TFF mmetia Taifa Aibu kwa Uchaguzi Tata wa Wachezaji eFootball

TFF mmetia Taifa Aibu kwa Uchaguzi Tata wa Wachezaji eFootball

Damaso

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2018
Posts
6,132
Reaction score
10,514
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limejikuta katikati ya lawama nzito baada ya kashfa ya uchaguzi wa wachezaji wa kuwakilisha taifa katika mashindano ya eFootball World Cup 25.

1758264760672.jpg


Yaani badala ya kuchagua mabingwa wa kweli wanaopatikana mitaani—wale wanaojulikana kwa uwezo wa ajabu kwenye PlayStation na hutembea na game pad zao—uongozi umeamua kubeba watu kwa kujuana, mnaweka watu wanaokwenda kuuza sura tu.


Ni jambo la kusikitisha kuona kuwa wachezaji walioteuliwa walishindwa kuonesha ubabe wowote katika hatua ya kufuzu, wakifanikiwa kushinda michezo mitatu pekee kati ya mechi saba, huku tukipokea vichapo vizito kutoka kwa Libya na Morocco.
1758264784065.jpg


Wakati huo huo, mashabiki na wadau wa michezo ya PlayStation wanashangaa ni vipi vijana wenye vipaji vikubwa kutoka maeneo kama Magomeni, Tabata, Ilala Dar es Salaam, Ngarenaro Arusha, au Dampo na Rufiji Mwanza, hawakupatiwa nafasi ya kupita ili waiwakilishe Tanzania?
1758264779972.jpg


Mitaani, mabingwa hawa wa eFootball huchukua timu ndogo kama Wolverhampton ama Sunderland na bado wanaweza kuwapiga mabingwa wanaotumia *Real Madrid au PSG kwa mabao mengi. Ni kiwango cha juu cha ubunifu, mbinu, na akili ya kiufundi ambacho kingeweza kuipa Tanzania heshima kubwa kimataifa.

1758264773224.jpg


Kwa nini TFF imeshindwa kuona dhahabu hizi mitaani? Sasa ni wakati wa kuachana na hizi mambo za kujuana na kuanza kuthamini vipaji halisi vilivyo mitaani ili taifa lisijikute tena likidhalilika. Nendeni mitaani mkakutane na Master PS wamejaa sio hawa wauza sura kwenye TV.
 
Tatizo mambo yetu Local sana hao wa mtaani wangekua wanacheza online tupate stats halisi za wachezaji bora Tanzania, lakini pia tunahitaji mashindano ya PS kwenye ngazi za mikoa tupate kikosi bora cha nchi.
Yaah kabisa mkuu, mpira wa miguu tushatoka kapa japo tunatumia mabilioni kujikakamua.

Ila kuna michezo ambayo haitiliwi macho ila wachezaji wake wanafanya vizuri.
Hata kitu kama PlayStation nacho kweli tunakosa kutoka kimasomaso.
 
Game kitambo toka 2004 PS1, PS2,PS3,PS4, PS5 kote huko ni hatari hawa waarabu koko hawazuii sare hata michezo 20, kule mbeya nimewanyoosha sana walikua wananiona kama jini kwenye ps2 nilikua napiga mabingwa wao huku nikiwafunza mbinu

Kuna mwanang yeye ndo ajira yake hiyo na anamke na watoto, asubh anaamka zake anatembea vijiwe vyote vya ps kucheza kamali hapo dar
 
Back
Top Bottom