TFF kufufua mashindano ya FA msimu wa 2014/2015

TFF kufufua mashindano ya FA msimu wa 2014/2015

mkolaj

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2014
Posts
3,023
Reaction score
1,093
Chini ya uongozi wa Jamal Malinzi pale tff wameamua kufufua tena yale mashindano yenye msisimuko kuliko ligi kuu namaanisha mashindano ya FA.Mashindano hayo yataanza kutimua vumbi mwez novemba mwaka huu na yatahusisha timu zote zilizosajiliwa....mashindano yamedhamiwa na mfuko wa ukuzaji mpira wa fifa ila wadhamin wengine wanakaribisha pia katika kufadhil mashindano haya il yawe na msisimuko zaidi....Habar hiz zimetoka ndan ya tff...
Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Mashindano wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Martin Chacha amesema wanatarajia mashindano ya Kombe la Chama cha Soka (FA) kuanza Novemba.

Akizungumza na Mwananchi, Chacha alisema kufanyika kwa mashindano hayo kunategemea msaada watakaopata kutoka Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) pamoja na kupata wadhamini wa ndani.

“Tumejipanga mashindano yaanze Novemba, lakini hatuna uhakika sana tunawasubiri kwanza Fifa, kwani walipokuja hivi karibuni tulizungumza nao kuhusu jambo hilo na waliahidi kutusaidia.

“Tunataka mashindano yakianza yawe bora kwani nia ni kupata bingwa wa uhakika ambaye ataiwakilisha nchi kwenye Kombe la Shirikisho Afrika, hivyo hatuwezi kukurupuka na kuyafanya mashindano hayo pasipo maandalizi hasa katika upande wa wadhamini.”

Naye ofisa mtendaji mkuu wa Bodi ya Ligi, Silas Mwakibinga alisema: “Tumejipanga vizuri ndiyo maana umeona hata ratiba tuliyotoa ni nzuri kulingana na mazingira yaliyopo kwani tumetoa nafasi ya kupisha michuano ya FA ambayo itafanyika hivi karibuni pia tumezingatia na umbali wa timu zinaposafiri kwenda mkoa mwingine kucheza mechi.”

Chanzo:Mwananchi
 
Back
Top Bottom