Askari Muoga
JF-Expert Member
- Oct 22, 2015
- 6,113
- 4,655
Katibu Mkuu wa TFF, Mwesigwa Celestine, amesema kamati hiyo itakaa tena na kuna shahidi wengine wataitwa kuhojiwa.
Kikao hicho kimefanyika kuanzia leo asubuhi katika hoteli ya Protea jijini Dar es Salaam na waamuzi, wafanyakazi wa bodi ya ligi, viongozi wa simba, Kagera Sugar, waamuzi wa mechi kati ya Kagera Sugar dhidi ya African Lyon na beki Mohammed Fakhi wamehojiwa.
Baada ya kuhojiwa, kilichofuatia lilikuwa ni suala la kamati kukaa kwa takribani saa moja kuonyesha walikuwa wakimalizia kuhusiana na kile walichowahoji wahusika.
Kabla, kamati ya Saa 72, ilikuwa imeipa Simba pointi tatu na mabao matatu licha ya kufungwa kwa mabao 2-1 dhidi ya Kagera Sugar.
Kamati ya Saa 72, ilibaini Kagera Sugar ilimchezesha Fakhi mechi hiyo kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba akiwa na kadi tatu za njano.
Lakini Kagera Sugar wakaendelea kusisitiza kwamba Fakhi alikuwa na kadi mbili tu za njano alizopewa katika mechi ya Mbeya City na ile dhidi ya Majimaji na si dhidi ya African Lyon