RUCCI
JF-Expert Member
- Oct 6, 2011
- 1,701
- 1,714
Klabu za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara zimetakiwa kuanzia msimu ujao ziwe na ofisi, Uwanja wa mazoezi, kuendeleza programu za vijana ikiwa ni pamoja na kuwapa haki ya kusoma.
Hayo yamefikiwa katika kikao cha Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Jumapili (Juni 05, 2016) cha kupitia taarifa mbalimbali za ligi na kukubaliana namna ya kuboresha mashindano mbalimbali ikiwamo Ligi Kuu, Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC), Ligi Daraja la Kwanza ya Startimes, Ligi Daraja la Pili na Ligi ya Mabingwa wa Mkoa kilichofanyika mjini Dar es Salaam.
“Kadhalika kamati iliangalia uendeshaji wa Ligi za vijana wenye umri wa chini ya miaka 20 na Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania (TWPL) ambayo wiki iliyopita ilipata udhamini wa haki za kuonyeshwa kwenye televisheni kutoka kituo cha televisheni cha Azam,” imesema taarifa ya TFF.