TFF - Simba ni Bingwa wa Msimu wa 2017/18

AKILI TATU

JF-Expert Member
Feb 10, 2016
2,658
2,804
MKURUGENZI wa Ufundi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Salum Madadi, amesema kwa mwenendo wa usajili wa Simba ulivyo, hakuna shaka timu hiyo ndiyo itakayochukua ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu ujao wa 2017/18.

Madadi ameyasema hayo jana Ijumaa kwenye mkutano wa waandishi wa habari ulioandaliwa na Kampuni ya Michezo ya Kubahatisha ya SportPesa jijini Dar es Salaam kuzungumzia ujio wa Klabu ya Everton ya England Julai 12, mwaka huu.

Akizungumza mbele ya waandishi wa habari waliyohudhuria ndani ya semina hiyo, Madadi alisema jinsi Simba inavyoendelea na usajili wake ina nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa wa ligi msimu ujao.

“Simba itakuwa bingwa kwani inafanya usajili mzuri na kwa jinsi wanavyoenda ni wazi watakuwa na kikosi bora cha ushindani kwa msimu ujao wa ligi na mechi za kimataifa.

“Mabingwa wa msimu ujao Simba wanaweza kupata fursa ya kucheza na Everton pia mabingwa wetu watetezi Yanga, hii tunaomba kama itawezekana wacheze na Everton kabla ya Ligi ya England kuanza,” alisema Madadi.

Katika hali ya utani, Tarimba alijibu kijembe hicho cha Madadi kwa kusema; “Kwenye suala hili la ubingwa wa Simba msimu ujao, hebu tusubiri mwisho wa msimu tuone ila kwa kuwa amesema mkurugenzi wa ufundi haya.”
 
Najua Salum Madadi amesema hiyo Kiutani tu kwakuwa Yeye ni mwana Simba SC mwenzetu ila kama tunavyowajua Waandishi wetu wa Habari ' upeo ' huwa ni wa pale pale tu nao bila hata ya kulichambua wamelileta Kwetu walaji hivyo hivyo na sisi tumelipokea Kimihemko.

Labda niseme tu kama mwana Simba SC ' niliyetukuka ' kabisa kwamba nafurahi kwa ' usajili ' huu unaofanywa sasa na Kamati yangu ya Usajili inayoongozwa na Kapteni wa zamani wa JWTZ Zackaria Hanspoppe a.k.a Mr. Cowboy kwani wanaosajiliwa ni ' Majembe ' ya ukweli.

Kiufundi

Wanasimba wenzangu hasa wale mnaoujua mpira vizuri na pia ni Wadau wa mpira wazuri katika mpira kuna mambo mawili kuwa na Kikosi imara lakini pia kama hao Wachezaji wataweza kuwa na ' Chemistry ' nzuri ambayo itaweza kuisaidia Timu. Tatizo ambalo naanza kuliona na naomba nitoe tu angalizo mapema ni kwamba siku zote usajili kabambe huwa siyo sululuhisho la ushindi kwa Timu.

Tatizo sugu la Simba SC yetu

  1. Kocha huwa hapewi uhuru wake mwenyewe
  2. Kocha huwa kuna muda anapangiwa Kikosi hasa katika mechi za Yanga FC na Azam FC kitu ambacho ni hatari
  3. Motisha kwa Wachezaji huwa si nzuri ila inaimarishwa tu wakati wa Derby yetu na Yanga FC
  4. Tunaamini sana ' Ndumba / Uchawi ' kuliko Ufundi
  5. Kila Kiongozi wa Simba SC na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Simba SC ni Kocha ' msaidizi '.
  6. Tumefuga ' Wasaliti ' wengi sana ambao siku zote ndiyo hutuangamiza na mwishoni kufanya vibaya
  7. Wachezaji kutojengwa Kiumoja ambapo huwa kuna Makundi kitu ambacho hakina afya katika Timu

Angalizo

Wanasimba SC wenzangu nawasihi kabisa tuache kuanza ' kuwananga ' Watani zetu Yanga FC na kujiona kuwa kwa usajili huu ' Kabambe ' unaofanyika basi tayari sisi ni Mabingwa wa VPL, ASFC, MAPINDUZI na CONFEDERATION ila tunachotakiwa kukifanya ni Kukiombea tu kwa Mungu Kikosi chetu kiweze kuelewana haraka na kifanye vizuri.

Yanga FC ambayo kwa sasa wanaonekana kama ni ' Wakiwa ' kama wakituliza akili zao, wakakubali hali yao waliyonayo sasa, Wachezaji wao nao wakajitambua na kutanguliza kucheza kwa ' Jihad ' huku wakiwa na hiki hiki Kikosi chao ambacho kimekaa muda mrefu na kina maelewano hata baada ya kuondoka kwa Niyonzima na nasikia na Ngoma nae bado Yanga FC inaweza kufanya vizuri na mwishoni Simba SC tukajikuta tunakimbilia tena FIFA ' kimaneno ' kama Viongozi wetu walivyotufanyia na kutufunga midomo wana Simba SC wote kwa huu usajili.

Hata tusajili Wachezaji wa aina gani ila Mimi GENTAMYCINE bado nitaendelea ' kuwaheshimu ' Yanga FC ila hata na Wana Yanga FC nao wajue kuwa siku zote kutesa huwa ni kwa zamu na kama na Wao wasipokuwa na umoja na mshikamano huku wakijitafakari nini cha kufanya nisiwafiche na nisiwe ' Mnafiki ' kwa hawa Wachezaji waliosajiliwa kuna hatari siku ya mechi ya Simba na Yanga basi wana Yanga FC wote wakapatwa na aibu ya ' Karne ' kwa kufungwa magoli mengi na ya aibu.

Yangu ni hayo tu.
 
umenena makuu kiongozi,tatizo la simba sc ni hilo tu,kila kiongozi ni kocha ,na hapa ndipo natamani mo dewji akabidhiwe hii timu mapema ili kusudi hizo sijui kamati za ufundi,sijui makinikia gani huko yafikie mwisho tuiache timu iongozwe kisayansi
 
Back
Top Bottom