The hammer
JF-Expert Member
- May 17, 2011
- 2,396
- 1,784
Leo kuna michezo kadhaa imechezwa ya ligi kuu Tanzania bara.Kuna mapungufu niliyoyaona ambayo kwa sasa imekuwa kawaida sana katika soka letu hapa Tanzania.Mchezo uliochezwa pale mwanza kati ya Total African na Azam haukuwa mchezo wa ushindani bali ilikuwa nani anaweza kucheza kwenye maji.
Uwanja ulijaa maji sana kiasi kwamba ule mchezo ungetakiwa uchezwe kesho.Hivi kuna tatizo gani kuahirisha mchezo kama ule unaochezwa kwenye maji ya namna ile...Je kuna mashindano yoyote ya CAF yanaweza kuchezwa kwenye uwanja uliojaa maji kama vile?
Mpira wa miguu ni burudani na mashabiki na wapenzi wa mpira na kuona vipaji vya wachezaji na si kutafuta point tu,pale mshabiki anafurahia nini,unapima uwezo wa mchezaji vipi pale,kiwango cha timu pale unakipimaje.Hivi timu ya daraja la iv si ingeweza kuleta ushondani mzuri katika moja ya timu zile zilizokuwa pale uwanjani na kuleta matokeo ambayo si halisi katika mpambano katika uwanja mkavu?
Msimu uliopita Azam ilimaliza mchezo wake wa ligi kuu kwa mtindo huo huo,ina maana imekuwa kawaida na hakuna maamuzi ya kuahirisha mchezo.Ni sababu zipi zinapelekea mchezo usiahirishwe katika hali kama ile?