TFF na Jeuri ya kuivimbia serikali

TFF na Jeuri ya kuivimbia serikali

Suluhisho langu ni kwamba wziri muhusika awaandikie baruaa fifa awaambie kwamba tff kama chombo kilicho ndani ya sjmt basi inatakiwa kufuata katiba ya nchi kama vyama vingine vyovyote ingawa pia inatakiwa kufuata kanuni za shirikisho.

Kwakuwa tff ilikiuka katiba na kufanya marekebisho ya katiba bila kufuata utaratibu basi tff uongozi uliopo madarakani umekosea na kwa mujibu wa sheria za nchi viongozi hawa wanashtakiwa kwenye mahakama zetu za kiraia. Na hii iwe funzo kwa viongozi wengine watakaofuata.

Kwa mantikihiyo bas serikali kama serikali inatoa agio la uchaguzi kufanywa kwa kutumia katiba ya zamani, na hapa hata kama nyie ndo wafadhili lkn ikumbukwe kwamba annual contribution ambayo tff wanalipa inatokana na kodi za wananchi hivyo lazima serikali iingilie kati. Na fifa wambiwe wazi hamuwez mkatengeneza nchi nyingine ndani ya taifa huru kupitia michezo mnayoiratibu.

umesema kweli kabsa lazima wafuate katiba ya nchi hawako sayar nyingine ambako wanaweza kujitungia sheria ambazo zinapingana na sheria za nchi

hawa nao ni kati ya ya mafisadi katika nchi hii! kwani inashangaza sana hawajawahi kutoa ripoti ya mapato na matumiz toka wameingia, na wanakusanya viingilio vya watu ambao wanatozwa vat na vilabu vinalalmika mpaka kufikia timu zingine kutaka kususia uwanja mpya maana makato ni makubwa mpaka kufikia serikali kuingilia ila wenyewe walikaa kimya kama hamna tatizo vile.

halaf sielew kabisa wanaowasifia kwamba wamekuza mpira wakat toka wameingia kwenye uongoz, tanzania kwenye rank za fifa imekua ikishuka tu saiz ni ya 127 hata majiran zetu wakenya,waganda wametupita

pia toka wameingia hatujaweza kuqualify hata mara moja kwenda mataifa ya afrika angalia wakenya,ethiopia,sudan zote zimeenda mataifa ya afrika

na hiyo hiyo programu yao ya tsa haijafanikiwa kuzalisha kijana hata moja tunayeweza kumtegemea katika timu ya taifa au akaenda kucheza nje ya nchi,wote unaowaona wanatamba ni raw football players hawajapikwa na programu ile atleast kipingu alitoa wachezaji katika kizaz cha akina kaseja
 
Mi swali najiuliza kwa tenga na tff yake hawajibu hoja za serikali kuwa mabadiliko ya katiba hayakufuata taratibu na badala yake wanakimbilia kusema tutafungiwa na FIFA, wangekuwa ni viongozi wenye malengo mazuri na mpira wa tz basi wangeitisha kikao na kubadilisha katiba kama serikali inavyotaka, ila kwa kuwa ni wezi watupu wanaogopa uchaguzi kwani malengo yao ya kurithishana uongozi wa TFF yatakwama

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Jamani nauliza tu kutaka kujua, hivi FIFA ni chombo kilicho juu kabisa kiasi kwamba hata UN haiwezi kuwaingilia? Let's say tumefungiwa, ina maana hakuna sehemu yeyoye kama nchi tunaweza kukata rufaa na kufunguliwa?
 
Haiwezekan niondoke nyumban nikamuachia mtot wng maagizo apike chakula then nirud nimkute hakupika..... Nikaamua kumsema baada ya muda et aendekushtak kwa baloz wa nyumba kumi then anategemea nitamuogopa balozi???? Haya ndio maigizo ya TFF, SERIKAL NA FIFA
 
Sakata la malumbano yanayoendelea baina ya serikali na TFF KUHUSU KATIBA yanazidi kuchukua nafasi siku hadi siku....sielewe TFF inataka nini? na inatoa wapi huu musuli wa kuichezea serikali hii? TFF leo wanakuja na mkwala wa kufungiwa Tanzania eti serikali inaingilia maswala ya mpira wa miguu Tanzania...

Huyu Angetile ni nani katika nchi hii? huyu Tenga ule ustaarabu wake aliokuwa nao na hata akakubalika na wapenda soka leo umeishia wapi mbona naye anakuwa mswahili na mbabaishaji, Kwa kaweli inatia mashaka na serikali lazima ijitutumue kuepuka kuitwa serikali DHAIFU

Inakuaje TFF kama TFF inailazimisha serikali... kwa maana kwamba inampangia Waziri muda wa kuongea na nani wa kuongea naye.. Huu ni udhalilishaji mkubwa sana kwa serikali na mtu yoyote anayemdharau Waziri ni Punguani... na kumdharau Waziri ni kuidharau serikali nzima kwa ujumla wake na ni dhahiri unamdharau yule aliyewateua mawaziri ambaye ni Mheshimiwa Dr. Jakaya Mrisho Kikwete Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.. mpaka sasa wadau hawajaona kosa lolote la serikali katika sakata hili... lakini tunashangaa na kichwa ngumu cha Angetile na Tenga... kwa dharau hii wanaoionyesha ni aibu kwa serikali nzima ............lsio bure lazima wanaagenda ya siri

 
Back
Top Bottom