe umesema wamechelewa, ulitaka wapae na ungo ? TFF ilipaswa kuwafikiria, ili wacheze japo Jumatano ijayo.
 
Sasa mna wasiwsi gani nyie si anibiteni?.sifa ya anibiteni ni iwe mvua iwe jua boli linatembea
 
man duga, Yanga wamecheza Jumatano usiku, wakalala, Aalhamisi mchana wakaonza safari kurudi wakafika hadi Dubai wakalala ili kesho yake waunganishe ndege na kufika Dar mchana. Hawakupumzika, usiku wameunga kwenda Mwanza. Ruti yao iliwalazimu kufika hivyo, wewe umesema wamechelewa, ulitaka wapae na ungo ? TFF ilipaswa kuwafikiria, ili wacheze japo Jumatano ijayo.
Kwa muda wa Tunisia mechi imeanza jioni saa 12 ikaisha saa 2 usiku. Wangeanza safari saa tatu usiku kwa ndege binafsi wangefika bongo alhamisi saa tatu asubuhi. TFF hana kosa hawezi kufuata ratiba ya timu inavyopenda yenyewe.
 
Back
Top Bottom