TFF kilichoshindikana kwa Tuisila Kisinda kiliwezekana kwa Perfect Chikwende (double standard)

Kumbuka ilikuwa wakati wa usajili wa dirisha dogo. Chikwende alishacheza michuano ya CAF akiwa na timu yake ya Platnum hivyo Simba wakamsajili kwa ajili ya ligi Kuu tu.
sasa kwanini KAHATA jina lake lilitolewa katika wachezaji wanaocheza ligi kuu?
 
Yanga ni kusanyiko la majuha ndiyo maana viongozi wako kimyaaa baada ya kuona wamechemka sasa hawa kina kajambanani wamechukulia upotoshaji wa Haji Manara kuwa ndiyo sheria. Haji ana mission yake maalum kuthibitisha kile alichowahi kusema kuwa huko Yanga wenye akili timamu ni Sunday Manara na Mzee JK tu.
Waende tena CAS
 
Na yule mropokaji Haji Manara ndiye anazidi kuwavuruga kwani hata wachangiaji wengi humu wananukuu kauli za upotoshaji za Haji Manara.
Kwahiyo hao Mashabiki wao hata kale kaufahamu ka kujua tu kwamba hapa viongozi wetu wamechemka wao hawana ?

Basi , kama ni hivyo haji keshawaona ni mazezeta anajidanganyia kadri anavyoweza.

Sent from my Infinix X612 using JamiiForums mobile app
 
Mwaka huo kanuni zilikuwa zinaruhusu wachezaji 12 CAF na wachezaji 10 wa ligi ya Bara, kwa hiyo ukipeleka majina ya wachezaji 12 TFF inabidi useme nani akatwe. Kanuni za mwaka huu zimebadilika kwa upande wa TFF, na zimeruhusu kusajili wachezaji 12 sawa na wa CAF. Sasa ukipeleka majina 13, huyo aliyezidi atacheza ligi gani? Na kama haujasema nani akatwe, si anakatwa wa mwisho? Au ulitaka TFF ichague yeyote ili Tuisila aingizwe, je TFF ingemchagua Mayele, si mngeenda hadi kwa Mama Samia? Kwa nini msikate wenyewe?
Sio kweli kanuni za caf ziko wazi,unaweza kuoeleka hata majina 40 ya wachezaji
IMG-20220905-WA0014.jpg
 
lilitolewa ili wabaki wachezaji 10 tu wa kigeni kucheza ligi kuu kama kanuni zao (TFF) zinavyotaka.
Hawataki elewa hilo hata hii 40 ya caf ndo iwe tiketi ya kulundika wachezaji zaidi ya 12, na kahata ile mechi simba anafungwa zimbabwe alikuwepo,chikwende kaja dirisha dogo wasubiri december kimfukuza huyo majeruhi kambole
 
Kuna swali najiuliza, hivi team ikisajili mchezaji na kabla ya deadline huyo mchezaji huyu akawa mgonjwa, inamaana hairuhusiwi tena kusajili mchezaji mwingine kabla ya hiyo deadline?

Kama ni ndio basi kuna mahala kanuni zetu hazipo vizuri.

Sipo hapa kusema nani yupo sahihi nan ani hayupo sahihi ila kwa namna hii team ya Yanga ninaweza kuipongeza kwa kuibua mapungufu katika kanuni zetu. Kwanini?

Haiwezekani mchezaji amesajiliwa katika muda sahihi na kufuata taratibu zote halafu iwepo kanuni ya kumzuia mchezaji huyo. Hiyo kanuni itakuwa na mapungufu makubwa sana au itakuwa imewekwa kimtego kwajili ya ‘’watu flani’’ na kwa bahati mbaya watu hao wameingia kwenye kumi na nane za ‘’watawala’’ ambao kwa siku za hivi karibuni wanasema wanaongoza kwa mawazo yao na si kanuni. Kanuni hutumika tu pale “unapoonekana kushindana na mamlaka.”

Kwanini?

Ni vile tu tumekuwa wasahaulifu sana hasa hawa ndugu wa TFF wamekuwa wasahaulifu mno kupindukia,

Mwaka jana 2021, katika usajili wa dirisha dogo, SIMBA SC ilimsajili Perfect Chikwende na kufanya idadi ya wachezaji wa kigeni kufikia wachezaji 13. Kilichofanyika Francis Kahata akatolewa kwenye usajili wa ligi ya ndani halafu Perfect Chikwende jina lake likaingizwa. Francis Kahata akasajiliwa kwenye mashindano ya kimataifa tu. Kitu ambacho this time around Yanga wamefanya hivyo hivyo.

Lakini wakati huo hatukusikia TFF ikikataa usajili huo.

Wachambuzi wenye ‘mbambamba’ nyingi kama akina Juma Ayo, Jemedari Said na Wilsom Oruma hatukuwasikia pia katika uchambuzi wa kujifanya wanajua kutetea sheria kama wanavyotetea sasa.

Hivyo hapa inaonekana kuna ‘ajenda’ ya siri kama ‘mungu mtu wa mpira’ alivyosema ukishindana na mamlaka wewe ndio utakaye umia. Ni wazi kuna watu wameanza kupata maumivu kwasasabu sheria ileile inayoibana team B sasa haikumbana team A.

Swali la msingi ni kujiuliza tu hizi sheria ni kwa team zote au kwajili ya team flani flani?
Chikwende alisajiliwa dirisha dogo
 
yea kimsingi TFF haitaki tena trick ambayo simba waliitumia kwa chikwende, yanga wanataka watumie ile trick, ndio maana kuna hayo malalaiko,
hakukuwa na trick ndiyo maana Simba iliongeza wachezaji wengine kama vile yule beki Muduwa na mmoja simkumbuki jina waliosajiliwa kucheza michuano ya CAF tu na siyi ligi kuu.
 
Sababu caf waliweka sheria ya dharura ya covid 19 siyo kahata tu, kulikuwa na beki wa zimbabwe peter muduhwa na lokosa jr pia walikuwa kwa ajili ya caf games,sheria haipo tena labda caf waliitoa kwa kuionea wivu yanga
Hiyo sheria ya COVID ipo bado na kama haipo ni lini ilikuwa abolished?
 
Ilishawahi kutungwa kanuni ya bench la timu kuto vaa vipensi, Hii ikitokea baada ya aliyekua kocha wa Yanga kuwa ana vaa pensi akiwa uwanjani, Tff hii hii ya Karia, Baada ya Zahera kuondoka Yanga kwasasa kanuni iyo haifanyikazi, Matola kocha wa Simba anavaa pensi na abugudhiwi.
Matola ni head coach?
 
Back
Top Bottom