TFF na Azam Group Wataua soka letu kabisa

NGARUKA

JF-Expert Member
May 5, 2014
404
225
Jamani kama umefuatilia tuzo za VPL jana,kuna kitu kilicho nishangaza hasa tuzo ya Mchezaji bora wa ligi et ni Tchetche wa Azam. kulingana na watu aliopambanishwa nao akina Matogolo ni halali yake lakini TFF na Azam hawakuona nominee wengine bora.

Mfano la Liga umchukue Neyma,umpambanishe na Morata na Villa si kura atapewa Neyma. Katka tuzo hakuna BALANCING ingawa mimi Shabiki wa Yanga lakini yule mfungaji bora angestahili kabisa kuwa Mchezaji bora wa VPL.

Ngoja niwaambie Yanga na Simba ziliua mwili wa soka la Tanzania lakini Makampuni ya Azam na timu yao kwa kutumia pesa zao Wataua MWILI NA ROHO YA SOKA la Tanzania. na kwa mtindo huu soka letu liwe la HAPAHAPA TU.

Kwa hali hii ni heri kukaa kuangalia Arsenal anacheza na QPR kuliko kwenda uwanja wa taifa. Huko wawapeleke wafanyakazi wa Azam group. Ukiangalia namna Supersport inavyokuza soka la A.kusini licha ya kuwa na timu ligi kuU utaona Madudu ya Azam Group.
 
mwangalingimungu

JF-Expert Member
Jul 29, 2013
1,285
2,000
Takwimu zinaonyesha mada hii imeshasomwa na watu zaidi ya 140, lakini hakuna aliyeitolea maoni. Ndio kusema hakuna maoni mwafaka na au dhidi ya mtoa mada? Hapana. Ni kwa sababu wengi wanawafikiana naye lakini wanahisi muhali kuikosoa timu wanayodhani ni bora nchini kwa sasa. Unafiki wa aina hii ndio Waingereza huufananisha na tembo aliyeingia kwenye chumba kilichojaa watu, na kila mtu akajikausha eti hajamwona: Elephant in the room!
 
Matola

JF-Expert Member
Oct 18, 2010
40,697

sasa wewe ni kipi ulichochangia hapa? pambafu.
 
MPUNGA

JF-Expert Member
Nov 10, 2010
838
500
Hivi kuna PFA ya BONGO, Kama ipo wao walimchagua nani? Au wachezaji wetu bado ni wachezaji wa ridhaa?

Waandishi wa habari kupitia chama chao nao kwa nini wasiwe wanachagua mchezaji bora sambamba na ligi inapoisha?
 
MKALIKENYA

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
1,196
1,170
Naungana mkono hoja AZAM wanataka ku dominate hata vitu vinavyotakiwa kuwekewa ushindani, Simba na Yanga msimu unaofata unganeni mdai haki yenu ya matangazo Yanga walijaribu mwaka huu lakini wakaangushwa na RAGE uongozi mpya wa Simba na Yanga nitawaona wana akili timamu watakapokuwa na kwanza kupambana ongezeko la pesa kutoka AZAM TV, eeh hata takwimu zinaonesha mechi zinazohusisha timu hizo ndio zinaangaliwa na watu wengi iweje wapawe mgawo sawa na Ruvu Shooting au Mgambo huu ni uwonevu kabisa nasikitika kuona haya yanatokea katika zama hizi za uelewa wa watu upo juu sana.
 
cnjona

JF-Expert Member
Mar 24, 2014
1,021
1,250
Miezi kadhaa iliyopita watu mlisema AZAM italeta mapinduzi ya soka letu, sasa naona taratiiiibu akili zinaanza kukaa sawa, na mwisho tutaelewa MANJI alimaanisha nini.
 
NGARUKA

JF-Expert Member
May 5, 2014
404
225
We mwanga......... acha unafiki,mi nakujua unaendesha kale kabaiskeli ka Azam hivyo una benefit na Azam directly.
Huu uzi waachie wapenda soka halali wa Tanzania na litimu lenu linalotumia M150 kwa ubingwa wa M70.
Hapa Waingereza Wana-conclude kwa kusema
ZERO Brain
 
Mphamvu

JF-Expert Member
Jan 28, 2011
10,711
2,000
TCheche ni mchezaji bora ndio, hata umlinganishe na nani. Unless unaangalia ubora katika vyombo vya habari badala ya kutazama mechi.
 
sabasita

JF-Expert Member
Oct 29, 2009
1,505
1,225
TCheche ni mchezaji bora ndio, hata umlinganishe na nani. Unless unaangalia ubora katika vyombo vya habari badala ya kutazama mechi.
mi mshabiki wa simba lakini kipretcheche sio wa kucheza bongo, he is a complete player
 
Mphamvu

JF-Expert Member
Jan 28, 2011
10,711
2,000
mi mshabiki wa simba lakini kipretcheche sio wa kucheza bongo, he is a complete player

Kuna watu hata sijui huwa wanafikirije mpira, hawajui kuwa magazeti hutengeneza stori za Simba na Yanga kwa malengo ya kibiashara. Nao wanaingia mkenge na sifa za humo, huyo bwana sio tu bora, lakini amedumu na ubora wake kwa misimu kadhaa ambayo amecheza Ligi Kuu. Sema kwa kuwa haandikwi na haya magazeti yetu wala kuripotiwa na maredio watu wanamchukulia poa...
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom