TFF na muda wa mechi za kimataifa.

Jacobus

JF-Expert Member
Mar 29, 2011
4,687
1,701
Naona inakuwa mazowea kwa mechi za mashindano za kimataifa zinazoihusu timu yetu ya taifa kupangwa kuchezwa hapa saa tisa alasiri, najiuliza ni kigezo gani wanakitumia hawa TFF kwani kama kuwakomoa wageni kwa hali ya hewa hata wachezaji wetu wanaumia. Ninamaana kuwa ligi yetu michezo yote huanza saa kumi jioni na wachezaji wetu wa nje ndio kabisa kwani huko mechi zao huchezwa mpaka usiku. Nawaomba TFF wautumie uwanja huu mpya kwa kuwaonea huruma wachezaji na watazamaji wetu kwani pesa haina mwisho.
 
Back
Top Bottom