TFF na juhudi zake za kudidimiza kandanda nchini. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

TFF na juhudi zake za kudidimiza kandanda nchini.

Discussion in 'Sports' started by Jacobus, Oct 1, 2012.

 1. Jacobus

  Jacobus JF-Expert Member

  #1
  Oct 1, 2012
  Joined: Mar 29, 2011
  Messages: 3,580
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  "UDIKTETA" kumbe haupo kwenye SIASA pekee na naamini huanzia NYUMBANI kwanza.
  Hivi soka letu kama nchi litafufuka kweli ikiwa watawala pale TFF wanaona mawazo yao tu ndo sahihi? Udhamini wa timu ni tofauti kabisa na udhamini wa klabu. Mdhamini wa LIGI hudhamini mashindano kwa nia ya kutangaza biashara yake kupitia hayo mashindano na mdhamini wa klabu hufanya hivo hivo kupitia klabu kwa kipindi watakacho kubaliana na mdhamini wa klabu ndio huwa na mzigo mkubwa zaidi kwani gharama za kuendesha klabu huwa zake.
  Sasa usanii huu wa watawala wa TFF kutaka vilabu eti visipate mdhamini mwenye BIASHARA sawasawa na mdhamini wa ligi ya TFF mie haiingii akilini kabisa kama sio pana maslahi binafsi hapa ni nini?
  Pana kampuni za simu nyingi tuu ambazo zingependa kudhamini vilabu visivokuwa na uwezo wa kujiendesha lakini TFF ni kikwazo, pale England Backlays bank inadhamini ligi ya nchi hiyo (BPL) lakini haijaizuia Liverpool kuwa na mdhamini wake Starndard Chartered bank!!!!!!!!!!!!
  Tungekuwa hatuoni TV ligi za wenzetu wenye akili za kuendeleza soka hatungekuwa na cha kusema kuhusu utendaji mbovu wa TFF. Angalia mashindano ya kombe la Taifa yamefia wapi?
  Hivi hatuwezi kuwa na tabia ya mashabiki wa Yanga na Simba pale timu zao zifunganapo kutimua viongozi bila kujali timu hizo kwenye mashindano ya kimataifa zinafanya nini???????
  TAFAKARI NDUGU.
   
 2. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #2
  Oct 1, 2012
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,932
  Likes Received: 2,084
  Trophy Points: 280
  Nadhani ni tatizo la "bei" tu. Mkataba wa udhamini, kimsingi ni mkataba wa kuuza haki (ya kutangaza). Sidhani kama itakuwa rahisi kwa Vodacom kukubali kuachia hicho kipengele cha "haki ya upekee" huku wao wakiendelea kutoa dau lilelile (udhamini uleule)!

  Tunaambiwa vilabu vilishirikishwa, inakuwaje hicho kipengele kinakuwa kama ni kigeni kwao baada ya mkataba kusainiwa? Utaratibu wa kushugulikia disputes kwenye mkataba huo zipoje? Na tatatibu za kuvunja zipoje? Kuna kampuni nyingine ipo tayari kutoa dau kama hilo la Vodacom bila kuwapo kwa hicho kipengele cha upekee?

  Btw, kwani wakati ligi inadhaminiwa na TBL (Safari Lager) masharti yalikuwaje? Hicho kipengee cha upekee hakikuwepo?
   
 3. Jacobus

  Jacobus JF-Expert Member

  #3
  Oct 3, 2012
  Joined: Mar 29, 2011
  Messages: 3,580
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Sawa lakini huyu mdudu aitwae "HAKI YA UPEKEE" katoka mbinguni? Kama sio maslahi binafsi kwa watawala wa TFF (na nadhani ndo walikiweka).
  Pana mfano mdogo kwenye radio zetu, utakuwa unasikiliza kipindi fulani na ndani ya kipindi hicho hicho utasikia tangazo la Voda, Airtel, Zantel, Tigo na hata TTCL, humo hakuna "HAKI YA UPEKEE"?
   
Loading...